Wanaolalamikia tozo ya jengo nahisi hawana uelewa au sio wazalendo

Wanaolalamikia tozo ya jengo nahisi hawana uelewa au sio wazalendo

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Mimi mara ya kwanza nilikua mpingaji mkubwa wa tozo ya jengo, nilipinga sana nikwa najiuliza kwanini tulipie kodi ya jengo hata ambao tumepanga.

Lakini baada ya kujifikiria kwa kina nimeona huu ni upuuzi watanzania tumezoea kulalamika hovyo.

Nimebadilika ninaunga mkono.

Just imagine wabongo unakuta jengo moja wapo wapangaji hata watano ila wote kwa pamoja hawataki kulipa buku kwa mwezi, na muda huo huo wanataka serikali iwape huduma bora za jamii.

Watanzania tubadilike sina hakika kama kuna mtanzania aliyepanga nyumba nzima au anayemiliki nyumba eti anakosa buku kwa mwezi, au sio kwamba akitoa buku kwa mwezi itamuathiri uchumi.

Wapangaji wetu wa uswahili ndo kabisaa nyumba moja wapangaji tisa kweli wote kwa pamoja mshindwe kulipa buku kwa mwezi?

Mambo mengine tuache kulalamika ni heri tulalamike endapo tukiona hela hiyo inatumika vibaya serikalini.

Hii nchi itajengwa na wananchi.
 
Uzulumati mwingine kama ule wa NSSF Fao la kujitoa....
We kula bure tu kwa Shemeji yako
 
Tozo ziegemee kwenye kumkamua Mwananchi!!

IMG_20210821_145411.jpg
 
Mwisho utatuita wapinga Tozo waRundi wasiotakia mema nchi hii 🤣🤣
 
Napendekeza na VAT iongezewe kutoka 18% mpaka 25% ili tusonge mbele kwa kasi zaidi
 
Back
Top Bottom