Wanaopewa madaraka bila kupanga kuyataka hawana agenda

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na Mabwana mtu kuutaka Urais ni kwa sababu ana agenda. Ana agenda ya kufanya. Hiyo ndiyo tunapaswa kuisikia na hiyo ndiyo anayopaswa kutushawishi nayo.

Mtu anapewa vipi mamlaka na kisha kujinasibu kuwa hakutaka, hakujua, hakupanga wala hakutegemea?

Tunamchagua vipi mtu huyu? Anatushawishi au kutuvutia vipi huyu? Atatufaa vipi na kwa lipi?

"No wonder" tuko hapa tulipo. Tutabakia hapa hapa kama hatutaamka na kufanya maamuzi magumu ikibidi.

Kwa mustakabala wa nchi yetu tuna mkuluro wa mambo ya kuyakataa kwani huo ni wetu na uko mikononi mwetu:
1. Tukatae mazingira yoyote ya kutofuata katiba.
2. Tukatae mazingira yoyote ya chaguzi kuhujumiwa.
3. Tukatae chaguzi kutokuendeshwa katika mazingira yasiyokuwa huru, haki wala kuaminika.
4. Tukatae matamko ya watu kuwa ndiyo Sheria au katiba ya nchi.
5. Tukatae mamlaka kutolewa kwa ridhaa ya mtu badala ya ridhaa ya wapiga kura.
6. Tukatae wagombea kuenguliwa kwa sababu za kubumba bumba zisizokuwa na mashiko yoyote ya kikatiba.
7. Tukatae vyombo vya dola kuwa vyombo kandamizi.
8. Tukatae nk. nk.

Yapo mengi ya kukataa kabla hatujachelewa. Vinginevyo tunaweza kuta mkuu kabisa na uGIP nao kajimilikisha.
 
Kaa hapo hapo wasubirie MATAGA na UVCCM wanakuja kukupa vidonge vyako
 
Ni kweli kabisa, na ajenda yao kuu huwa ni kujitukuza na kulinda hayo madaraka yanayowapwaya!
... wamedandia gari chakavu alilowaachia mzee Nyerere, ... kazi kucheza na virungu ... leo nukuu hii, kesho nukuu hii ... SIKU ZINAKWENDA!
👊😅✌️
 
Je! Siku moja kabla ya kuandika uzi huu ulijua utacho kiandika? Ukinielewa hapa utaelewa mantiki ya profesa.
 
Hahaha anayepewa cheo na Rais hufanya kazi kwa manufaa ya Rais kwanini mtafute mchawi wa maendeleo yenu wakati mnamfahamu?!

Mtu anateuliwa na Rais ili amtumikie Rais kwa manufaa ya Rais, na ujira anaolipwa kwa kazi hiyo ni kwa tumbo lake na familia yake.

Rais asiyechaguliwa na wananchi hawatumikii wananchi bali anawatumia wananchi kujinufaisha yeye, kwa lugha iliyozoeleka ni mtawala wa kikoloni.

Rais hana ridhaa ya wananchi, anao wateua ni genge lake la kutekeleza matakwa yake ya kutawala, wanamtumikia yeye.
 
Njia pekee halali na kikatiba na kwa sanduku la kura. Kwa bahati mbaya njia hii imefungwa na wenye mamlaka na uwezo wa kufanya hivyo.
 
Kwani maumivu ya penicillin injection ya October 28th hayajapoa tuu?
 
Ukikua utaelewa madhara ya mtu anayeikimbilia ikulu kupewa nafasi ya urais.

Utaelewa rushwa inayokuwepo wakati mtu akiwa katika mchakato wa kutaka kuwa rais kwa kuanzisha makundi ya kumuunga mkono.

Utaelewa kuwa mshikamano wa Tanzania unatokana na busara za RIP Nyerere za kuwafanya watanzania wakayakwepa makundi yenye kuweza kuigawa nchi.

Ukikua utazijua historia za mataifa ya afrika na namna yamekuwa yakishindwa kuuelewa mtego wa siasa za makundi. Zenye kukubaliana na wenye majina makubwa kuwa na ushawishi wenye kuvunja moyo wa nchi.

Hakika ukikua utayajua mengi ya kisiasa.
 
Hii haitofautiani na Pesa za Madini enzi hizo ,uliishia kumiliki Mabeberu wa Kondoo leo unaokota Jiwe lenye thamani ya Mamilioni ya Shilingi.Tuna kodi mpaka Tax ya kubeba Kofia.
 
Ukikua utaelewa madhara ya mtu anayeikimbilia ikulu kupewa nafasi ya urais.

Utaelewa rushwa inayokuwepo wakati mtu akiwa katika mchakato wa kutaka kuwa rais kwa kuanzisha makundi ya kumuunga mkono.

Utaelewa kuwa mshikamano wa Tanzania unatokana na busara za RIP Nyerere za kuwafanya watanzania wakayakwepa makundi yenye kuweza kuigawa nchi.

Ukikua utazijua historia za mataifa ya afrika na namna yamekuwa yakishindwa kuuelewa mtego wa siasa za makundi. Zenye kukubaliana na wenye majina makubwa kuwa na ushawishi wenye kuvunja moyo wa nchi.

Hakika ukikua utayajua mengi ya kisiasa.

Ni kawaida kwa mazezeta kumnukuu mwalimu (rip) out of context ku justify upuuzi wao bila kujali degree.

Nyerere (rip) brilliant kama alivyokuwa angekuwa wa kwanza kuyakataa yote haya kama yalivoorodheshwa kwenye mada.

Mwalimu alikuwa mtu wa kushindanisha hoja. Mkimbia mdahalo asingeiona ikulu. Mkanyaga katiba angeisikia ikulu kwenye Bomba.

Bahati yao mwalimu hayupo.

Ama kweli, kufa kufaana!
 
Nyerere alituonya juu ya kuwaamini wanaokimbilia ikulu kwa kuhonga na wewe unawatetea.

Mdahalo wa Magu ni vitendo zaidi. Mdahalo wake ni kushughulika na shida za watu moja kwa moja.

Lissu ni fundi wa kuongea mbele ya kamera lakini kuwadi tu wa wazungu.

Mazezeta ni kama wewe unayeishi na maumivu moyoni, na hakuna wa kukusaidia.
 
Kwenda ikulu kwa kuhonga kumetokea wapi?

Agenda ni kuhonga.

Eti mdahalo vitendo - kuuwa na kuteka watu? Bure kabisa!

Kumbe zezeta wewe unadhani wewe siyo zezeta?

Maajabu ya firauni.
 
Mabibi na Mabwana mtu kuutaka Urais ni kwa sababu ana agenda. Ana agenda ya kufanya. Hiyo ndiyo tunapaswa kuisikia na hiyo ndiyo anayopaswa kutushawishi nayo.

Mtu anapewa vipi mamlaka na kisha kujinasibu kuwa hakutaka, hakujua, hakupanga wala hakutegemea?

Tunamchagua vipi mtu huyu? Anatushawishi au kutuvutia vipi huyu? Atatufaa vipi na kwa lipi?

"No wonder" tuko hapa tulipo. Tutabakia hapa hapa kama hatutaamka na kufanya maamuzi magumu ikibidi.

Kwa mustakabala wa nchi yetu tuna mkuluro wa mambo ya kuyakataa kwani huo ni wetu na uko mikononi mwetu:
1. Tukatae mazingira yoyote ya kutofuata katiba.
2. Tukatae mazingira yoyote ya chaguzi kuhujumiwa.
3. Tukatae chaguzi kutokuendeshwa katika mazingira yasiyokuwa huru, haki wala kuaminika.
4. Tukatae matamko ya watu kuwa ndiyo Sheria au katiba ya nchi.
5. Tukatae mamlaka kutolewa kwa ridhaa ya mtu badala ya ridhaa ya wapiga kura.
6. Tukatae wagombea kuenguliwa kwa sababu za kubumba bumba zisizokuwa na mashiko yoyote ya kikatiba.
7. Tukatae vyombo vya dola kuwa vyombo kandamizi.
8. Tukatae nk. nk.

Yapo mengi ya kukataa kabla hatujachelewa. Vinginevyo tunaweza kuta mkuu kabisa na uGIP nao kajimilikisha.
Barabara ya rusumo imefanyiwa matengenezo?
 
Kwenda ikulu kwa kuhonga kumetokea wapi?

Agenda ni kuhonga.

Eti mdahalo vitendo - kuuwa na kutaka watu? Bure kabisa!

Kumbe zezeta wewe unadhani wewe siyo zezeta?

Maajabu ya firauni.
Mazezeta ni watu kama wewe wenye kuwaza vitu ambavyo haviwezi kutokea Tanzania.

Mdahalo wa kazi gani wakati kazi anazo fanya ni mdahalo tosha?.

Sisi kama taifa tufuge uvivu halafu tutegemee uwezo wa rais kwenye midahalo kuwa ndio suluhisho la umaskini?. Huu ndio uzezeta wenyewe.

Siungi mkono mauaji lakini hakuna nchi labda ukiondoa Vatican ambayo haina wala haijawahi kuwa na mauaji au utekaji wa watu. Haipo hiyo nchi.
 
Back
Top Bottom