Kwa square metre moja ulitumia maji kiasi gani tokea uoteshe nyanya hadi uanze uvunaji
Hua ninalima matuta 6 yenye ulefu wa mita 28 kila moja tuta.kila tuta lina upana wa futi moja juu na mwinuko wa nusu futi au zaidi kutoka chini. Pia katika upana wa futi moja naweka miche miwili sambamba na kupitisha drip mbili kwa kila tuta toka mwanzo hadi mwisho wa tuta.
Nimeweka tank la maji la lita 2000 ambalo msimu wa kukua nyanya(miezi mitatu) huwa namwagilia mara mbili kwa siku(kufungulia bomba kwenye tank msimu wa jua ili kumwagilia ) ikisha isha msimu wa kuota huwa namwagilia endapo ntaona udongo umekauka sabab maji yakizidi nyanya huanza pasuka lakini kwa maelezo ya mtaalam alisema niwe namwagilia mara moja kwa siku
Mbegu ya nyanya nnayotumia ni anna f1 inayokua kwa miezi 3 na kuvunwa miezi 6 jumla huchukua miezi 9 hadi kukauka
Niende kwenye jibu sasa
Endapo nkifuata utalatibu wa kitaalamu wa kumwagilia mara moja kila siku msimu wa mavuno
2000*2*90=litres 360000 msimu wa kuota miezi 3
2000*1*180=litres360000msimu wa kuvuna miezi 6
(litres*awamu za kumwagilia kwa siku*siku)=litres
Jumla inatumia 720000 litres hadi unamaliza kitaalamu
Lakini icho kiasi ni kikubwa sana hata mi sikufikisha kwani nlikua namwagilia pale tuu ntapoona udongo mkavu
JIBU
Nlilima matuta6 yenye urefu m 28
6*28=168metres urefu
Upana ulikua futi moja ambayo ni kama 0.3metres
0.3*168=50.4meter square jumla ya eneo lote nlilolima
720000/50.4=14284.7litres per square
Uki round up ni kama 14000
Hivyo nlitumia litres 14000 kwa mita moja ya mraba
NOTE(IKUMBUKWE KUWA)
nyanya nliolima inatumia maji mengi sana kwani huzaa kwa wingi kwa watalamu nadhani mnaijua
Nyanya hii hukaa miezi 9 sio kama zile nyingine zile za 3 months
Huu ni ushauri wa kitaalamu nliopewa ingawa hizo lita hata mi sku fikisha
Msimu nliofanya ni kiangazi
Nyanya nyingi ziliasiliwa na fungus waliotokana na wingi wa maji kwenye udongo na kutofikisha mieZi tisa ila zote zilivuka miezi 6
Natumaini umenielewa