Wanaompenda vilivyo jamaa, wamwambie kuwa hapendwi wala hapendezi

Wanaompenda vilivyo jamaa, wamwambie kuwa hapendwi wala hapendezi

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Kuna watu wana ugonjwa wa ukosefu wa ubunifu kiasi cha kugeuzwa wadudu. Watu, sorry, wadudu hawa wana silaha moja tena ya hovyo.

Nayo ni kujikomba, kusifia hata ujinga, kujigongagonga, kutabiri upuuzi, kuimba pambio na mashairi tena wamuimbiaye akiwa kipofu na taahira. Je, hapa tatizo ni nini? Ni wale wasifuo au wale wasifiwao au wote? Kwani, nani asiyejua kuwa kizuri huwa chajiuza na kibaya chajitembeza? Nguruwe ni nguruwe hata apakwe lipstick. Juha ni juha hata aitwe msomi.

Fisi ni fisi hata avishwe ngozi ya kondoo. Nguruwe ni mchafu tu hata apakwe mafuta na kufukiziwa ubani na utuli. Cha hovyo ni cha hovyo hata kisifiwe vipi. Sijui kama kuna mavi au ushuzi mzuri. Mie sijui na sitaki hata kujua. Ubaya ni ubaya hata uitwe uzuri hauishi ubaya wake.

Uongo ni uongo hata uitwe ukweli na kuaminika, bado ni uongo tu. Ni mpumbavu apangaye kupaka rangi upepo. Sikieni maneno haya ya mwenye akili lau yawaweke huru. Mtumwa au wa kujituma au kulaimishwa ni mtumwa. Tofauti ni kwamba mtumwa wa kulazimishwa anaweza kujikomboa ilhali yule wa hiari anachukia na kuogopa ukombozi.

Huyu, hana tofauti na kuku atagaye mayai na kulishwa nafaka kavu ilhali mayai yake yenye virutubisho yakiliwa na wengine. Mbwa hulinda mali lakini yu maskini daima. Sindano hushona nguo ila siku zote i uchi. Ngoja niachie hapa kupiga kelele kimya kimya na kuwaza kichini chini wanangu.
 
Watu wanasumbuliwa na serikali inayoteka watu na ufisadi uliokithiri, wewe umejaza upupu ku deal na mtu mmoja asiye na impact yoyote kwenye taifa. Sometimes chuki binafsi zinaleta msongo wa mawazo. Rudia kusoma essay uliyoandika uone kama Ina umuhimu kwenye jamii.
 
Watu wanasumbuliwa na serikali inayoteka watu na ufisadi uliokithiri, wewe umejaza upupu ku deal na mtu mmoja asiye na impact yoyote kwenye taifa. Sometimes chuki binafsi zinaleta msongo wa mawazo. Rudia kusoma essay uliyoandika uone kama Ina umuhimu kwenye jamii.
Sijui kama unajua ulichoandika ukiachia mbali kujionyesha ulivyo chawa tena wa kunuka. Hata hivyo, nakushukuru kwa kuudhika na kuchangia. Kwani, nimemtaja nani huyo anayekuwashawasha hadi unaonyesha uzwazwa na uchawa wako? Hii, hii nimewaandikia wenye akili na wanafalsafa na siyo mafaala mwanangu.
 
Eti nguruwe ni nguruwe tu hata apakwe lipstick 😄 🤣

Nguruwe wetu amepakwa Wanja kudadadek
 
Back
Top Bottom