Wanaopiga kampeni ya “Kataa Ndoa” waonywa!

Wanaopiga kampeni ya “Kataa Ndoa” waonywa!

Ni heri Mwanaume asimguse mwanamke ila kwa sababu ya uzinzi tunashauriwa kuoa". Kama Bible yenyewe inakataa kuoa mm nani????
Andiko unalosimamia ni 1 Wakorintho 7:1-9. Hilo halikatazi kuoa'
Hapo Paulo alikuwa anajibu maswali kutoka kwa Wakristo wa Korintho kuhusu ndoa na useja. Katika mstari wa kwanza, anasema:
“Ni vyema mtu asimguse mwanamke” (1 Kor 7:1)
Hii haimaanishi kuwa ndoa ni mbaya, bali Paulo alikuwa akizungumzia useja, yaani wanaoweza kukaa kama yeye wafanye hivyo kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hata hivyo anaendelea kusema:
“Lakini kwa sababu ya zinaa, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. (1 Kor 7:2)

Hii inaonyesha kuwa ndoa ndiyo suluhisho la tamaa za mwili. Ndoa ndiyo jambo linaloweza kumfanya mtu asianguke kwenye dhambi ya zinaa.

Katika mstari wa 7-9, Paulo anasema anatamani watu wote wawe kama yeye (yaani, waishi bila kuoa ili wawe huru kumtumikia Mungu). Lakini anakubali kuwa si kila mtu ana karama hiyo ya useja. Anaongeza:
“Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” (1 Kor 7:9)

Sasa unapowaambia watu wakatae ndoa wakati hawawezi kujizuia kukaa bila kuwagusa wanawake, huoni kuwa unawaingiza kwenye uzinzi?
 
Sasa hivi nina alcohol nyingi sana kichwani. Nikiamka kesho asubuhi nitaisoma vizuri thread yako. Mimi kama kaka yako nitakuelekeza vizuri wapi ulipokosea
Bado tu alcohol haijaisha kichwani. Nasubiri kusikia hoja zako
 
Rubbish talk.
Even rubbish serves a purpose—waste can nourish the soil, and discarded things can find new value. Likewise, meaningful discussions flourish through reasoned arguments, not mere dismissal. Thoughtful discourse requires substance, not contempt.
 
Bado tu alcohol haijaisha kichwani. Nasubiri kusikia hoja zako
Katika kizazi tulichopo ndoa ni concept ambayo tayari imeshapitwa na wakati. Muundo wa ndoa ulisukwa kwenda sambamba na mfumo dume, katika zama hizi za usawa wa kijinsia lazima taasisi ya ndoa itaanguka tu kwa sababu misingi yake haikuwekwa kwenda sambamba na haya mambo ya 50/50 na feminism.

Tuangalie masuala kadhaa yanayohusu ndoa ambayo yalikua na uhalali nyakati za mfumo dume lakini kwa sasa hayana uhalali tena.

1. Kugawana mali baada ya kutalakiana.
Katika zama za mfumo dume mwanamke hakujumuishwa kwenye masuala yote ya kiuchumi kuanzia kirithi mali, kumiliki mali, elimu n.k katika hali kama iyo ni haki kwa mwanamke uyo kupata mgao wa mali ndoa ikivunjika. Kwenye jamii ya sasa mwanamke kapewa uhuru na access zote za kujitafutia hela na mali kwaiyo hakuna sababu inayomlazimu awe tegemezi na kupata mgao kutoka kwenye mali za mwanaume.

2. Mmong'onyoko wa maadili ambao umefanywa kuwa ustaarabu wa maisha ya kisasa.
Wanawake wanatembea nusu uchi, wanapost picha chafu mtandaoni. Mambo ambayo mwanaume ulitakiwa kuyapata ndoani unayapata ukiwa bachelor. Maeneo ya mwili wa mwanamke ambayo ulitakiwa kuyaona chumbani unayaona mtaani na mtandaoni. Zamani uchi wa mwanamke ulikua priceless sasa hivi uchi wa mwanamke una price tag. if i can get free milk why keeping a cow?

3. Hakuna namna ya kumwajibisha mwanamke.
Nyakati za mfumo dume kulikua na standard rigid za kumwajibisha mwanamke. Mwanamke kukosa bikira ilikua aibu kubwa sana kwenye familia matokeo yake mabinti walijitunza mpaka ndoa. Sasa hivi tupo kwenye kizazi ambacho mabinti na wanawake wamepewa uhuru wa kufanya ngono kiholela bila kuwa accountable.
 
Asilimia karibia 90 ya walio oa na wana miaka zaidi ya 5 ya ndoa ukiwauliza kama wakirudi miaka 5 nyuma wanaweza kurudia kuoa?? Watakujibu hapana, wengi wamebaki kuishi kwenye maisha ya ndoa kinafiki kisingizio ni ‘watoto’. Upuuzi wa namna gani hii?? Niishi maisha yangu yaliyobakia bila amani ya moyo na utulivu wa nafsi kisa watoto?!!! Hell No
Inafahamika, kataa ndoa ni kundi la wanaume waliopoteza marinda na kubaki na kamba. Tuwahurumie tu, wamevurugwa na kupotezwa mwelekeo. Mbaya zaidi hawana maisha marefu kwa sababu ya kusononeka kila mara baada ya matundu yao kuharibika na kupoteza wateja. Pole yenu kundi la kataa ndoa.
 
Wakati watu wakiingia msalani wanaacha kinyesi chooni wewe ukiingia msalani unaacha akili unatoka na kinyesi kichwani, Pole.
 
Katika kizazi tulichopo ndoa ni concept ambayo tayari imeshapitwa na wakati. Muundo wa ndoa ulisukwa kwenda sambamba na mfumo dume, katika zama hizi za usawa wa kijinsia lazima taasisi ya ndoa itaanguka tu kwa sababu misingi yake haikuwekwa kwenda sambamba na haya mambo ya 50/50 na feminism.
Kwetu sisi tunaoamini Neno la Mungu, suala la ndoa halijapitwa na wakati. Bado tunakiri kama Maandiko yanenavyo kuwa ndoa na iheshimiwe. Bado tunatambua kuwa mwanaume ni kichwa cha mke. Na bado tunatambua kuwa Mungu anachukia kuachana(talaka). Hivyo hatuungi mkono kampeni za kukataa ndoa.

Kama concept ya ndoa imepitwa na wakati, kwanini ziwepo kelele za kuwaambia watu wakatae ndoa? Mambo ya ndoa si yangekufa tu yenyewe?

Mimi natambua Ibilisi yuko nyuma ya kampeni hii kwa sababu watu wakikataa ndoa ndio uzinzi utaongezeka zaidi, maana wanaokataa ndoa hawakai hivyo hivyo walivyo, bado wanatafuta wanawake. Na uzinzi ukiongezeka, shetani anafurahi kwa sababu anakuwa amepata watu wa kwenda naye katika adhabu ya moto wa milele.
 
Kero kwenye ndoa inaanza pale mwanamke anapoanza kufosi kufanyiwa vitu ili ajisikie kama ndio anatongozwa kwa mara ya kwanza.

Wanaume hatuna shida na excitements ila tunataka wanawake zetu wamaintain utulivu,maelewano na wawe na akili ya uelewa.

But shida ni mwanamke anataka kujifeel kama mara ya kwanza mlipofanya,mara ya kwanza alipokuona,mara ya kwanza mlipo kiss,mara ya kwanza mlipo toka out kitu ambacho ni kigumu sana matokeo yake ndio wanawake hutafuta mwanaume wa nje ili kupata ile feeling ya msisimko mpya wa kihisia.

Mwisho wa siku ndio unabakia kununiwa kila siku bila sababu. Hapo lazima uende nje kutafuta mali ya kukuliwaza.
 
Kwetu sisi tunaoamini Neno la Mungu, suala la ndoa halijapitwa na wakati. Bado tunakiri kama Maandiko yanenavyo kuwa ndoa na iheshimiwe. Bado tunatambua kuwa mwanaume ni kichwa cha mke. Na bado tunatambua kuwa Mungu anachukia kuachana(talaka). Hivyo hatuungi mkono kampeni za kukataa ndoa.
Hoja yako ungeiweka katika mlengo wa dini yako ungeeleweka zaidi yaani kama wewe ni mkatoliki walenge wakatoliki wenzako kwa sababu sio kila mtu anafuata au kuamini dini yako. Tanzania sio nchi ya kidini.
Kama concept ya ndoa imepitwa na wakati, kwanini ziwepo kelele za kuwaambia watu wakatae ndoa? Mambo ya ndoa si yangekufa tu yenyewe?
Ndipo tunapoelekea. Chat ya ndoa inazidi kushuka chini. Sasa hivi ni kawaida sana kukuta kijana 30's hajaoa wakati kwenye jamii ya zamani iyo ilikua serious issue.
Mimi natambua Ibilisi yuko nyuma ya kampeni hii kwa sababu watu wakikataa ndoa ndio uzinzi utaongezeka zaidi, maana wanaokataa ndoa hawakai hivyo hivyo walivyo, bado wanatafuta wanawake. Na uzinzi ukiongezeka, shetani anafurahi kwa sababu anakuwa amepata watu wa kwenda naye katika adhabu ya moto wa milele.
Again, hatuatweza kufika muafaka wa ilo suala kama ume-base kwenye dini kwa sababu watu wana imani tofauti. Ili twende sambamba ni vyema tukaleta hoja za kijamii zaidi sio za kidini
 
Sasa kama ndoa ni kuhusu tendo la ndoa. Ukibaniwa na mke unafanyaje?. Akianzisha maudhi na ukosefu wa heshima ufanyeje?.
 
34C77323-0E76-4E46-B86A-AE86A3751CA1.jpeg

Nikiwaza hapa tu nachoka🥲
 
Bongo ukishaona unaitwa kwenye fursa ujue wewe ndio fursa yenyewe, kama ndoa ingekuwa nzuri vijana wangekimbilia wenyewe sio kulazimishwa namna hii
 
Are you insinuating that my discourse is devoid of merit? If so, upon what intellectual or doctrinal foundation do you predicate such a denunciation? This subject pertains to an intricate moral and theological axiom—thus, I am most intrigued to fathom the profundity of your rationale.
Aaaiiseeee,,,,kumbe bado sikifahamu kiingereza aiseee!!!!!🙂‍↔️
 
Andiko unalosimamia ni 1 Wakorintho 7:1-9. Hilo halikatazi kuoa'
Hapo Paulo alikuwa anajibu maswali kutoka kwa Wakristo wa Korintho kuhusu ndoa na useja. Katika mstari wa kwanza, anasema:
“Ni vyema mtu asimguse mwanamke” (1 Kor 7:1)
Hii haimaanishi kuwa ndoa ni mbaya, bali Paulo alikuwa akizungumzia useja, yaani wanaoweza kukaa kama yeye wafanye hivyo kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hata hivyo anaendelea kusema:
“Lakini kwa sababu ya zinaa, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe. (1 Kor 7:2)

Hii inaonyesha kuwa ndoa ndiyo suluhisho la tamaa za mwili. Ndoa ndiyo jambo linaloweza kumfanya mtu asianguke kwenye dhambi ya zinaa.

Katika mstari wa 7-9, Paulo anasema anatamani watu wote wawe kama yeye (yaani, waishi bila kuoa ili wawe huru kumtumikia Mungu). Lakini anakubali kuwa si kila mtu ana karama hiyo ya useja. Anaongeza:
“Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.” (1 Kor 7:9)

Sasa unapowaambia watu wakatae ndoa wakati hawawezi kujizuia kukaa bila kuwagusa wanawake, huoni kuwa unawaingiza kwenye uzinzi?
Ukimsoma vzr hapo Paulo anasema sababu kubwa ya kuoa ni kuzia tu matamanio nothing else. so hakuna dhambi ya kutooa au kutoolewa. plus wanawake ni wengi kuliko wanaume so big % ya wadada hawataolewa hata wasagae meno na washinde huko church....Na hakuna faida ya mwanaume kwenye ndoa so why uingie kwenye mkataba ambao hauna faida nao......All in all yote ya duniani ni mipango yake so kama alipanga utaoa au kuolewa then itatokea na kama akisema no ni no. kama afande sele alivyoimba sio lazima wote tuwe wasanii wengine wabaki tu kuwa washabiki. So sio kila mtu lazima aoe au aolewe ukiolewa wewe au ukioa wewe inatosha now shughulika na familia yako. Achana na maisha ya wengine. KILA.MTU ABAKI NA DHAMBI ZAKE. tutakutana huko Kwenye judgement
 
Ukimsoma vzr hapo Paulo anasema sababu kubwa ya kuoa ni kuzia tu matamanio nothing else.
Kuna faida nyingi za kuoa zaidi ya hiyo. Usisahau Mungu aliwaambia Adam na Hawa wazae waijaze nchi. Wao wangekataa ndoa yao wewe leo ungekuwepo?

Tukiacha hilo, issue ni kwamba hao wanaokataa ndoa, bado wanaenda kuzaa nje halafu watoto wanaowazaa wanaacha kuwalea; hii ni mbaya.
 
Back
Top Bottom