Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia

Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia

Na huu ndio ukomo wa fikra za wasomi wetu.

Yani uwezo wa fikra ni tozo tu kwa kila kitu. Hapo huyo Janaba atajisifu kuwa amekuja na bonge la source ya mapato kwa hospitali.

Ukienda hapo mpaka kumaliza huduma si chini ya masaa 6. Kwahiyo uhofie gharama za matibabu na parking pia?

Kesho Queen Matozo atasimama nae kuunga mkono hili swala kwa madai kila mtu achangie nchi. Yeye na wasaidizi wake wakiumwa wanapanda ndege kwenda ulaya.
 
SEma kweli, unapaki kununua maji ya 500 unalipishwa 500/- yani bora ungeingia hoteli ya maana unywe ya buku 4 na internet free na parking free.

HAYA MAAMUZI YANAPITISHWA NA MADIWANI DARASA LA SABA WALIOPITA KWA KISHINDO na hizo fedha ZOTE ZINALIWA kama ripoti ya CAG ionyeshvyo.
Yaani utoke mbagala au bunju kufuata hio parking free mjini
 
Kwani ukigoma kulipa hizi fee watakufanya nini, maana hadi uchochoroni . Hizi parking zifaa city center
 
Kwa msongamano ulivyo hapo mhimbili utamaliza kuhudumiwa kwa dakika 20?kila sehemu ya nchi hii ni tozo huku tozo zikiishia kwa mafisadi.Hii nchi inazidi kuharibiwa kila kukicha
 
😳🙄
Hivi kule nyuma ya hosp kwenye lile bonde lao walikokuwa wanafugia mbu mbona panatosha kabisa kujenga parking, kama kweli shida ni kupunguza msongamano wa magari.
 
Tozo ya kijinga kabisa hospital zenyewe gharama kubwa harafu mnataka atoe hela kwa sababu ya kuja kumleta mgonjwa au kutibiwa Prof nakukubali ila hapo umeteleza sana baadae mtasema ili kupunguza msomango kwenye ward itabidi ndugu walipie kuangalia ndugu zao mnakoenda mnachukua miguu ya Mkoloni bila kujijiua...
Ukilinganisha na wapi? Wewe si waenda South. Huduma zitazidi kuwa duni, kama hakutakuwa na uwekezaji kwenye taasisi kama za afya.
 
Ukilinganisha na wapi? Wewe si waenda South. Huduma zitazidi kuwa duni, kama hakutakuwa na uwekezaji kwenye taasisi kama za afya.
Umeelewa ulichokiongea au ndio wale wapiga makofi kwa kuwa wengi wamepiga makofi...
 
View attachment 2577341

Wanaopaki magari muhimbili kuanza kulipia

5.4.2023
WANAOPAKI magari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili watalazimika kulipia ili kuondoka changamoto ya msongamano wa vyombo vya usafiri vinavyoingia hospitali hapo.

Profesa Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji Hospitali hiyo, Profesa Mohamed Janabi, amesema utafiti uliofanywa na uongozi wa hospitali hiyo umebaini kuwa magari yanayoingia ni kati ya 3200 hadi 3800 kila siku ambapo yanayopaki wakati wowote ndani ya hospitali ni magari 1000 huku uwezo wa maegesho ukiwa ni 250.

Profesa Janabi amesema msongamano huo wa magari unasababishwa na wananchi kugeuza hospitalini kuwa eneo la maegesho kwani huacha magari yao ndani ya maeneo ya hospitali na kwenda kwenye shughuli zao.

“Tulipofanya uchunguzi ikabainika kuwa magari kati ya 400 hadi 600 wenyewe hawapo hospitali hali inayosababisha kuwa na magari mengi hivyo kuleta adha kwa wananchi wanaofika kupata huduma ambapo inamchukua mtu takribani dakika 40 kutafuta sehemu ya kuegesha gari lake” amefafanua Prof. Janabi.

“Wale wanaoleta wagonjwa na kushusha kisha kuondoka hawatalipa kwani mtu atapaswa kulipa tozo mara baada ya dakika 20 tangu aingie hospitalini. Pia fedha zitakazopatikana zitatumika kuboresha maegesho yaliyopo na kujenga mengine ya ghorofa ili kuegesha magari mengi zaidi ili kuondokana na usumbufu uliopo” amesisitiza Prof. Janabi


Prof. Janabi amebainisha kuwa tozo hizi za maegesho hazitahusu magari ya watumishi wa hospitali zilizo ndani ya Muhimbili, magari ya kubeba wagonjwa na magari ya serikali.

MY TAKE: Dakika 20 za gari kukaa ndani inatosha kushusha mgonjwa, kumpelek mapokezi, kulipa fedha, kupangiwa daktari na vipimo?

MAdiwani na uongozi wa HOSPITALI tunawapongeza uamuzi huu tutakuja kwa miguu, nyie mnaolipwa kwa kodi zetu mpate parking maana VX R ZA MILIONI 500 mlizonunuliwa na fedha zetu hazifai kukaa parking moja na vits za wanyonge.

Pia soma: Muhimbili sasa kulipisha tozo ya kuegesha magari
Safi sana
 
Back
Top Bottom