#COVID19 Wanaolaumu sera ya “maambukizi sifuri” ya China hawaelewi mazingira ya China

#COVID19 Wanaolaumu sera ya “maambukizi sifuri” ya China hawaelewi mazingira ya China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111355635280.jpg


Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari za nchi za magharibi vimejaribu kuibeza China kwa kusema sasa itabaki peke yake kwenye iliyokuwa ngome ya nchi zinazotekeleza sera ya maambukizi sifuri ya COVID-19, baada ya nchi nyingine zilizokuwa kwenye ngome hiyo (Australia, Korea Kusini, Japan nk) kuanza kulegeza hatua za zuio na kufungua mipaka yake. Pamoja na kuwa waandishi wa habari hizo wanaonekana kuifahamu vizuri China, lakini inaonekana kama kuna mambo mengi ya maisha ya kawaida kila siku kuhusu China wameyapuuza, kama hawajapuuza basi ni kunishambulia China bila msingi.

Kwanza, tukiangalia hali halisi ya miji mikubwa ya China, tunaweza kuona mazingira hatarishi ya kuenea kwa virusi ni mengi zaidi kuliko ilivyo kwenye nchi nyingine duniani. China ni moja ya nchi zenye majiji makubwa (Megacities) ambayo wakazi wake wengi wanatumia usafiri wa umma. Endapo mtu mmoja mwenye maambukizi akitumia usafiri wa umma kwa siku mbili au tatu kwenye moja ya miji mikubwa, uwezekano wa mamia ya watu kuambukizwa ni mkubwa.

Na hii sio kwa mji mmoja tu, inaweza kuwa kwa miji mingi hasa ikizingatiwa kuwa kuna usafiri wa mara kwa mara kati ya miji nchini China. Kwa hiyo kwa nchi kama China, gharama ya kuzuia maambukizi hayo ni ndogo sana ikilinganishwa na gharama inayoweza kutokea baada ya watu milioni moja kuambukizwa. Hali hii ni tofauti na ilivyo kwenye nchi nyingi za magharibi, ambako wengi hutaumia usafiri binafsi, na miji yao haina watu wengi kama majiji makubwa ya China.

Pili, labda ni uelewa mbaya wa sera ya “maambukizi sifuri”. Kwa jinsi China inavyotekeleza sera hii, haina maana kuwa China hakuna watu wanaoambukizwa. Si mara moja au mara mbili, kuna mawimbi ya watu walioambukizwa yanazuka. Lakini kinachofanyika ni kuwa kila maambukizi yanapotokea, hatua zinachukuliwa haraka kupambana na hali hiyo, bila kujali ni nani aliyeambukizwa. Hii ni tofauti na hali katika baadhi ya nchi za magharibi, ambazo zimeamua kuchagua virusi vienee na kupata kinga jumuiya (Herd immunity). Lakini hiyo inayoitwa kinga jumuiya kwa upande fulani inaonekana kama ni njia ya kunyoosha mikono na kukiri kushindwa kupambana na virusi, na kwa upande fulani ina ukakasi kidogo kwani maana yake ni kuacha ugonjwa huo uwashambulie watu wote, uwaue watu dhaifu na watu wale wenye nguvu wapone. Ilichofanya China ni kuwalinda watu wote waliopo China kwa usawa, na sio kuacha wadhaifu wafe kwa ugonjwa huu.

Tatu, kutokana na uzoefu wa China kwenye kupambana na magonjwa ya kuambukiza kama vile ugonjwa wa SARS, mamlaka za China zinafahamu kuwa kuacha virusi vienee bila kuchukua hatua yoyote, kuna madhara makubwa ya kiuchumi na kijamii. Kuna baadhi ya nchi zilijaribu kufanya hivyo matokeo yake ni kuwa kila kukicha tulikuwa tunasikia idadi ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa huo inaongezeka siku hadi siku. Kwenye nchi zilizochagua kinga jumuiya, shinikizo kwenye mfumo wa afya na uchumi lilikuwa kubwa, lakini kwa China shinikizo lilikuwa na muda mfupi tu.

Hata hivyo ni busara kukumbuka kuwa kila nchi inapambana na janga la COVID-19 kwa njia zake kulingana na mazingira yake. Uamuzi wa nchi moja kuamua kufungua mipaka yake na kuondoa hatua za zuio, hauna maana kuwa nchi nyingine zifuate hivyo.
 
Hao macho ndogo wanaendelea kula panya,popo,nyoka etc kila mdudu km kawaida huko mitaani.

No mercy magonjwa yanajirudia kila siku.

Upuuzi wao huo ndio umetuletea maradhi hayo miaka hapa duniani.

Wafe tu kwanza watupunguzie shida.

Na mnapokea chanjo kwa gonjwa wameanzisha wenyewe.
Amazing
 
WHA is your take home message?

Ujue kwa usiri wa udikiteita wa china hakuna anayejua ukweli wa kinachotokea china maana one can not report anything except the government
 
Hao macho ndogo wanaendelea kula panya,popo,nyoka etc kila mdudu km kawaida huko mitaani.

No mercy magonjwa yanajirudia kila siku.

Upuuzi wao huo ndio umetuletea maradhi hayo miaka hapa duniani.

Wafe tu kwanza watupunguzie shida.

Na mnapokea chanjo kwa gonjwa wameanzisha wenyewe.
Amazing
Ni sisi tuliokubali kuendeshwa na Msukuma mshamba anayejifanya kujua kila kitu. Akatuma profesa wa sheria akalete dawa Madagascar. Mawaziri wake wakakaa mbele ya vyombo vya habari wanatafuna tangawizi. Sisi ni wasenge sana kwenye ku deal na Covid.

China na watu wao 1.4 billion wameonyesha faida ya kutumia logic kwenye ku deal na covid na kama wamefanikiwa basi wapewe hongera na tujifunze vingi kutoka kwao.
 
Ni sisi tuliokubali kuendeshwa na Msukuma mshamba anayejifanya kujua kila kitu. Akatuma profesa wa sheria akalete dawa Madagascar. Mawaziri wake wakakaa mbele ya vyombo vya habari wanatafuna tangawizi. Sisi ni wasenge sana kwenye ku deal na covid.
China na watu wao 1.4 billion wameonyesha faida ya kutumia logic kwenye ku deal na covid na kama wamefanikiwa basi wapewe hongera na tujifunze vingi kutoka kwao.
Unapokua hujaelewa naongea nini usiniquote.
Case closed
 
Last paragraph nimeipenda.kila nchi inatumia mbinu zake kupambana na huu ugonjwa ,hivyo sio lazima kufuata anachofanya mwingine
 
Back
Top Bottom