Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia

Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
aaa.jpeg

Wanaopaki magari muhimbili kuanza kulipia

5.4.2023
WANAOPAKI magari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili watalazimika kulipia ili kuondoka changamoto ya msongamano wa vyombo vya usafiri vinavyoingia hospitali hapo.

Profesa Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali hiyo, Profesa Mohamed Janabi, amesema utafiti uliofanywa na uongozi wa hospitali hiyo umebaini kuwa magari yanayoingia ni kati ya 3200 hadi 3800 kila siku ambapo yanayopaki wakati wowote ndani ya hospitali ni magari 1000 huku uwezo wa maegesho ukiwa ni 250.

Profesa Janabi amesema msongamano huo wa magari unasababishwa na wananchi kugeuza hospitalini kuwa eneo la maegesho kwani huacha magari yao ndani ya maeneo ya hospitali na kwenda kwenye shughuli zao.

“Tulipofanya uchunguzi ikabainika kuwa magari kati ya 400 hadi 600 wenyewe hawapo hospitali hali inayosababisha kuwa na magari mengi hivyo kuleta adha kwa wananchi wanaofika kupata huduma ambapo inamchukua mtu takribani dakika 40 kutafuta sehemu ya kuegesha gari lake” amefafanua Prof. Janabi.

“Wale wanaoleta wagonjwa na kushusha kisha kuondoka hawatalipa kwani mtu atapaswa kulipa tozo mara baada ya dakika 20 tangu aingie hospitalini. Pia fedha zitakazopatikana zitatumika kuboresha maegesho yaliyopo na kujenga mengine ya ghorofa ili kuegesha magari mengi zaidi ili kuondokana na usumbufu uliopo” amesisitiza Prof. Janabi

Prof. Janabi amebainisha kuwa tozo hizi za maegesho hazitahusu magari ya watumishi wa hospitali zilizo ndani ya Muhimbili, magari ya kubeba wagonjwa na magari ya serikali.

MY TAKE: Dakika 20 za gari kukaa ndani inatosha kushusha mgonjwa, kumpelek mapokezi, kulipa fedha, kupangiwa daktari na vipimo?

MAdiwani na uongozi wa HOSPITALI tunawapongeza uamuzi huu tutakuja kwa miguu, nyie mnaolipwa kwa kodi zetu mpate parking maana VX R ZA MILIONI 500 mlizonunuliwa na fedha zetu hazifai kukaa parking moja na vits za wanyonge.

Pia soma: Muhimbili sasa kulipisha tozo ya kuegesha magari
 
Tozo ya kijinga kabisa hospital zenyewe gharama kubwa harafu mnataka atoe hela kwa sababu ya kuja kumleta mgonjwa au kutibiwa Prof nakukubali ila hapo umeteleza sana baadae mtasema ili kupunguza msomango kwenye ward itabidi ndugu walipie kuangalia ndugu zao mnakoenda mnachukua miguu ya Mkoloni bila kujijiua...
 
Ni wizi huo kama wanavyotuibia huku nje ya mji hata ukipark tu kununua maji lazima ulipie parking
 
Nadhani wagonjwa wangepewa nafuu ukiwa na risiti ya siku husika usilipe tozo ya maegesho
 
Tozo ya kijinga kabisa hospital zenyewe gharama kubwa harafu mnataka atoe hela kwa sababu ya kuja kumleta mgonjwa au kutibiwa Prof nakukubali ila hapo umeteleza sana baadae mtasema ili kupunguza msomango kwenye ward itabidi ndugu walipie kuangalia ndugu zao mnakoenda mnachukua miguu ya Mkoloni bila kujijiua...
Kama umewahi uguza mgonjwa na akafia hapo MNH baada ya kutumia zaidi ya milioni 5 unaelewa, ila wasio elewa wanafikiri mzaha.
 
SEma kweli, unapaki kununua maji ya 500 unalipishwa 500/- yani bora ungeingia hoteli ya maana unywe ya buku 4 na internet free na parking free.

HAYA MAAMUZI YANAPITISHWA NA MADIWANI DARASA LA SABA WALIOPITA KWA KISHINDO na hizo fedha ZOTE ZINALIWA kama ripoti ya CAG ionyeshvyo.
Ni wizi huo kama wanavyotuibia huku nje ya mji hata ukipark tu kununua maji lazima ulipie parkinga
 
Kama umewahi uguza mgonjwa na akafia hapo MNH baada ya kutumia zaidi ya milioni 5 unaelewa, ila wasio elewa wanafikiri mzaha.
Tanzania pana vitu vinashangaza sana wengine wanauza mali ili kutibu ndugu harafu anakuja mtu mmoja anataka aongeze gharama ambazo baadae tutasikia kwenye Riport ya CAG kuwa wameiba hela za maegesho waamuzi huwa hawapendi kuwapunguzia mzigo wananchi wao kutwa ni kuwaongezea mzigo huku wenyewe wakitibiwa bure kabisa tena Nje ya Nchi...
 
WA

shaunda kundi lao linaitwa CHAWA PRO MAX, la kumsifia mama: Hawa wanalipwa kwa fedha zinazokwapuliwa huku, sisi ndio followers wa hawa wanaotufanyia haya, mwijaku anaingiza mamilioni kwa kumshangilia huko insta huku ametangaza kuwa mshangiliaji tu
 
Hizo dk 20 walizopewa wanaoleta wagonjwa ndogo sana,wangewapa hata saa 1...
Dakika 20 umepaki emergency, unaenda SEWA HAJI, upate mgonjwa alipo, daktari akwambie subiri tunamwogesha, aje, msalimiane, umpe uji na fanta, utoke kununua dawa, YAANI HII NCHI , kama MUNGU YUPO aamue ugomvi.
 
Back
Top Bottom