Wanaolalamikia Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya tuongee hapa kidogo

Ishu wengi wanatokea dar
 
Mtangazaji wa radio kuwa mkuu wa wilaya POA, Ila asije akaongoza kikao cha kamati ya ulinzi ya wilaya kama anavyosoma taarifa ya habari.
 
Kiukweli mama katika hili amechemka, ni miongoni mwa teuzi mbovu zaidi za maDC kuwahi kufanywa hapa Tz.

Yaani wilaya yenye wakazi wa kudumu zaidi ya Laki mbili, hivi rais anakosaje kuokota hata mtu mmoja miongoni mwao mwenye uzoefu, uadilifu, busara na rekodi nzuri kwa umma ili kuwatumia wananchi wenzake?

Yaani mama Samia anakwenda kuokota watu huko kwenye mitaa ya Dar na Twitter, waigizaji, malaya wa miss Tz, watangazaji, wasaliti wa siasa, makada wa CCM kwenda kuwaongoza wengine! Huku nikuwadharau watanzania.

Ni bora hata kumchukua mwalimu mkuu mzoefu na muadilifu wa shule ya msingi mojawapo katika wilaya husika kuwa DC wa wilaya hiyo hiyo kuliko kuokoteza watu popote hapa Tz kwa umaarufu nk.
 
Ningependa kuona nyuzi zenye kudai KATIBA mpya,zikiwa nyingi.Kuweni siliasi basi
 
Katiba ndo mwarobain ya yote ,teuzi za Rais zimekua nyingi MPAKA kichefuchefu, nafasi zingine mfano U - DC n.k zinafaa watu kuingia kwenye kinyanganyiro na wapigiwe kura au zikae kiutumishi ,mfano watendaji wa kata ,maafisa tarafa, hata wakurugenzi ina bidi ,maana ni nafasi zinazo gusa wananchi wa chini moja KWA moja ,

Sasa tz Rais anateua KWA mjibu wa katiba iliyopo MPAKA Basi , halikubaliki , unateuwa MPAKA unaondoka madarakani hata uliowateuwa humjui ata mmoja ,vituko sana
 
Wakuu wa shule, maafisa elimu, madaktari, ma afisa kilimo wangapi wamepata uteuzi? Au hao nafasi yao ni kuongozwa na tu form IV twenye certificate ya journalism na wakimbiza mwenge
 
Kwa cheo cha Mkuu wa Wilaya hata Stive Nyerere sawa tu. Taabu kwa DED hapo ndo nasubiri kuona uhalisia na mwelekeo wa serikali. Humo nikiwakuta kina JB nitajua tumepigwa.
Jmha ha ha ha
 
aisee umewachana Thadei. Watakuchukia sana.
 
Wakuu wa shule, maafisa elimu, madaktari, ma afisa kilimo wangapi wamepata uteuzi? Au hao nafasi yao ni kuongozwa na tu form IV twenye certificate ya journalism na wakimbiza mwenge
ila hili nalo. Kutokana na uzoefu nchi yetu imezidi kuporomoka ikiwa mikononi mwa hao wenye elimu na weledi. Ngoja mama ajaribu nje ya mipaka hiyo.
 
Maisha ya kutumwa na kuelekezwa kila muda ndio kitu sipendi nataka kutumia brain yangu kufanya maamuzi na kazi bila
Kuwa makini nakauli zako. Niki wa pili aliongea na kuchonga sana zaidi ya haya. Yako wapi sasa?
 
Daah I support CCM Ila sio Kwa kutuletea mtu kama mchopanga , Niki wa pili na Basila Mwanukuzi,

Jamani inamaana huko mitaani hakuna watu competent??

No wonder why nchi yetu ni masikini mwaka wa sitini huu,

Maana hatuna viongozi wenye ubunifu wa kutatua changamoto zetu.

Inasikitisha mno.
 
Hii nchi nazani baada ya Nyerere hatujawahi tena pata kiongozi seriouse, tuna bahati Mbaya mno tofauti na nchi zingine
The grass are always greener on the other side! Hata hao "nchi zingine" wanaona bora kwetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…