Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mfalme amesema: “Anayeonywa mara nyingi akawa mkaidi, ataangamia ghafla asipone tena.”
Naongea na wewe, unayepiga kampeni ili kuwafanya watu wakatae ndoa. Pole sana kwa changamoto ulizokutana nazo, zilizokusababishia “ugonjwa” wa kupiga kelele usiku na mchana: “kataa ndoa, kataa ndoa.” Unapiga kelele weee watu wakatae ndoa, lakini kila wiki unasikia ndoa zinafungwa zikiambatana na sherehe “babu kubwa.”
Katika kampeni yako unadai ndoa ni mzigo wa mateso na matatizo. Unawaambia watu waikatae ndoa eti wajiepushe na maumivu ya ndoa. Kinachoshangaza ni kwamba hukatai uzinzi na uasherati - mambo yenye athari mbaya zaidi kwako. Afadhali uteseke katika ndoa halafu mwisho wa siku uingie mbinguni kwenye raha ya milele, kuliko kukumbatia uzinzi ambao tayari hukumu yake imeishatolewa: kutupwa katika ziwa liwakalo moto milele.
Ngoja nikufumbue macho, wewe mwanaume, mkuu wa kampeni hiyo batili. Ulipoingia kwenye ndoa ulifikiri mwanamke hana ubongo. Ulifikiri mwanamke hana macho na masikio. Ulifikiri mwanamke hana miguu na mikono. Hujasoma kitabu cha Mwanzo? Mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu wa mwanaume. Hivyo anafanana na wewe katika mambo mengi. Ndio sababu ulipomuoa yule mwanamke kisha ukaanza kumpiga na kumtukana, ukifikiri ndio unamnyamazisha, yeye naye alijibu mapigo. Ulipopaza sauti yako kumtukana, yeye naye alifumbua kinywa, akakutusi tena mbele ya majirani. Ulipofikiria kumuacha, kwakuwa yeye naye ana ubongo, akakuwahi mahakamani, talaka akakupa wewe badala ya wewe kumpa; na akadai mali mgawane.
Ndugu yangu, kwakuwa nakupenda, na kwakuwa najua hiyo njia mbadala uliyochagua inakupeleka pabaya, ntakupa “dawa” unywe, utapona ugonjwa wako. Ukiinywa sawasawa, naamini siku moja utaomba kumrudia huyo mkeo uliyemuacha.
Dawa yangu ni hii: Ukiona ndoa ina changamoto, suluhisho sio kuikataa, bali ni kujifunza jinsi ya kutatua changamoto husika. Elimu ni bahari. Ili mtu ajue jinsi ya kuishi na mke anahitaji kwenda shule. Anahitaji kuhudhuria semina na warsha na makongamano yanayotoa elimu ya ndoa. Kwa maneno rahisi, ili ndoa idumu kuwa ya raha, amani na upendo, ni lazima wanandoa wawe na maarifa sahihi ya namna ya kuishi pamoja kwa maelewano. Hiyo ndo dawa.
Namshukuru Mungu, nina uzoefu na elimu inayoweza kuwasaidia watu wafurahie ndoa kama mimi. Niulize maswali ya ndoa uliyokosa majibu yake, ntajitajidi kukujibu.
Nakuonya tena: usikatae ndoa na pia acha kabisa kampeni yako batili, inayomchukiza Mungu. Mungu amesema “Ndoa iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi(Waebrania 13:4). Ukikataa onyo hilo ukaendelea na uzinzi na uasherati, moto wa jehanum unakusubiri. Kama hutaki ndoa, afadhali ukae hivyohivyo ulivyo bila kumgusa mwanamke.
1 Wakorintho 6:9-10 BHN
"Au je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi ufalme wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti, wezi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyanganyi, hao wote hawatashiriki ufalme wa Mungu."