Wanaopiga simu Zimamoto kuripoti matukio ya uongo kuchukuliwa hatua za kisheria

Wanaopiga simu Zimamoto kuripoti matukio ya uongo kuchukuliwa hatua za kisheria

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kizimamoto Kinondoni, Kamishna msaidizi muandamizi, Salum Mohamed amesema watawachukulia hatua za kisheria wanaosababisha usumbufu kwa Jeshi la Zimamoto.

Kamanda huyo amesema kuna raia wamekuwa na tabia ya kuitumia namba ya Zimamoto kuzungumza mambo yasiyoeleweka au kuripoti matukio ya moto ya uongo na kusababisha usumbufu kwa jeshi hilo.

Ameyasema hayo akizungumzia tukio la moto la Mivumoni Islamic Seminary uliozuka saa kumi na moja alfajiri, Agosti 31 Mtambani ambalo moto wake umedhibitiwa.

Moto huo umeathiri mabweni mawili na ofisi za walimu tano pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.
 
Na huwezi kujua ni ya prank mpaka ufike .
So ni bora ku respond immediately .
Ili kuokoa maisha na Mali
Ikitokea ni prank sheria ifuatwe
 
😂😂 hao wanaofanya hivyo ndo wale hawanaga kazi zakufanya.. wabongo kwa kujaribu hatujambo Kama watu walikuwa wanapiga zile namba sijui za majini Mara mashetani watashindwa ya Zima Moto na isitoshe ni bure..🤣🤣

I love my country..
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 wabongo wa se nge sana , dah
 
Back
Top Bottom