Wanaoongoza Kivuko cha MV Kazi (Magogoni -Kigamboni) leo 22/08/2024. Wachukuliwe hatua kali

Wanaoongoza Kivuko cha MV Kazi (Magogoni -Kigamboni) leo 22/08/2024. Wachukuliwe hatua kali

Wala sio uoga! mimi kuogolea najua.
Ila hawa jamaa wamefanya jambo la hatari.
Na Jioni watu waliokuwa wanavuka wengi mno
Kuogelea hauna ujuzi, kuna yule mkurugenzi ambaye sasa ni marehemu, yeye kila siku alikuwa anaogelea kutoka Kigamboni mpaka Feri, lakini siku ya siku yalimkuta maji yakamzidi na ukawa mwisho wake.
 
TEMESA na Mamlaka zote zinazohusika na Vivuko, Wanatakiwa kuwachukulia hatua kali sana, Waliokuwa wanaongoza MV Kazi leo 22-08-2024 Saa 12:50jioni. Kutoka Upande wa Dar (Magogoni) Kuelekea Kigamboni.

Wamehatarisha sana maisha ya watu.
Kivuko kimetoka Wakati kuna meli iliyokuwa inatoka bandarini.

Awali walisubiri lakini meli ilivyofika karibu na wao wakatoa Kivuko.
Hii ni hatari sana kwasababu Meli na Kivuko vilipishana kidogo sana!
Huku ni kukosa umakini na kuhatarisha maisha ya watu kwa kukusudia kabisa.

Chunguzeni hili jambo sio lakawaida.
Nimetoa hadi muda lilipotokea.

Nimetanguliza hii habari hapa ila kesho nitawasaka pia hao wahusika.

Waache masihara kabisa na maisha ya watu.
😁😁 Kumbe tulikua kwenye pantoni pamoja! Ila mbona meli ilipita fresh ingawa kweli leo wamezingua maana hata sea taxi ilichelewa kuondoka
 
😁😁 Kumbe tulikua kwenye pantoni pamoja! Ila mbona meli ilipita fresh ingawa kweli leo wamezingua maana hata sea taxi ilichelewa kuondoka
Mbona alisubiria fresh tu?
Halafu galfa akatoa chombo
 
Kuogelea hauna ujuzi, kuna yule mkurugenzi ambaye sasa ni marehemu, yeye kila siku alikuwa anaogelea kutoka Kigamboni mpaka Feri, lakini siku ya siku yalimkuta maji yakamzidi na ukawa mwisho wake.
Dah! akafia hapo feri?
 
Ulikuwepo mkuu?
Ulishaona hata mara moja Meli na Kivuko kusogeleana namna ile?
Nilikuwepo kwa juu, meli ilikua unatoka bandarini haikua na mzigo ni kweli aliondoka meli wakati inakuja ila hakuisogelea kiviile ingawa meli ilikua inatembea polepole sana tena sana
 
Wakuu tuko kwenye kivuko cha MV kazi tunazungushwa tu kwenye maji
 
MV Kazi Asubuhi hii 17.11.2024
Inatuzungusha majini tu hapa feri.
Tumepanda saa 11:43Asbh. Sasa ni saa 12:03Asbh.
Ni balaa sana, Tunazungushwa tu na hatujui hitilafu
 
Poleni sana ....pale juna waongoza meli na camera .....mamlaka bandari zichukue hatua ukute alilewa zake jana weekend na mazoea mabaya sanaaa
 
Back
Top Bottom