Wanaomkandia Hayati Magufuli ni watukufu au waovu? Ni mafisadi au wema? Ni wazembe au wavivu?

Wanaomkandia Hayati Magufuli ni watukufu au waovu? Ni mafisadi au wema? Ni wazembe au wavivu?

Hapana nakataa kabsaa wachilia mbali Madhaifu ya JPM,ila jamaa alitaka kuibadilisha Tanzania sema kwa sababu hii Africa kuna watu wanataka wengine wapate na wengine wakose ndo kinachotuumiza sana.Hakukuwai na hakutowai kuwa na Rais kama JPM.
Mfike mahali muujue na kuukubali ukweli. Ipo wazi tu mengi ambayo watu wanalalamika kuhusu magufuli. Mfano tu wa mtu kama Sabaya liyepora watu mabilioni na kuwaumiza kwa vipigo na vifungo visivyo halali, mtu huyu alionekana safi kabisa kwa magufuli licha ya ukatili wake. Huyu ndiye Magufuli unayemshabikia ambaye uongozi wake umeacha madonda makubwa kama kwa Lissu na hata vifo kama vya akina Saanane na Azavor Mgwanda.
 
Mfike mahali muujue na kuukubali ukweli. Ipo wazi tu mengi ambayo watu wanalalamika kuhusu magufuli. Mfano tu wa mtu kama Sabaya liyepora watu mabilioni na kuwaumiza kwa vipigo na vifungo visivyo halali, mtu huyu alionekana safi kabisa kwa magufuli licha ya ukatili wake. Huyu ndiye Magufuli unayemshabikia ambaye uongozi wake umeacha madonda makubwa kama kwa Lissu na hata vifo kama vya akina Saanane na Azavor Mgwanda.
Sabaya bado yupo ndani najua Gereza la karanga pale Moshi,kama kweli alifanya huo wizi na kuchukua hela za watu shida ni yake na family waliemlea hivyo haiusiani Na JPM,ila kesi za Sabaya nyingi za kubambikizwa ndo mana jamaa any time atatoka,Na serikali ingeshamtoa ila inaogopa kukosa support kwa Chadema na lengo ni kuweza kupart hela za wafadhili.
Samia wenu yeye ni mikopo Samia ni wafadhili sjawai sikia hotuba yake yoyote anaongelea namna ya kufanya uzalishaji,kukusanya kodi kihalali,Hotuba zake ni "Tumezunguka tumepata wafadhili wamesema watatukopesha",Anajificha kwenye kivuli cha Democrasia ili akopeshweee. SABAYA ANAPATA SHIDA HUKO GEREZANI ILA ATATOKA.
 
WanaJF,

Heri ya Jumatatu! Mara nyingi sana nimesikia, nimesoma mengi juu ya uchafuzi wa image ya aliyekuwa Rais wetu JPM - wengine hujenga hoja dhaifu juu ya Katiba mpya (hawa wanaweza kuwa sahihi lkn tujiulize KIPINDI JPM ANAOMBA URAIS WAPI ALIPOAHIDI KULETA KATIBA MPYA? Aliahidi kushugulikia ufisadi na ndicho kilitokea!

Pili, aliahidi kushugulikia Miundombinu ya viwanja vya ndege ili akina Lissu, Lema, Zitto, Prof Lipumba, Mbowe, nk wapande ndege kwenda na kurudi nchini bila kikwazo - VIWANJA VILIJENGWA na wanufaika wakuu ni CDM, NCCR, ACT, CUF nk

Tatu, aliahidi kushugulikia Miundombinu ya Bwawa kubwa la umeme la Mwl Nyerere, Rusumo, Rea, na DARAJA LA BUSISI haya nayo yanaenda kukamilika - wanufaika watakuwa CDM, NCCR, CUF, ACT nk

Nne, aliahidi kufanya mageuzi ktk sekta ya madini leo kila wilaya ina soko na watu wanashughulikia masuala ya madini hapa pia wanufaika wakuu ni CDM, NCCR, CUF, ACT nk kwa kuwa RUZUKU mnazopata chanzo ni uimara wa mapato ya SERIKALI!

Tano, mengineyo - yapo mengi mazuri hatuwezi kuyataja yote hapa yaliyoanzishwa na JPM lkn CDM, NCCR, ACT, CUF nk hujitia upofu kama hawayaoni NI AIBU YAO leo wamekosa agenda na kukandya:-
(a) BODABODA
(b) Vikoba vya wanawake
(c) Wakulima wa avocado
(d) Watumishi wa umma!

Sisi CCM makundi hayo yote tumayachukulia kama mtaji wa kisiasa
CCM ni Tanzania!

Tanzania ni CCM.
Hao wote uliowataja na taasisi zao ni walipa kodi!! Na kodi zao ndizo zilitumika kujenga Nchi!! Wala hakuna pesa ilitumika binafsi!!
 
Back
Top Bottom