Wanaopenda kula kula kwani hamshibi?

Wanaopenda kula kula kwani hamshibi?

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Habari wadau,

Aisee wakuu, kuna watu wanapenda kula kula yani utakuta ratiba yake ya siku ameshakula makorokoro kibao.

Utakuta asubuhi saa 1 kanywa chai na kiporo , alafu ikifika saa 4 anakunywa supu na chapati 2, ikifika saa 5 anakula sambusa 2 na soda.

Ikifika mchana saa 8 anakula ugali na samaki na juice, ikifika saa 8 anakula karanga au keki ikifika saa 10 akikutana na muhindi anakula.

Usiku anakula tena lisahani la wali na nyama na juice.


Wadau nini chanzo cha kulakula kila saa? Ni ulafi au?
 
Ni kweli mkuu, ila wanakula ovyo kwanini wasile wakashiba kabisa..
Mazoea hujenga tabia mkuu walianza mdogo mdogo sasa ndio imekuwa tabia wanahitaji msaada wa kujitambua ili waache hiyo tabia
 
Mkiishi kwa kuwaza ya mengine ya kwenu mtayawaza sa ngapi?

Perhaps Trump aliyoyasema ni kweli
 
Mtu anaependa kula ujue mwili wake upo vizur

Kuna wengne wanataman wale ila wanaishia tonge moja tu

So usiubanie mwili
 
Kuna wengne hawawezi kula wakamaliza chakula, kwaio kula ivo mara kwa mara na kidogo kidogo kunawasaidia sana
 
Jitu unakuta umepanda nalo basi ktk safari mara limenunua mahindi ya kuchemsha linamenya maganda linakula.
Mara mishikaki, mara juisi daah alafu lina mwili mkubwa.
Hivi ni kwa nini mtu usile ukashiba halafu utulie!
 
Yaani I wish ningekuwa na mwili ambao haubadiliki nikila. Ningehamia jikoni aisee.
 
Jitu unakuta umepanda nalo basi ktk safari mara limenunua mahindi ya kuchemsha linamenya maganda linakula.
Mara mishikaki, mara juisi daah alafu lina mwili mkubwa.
Hivi ni kwa nini mtu usile ukashiba halafu utulie!
Kweli kabisa,mimi nikikaa karibu na mtu wa hivyo kwenye basi,Safari nitaiona ndefu sana.Yaani gari isisimame naomba nichukulie karanga,mara korosho,ndizi,maembe ,parachichi,chips,mahindi,kashata,bisi,Soda,maji,n.k.Huo mzigo unazidi hadi nauli ya kutoka Kgm_Dar kabisa.
 
Back
Top Bottom