Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.


Yohana mbatizaji alipokuwa anawaondolea watu dhambi alikuwa Mungu? Hebu soma Matayo 3:1-6:


“1Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi”.
 
Siyo Bwana aliyewapa huo uwezo sema kanisa katoliki ndiyo limewapa Mungu hawezi kumpa mwanadamu uwezo wa kumsamehe mwanadamu mwenzie dhambi kanisa katoliki mnafanya makufuru maana hiyo kazi ni ya Mungu pekee

Tatizo ni kwamba hamkusoma vizuri Lugha mashuleni kwenu na hivi msomapo lolote mnaambulia patupu. Ukisoma nukuu hii hapa chini utagundua kuwa kuna watu wa aina ya uelewa wako waliokuwa wanaelewa kwamba mwanadamu hana uwezo wa kuondoa dhambi isipokuwa Mungu.Ni katika mktadha kama huo Yesu anasema wanadamu wanao huo uwezo na mamlaka.Mkazo nimuokoleza katika aya ya 10:

5Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza,“Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.” 6 Baadhi ya waalimu wa sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao, 7 “Anathubutuje kusema hivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake.” 8 Yesu alitambua mara mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9 Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’ 10 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, 11 “Nakuambia simama; chukua mkeka wako uende nyumbani!”
 

Yapi mapungufu? Kutoelewa kwa watu mambo ndio upungufu?
 

Kama wewe ni Mkatoliki na huu ndio uelewa wako karudie mafundisho ya Ubatizo au Komunio ya Kwanza.
 
Padre ni kwa kiswahili...kwa kingereza ni Priest...

Haya nipe andiko
Padre > Father
Kuhani > Priest
Kwenye biblia hakuna neno Padre, na maana ya padre ni Father, kwenye biblia linamaana tofauti kabisa mfano sala ya wakatoliki ya Our Father,Who is in heaven..huwezi sema Padre wetu uliyembinguni....
 
Pointless

Imekupasua mfumo wa fahamu,nini? Kama ulikuwa hujui huo ndiyo "usangoma" alioufanya William Miller na wenzie(akiwemo Ellen White).Walianzisha dhehebu la kupiga ramli ya lini Yesu atarudi mara ya pili. Yesu alikwisha kusema kuwa kwa ubinadamu wake haijui tarehe lakini William na kundi lake kwa nia ya kutaka kupiga pesa za watu, wakajigeuza waganga wa kiimani kutabiri tarehe ya kurudi kwa Yesu Kristu! Upo hapo?
 
Padre > Father
Kuhani > Priest
Kwenye biblia hakuna neno Padre, na maana ya padre ni Father, kwenye biblia linamaana tofauti kabisa mfano sala ya wakatoliki ya Our Father,Who is in heaven..huwezi sema Padre wetu uliyembinguni....

Wapi kwenye Biblia kuna neno "Mwinjilisti" au "Mchungaji" katika muktadha ambao ninyi wasabato mnatumia?
 
Jesuit wamefanikiwa sana kwenye taratibu zao walizo weka kwamba dhambi zinasamehewa ikiwa utazitaja na kuziungama kwao hii ni aina ya upelelezi .
 
Wapi kwenye Biblia kuna neno "Mwinjilisti" au "Mchungaji" katika muktadha ambao ninyi wasabato mnatumia?
Umenipotezea mda kusoma post yako kumbe hata biblia huijui..unatetea udini badala ya Kuikubali kweli ili uwe huru..haya nambie maneno haya yanamaana gani na yanapatikanikana kitabu gani:
"Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;... "
 
Kwanza naanza kwa kupinga hoja yako kuwa "hakuna mnyama aliyechinjwa ili Adam na Hawa wapate vazi"
Hakuna mahali Biblia inasema hivyo
Usipende kuleka "assumption" kwenye maandiko.
Mungu ni muweza wa yote ili kupata ngozi sio lazima achinje mnyama

Tatu,unaposema hoja ya kuungama kwa padre ilikomeshwa na Yesu alipokufa msalabani.
Je,kama ilikomeshwa mbona aliwaagiza "MKIWASAMEHE WAMESAMEHEWA,MSIPOWASAMEHE HAWAJASAMEHEWA"

hilo agizo tuta li apply wapi kama tusipoungama kwa makuhani(mapadre)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine biblia inanipa changamoto!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

1. Mkuu uelewa huo wa wasabato kwamba Yesu hakuagiza watu kwenda kuungama dhambi ni matokeo ya kusoma mambo kwa kurukaruka.

2.Kingine wasichokijua ni kwamba wanafikiria mapadri wao hawaungami dhambi zao wanazosema mapadri wanazo kama za kulawiti, uzinzi na wizi.Dhambi hizo mapadri sio wa kwanza kuzitenda na wala hizo dhambi sio kwamba ndio dhambi kubwa kuliko zote.Hata mitume nao walikuwa wanatenda dhambi na bado dhambi hizo hazikubatilisha utume wao.
 
Jesuit wamefanikiwa sana kwenye taratibu zao walizo weka kwamba dhambi zinasamehewa ikiwa utazitaja na kuziungama kwao hii ni aina ya upelelezi .

1. Kipi kigumu zaidi, mtu kuja na kueleza dhambi zake kwa Padri kama Yesu alivyoagiza na kisha Padri mhusika kumwambia Mungu amemsamehe dhambi zake au Ellen White kujigeuza na kuwa Mungu wa kufahamu dhambi za watu na kutaka kuzitaja?

2. Yasome maandiko matakatifu sanjari na Historia.Shirika la Jesuits lilianzishwa kati ya mwaka 1545 na 1563 wakati suala la Kitubio linaonekana katika Kanisa la mwanzo kabisa kabla hata haijajulikana ni lini hao Jesuits walingalianzisha hilo shirika lao.(Rejea Society of Jesus - Wikipedia)
 

Ndio maana nimesema ninyi mnasoma kwa kurukaruka. Nimetumia Istilahi "Mktadha" umeelewa nilikutega nini?
 
Sasa mbona unawasambulia wasabato tu? Kwani hamna walutheran, walokole, waanglicana, wamoravian, nakadhalika? Cha muhimu muombe Roho Mtakatifu akupe mwongozo wa kusoma biblia vizuri na akupe ufahamu wa kuelewa. Mungu akubariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Padre siyo yesu, Na padre hana mamlaka ya kumsamehe mtu dhambi. Kanisa limetekwa.
 
Kanisa la roma halijawahi kuwa la kweli hata siku moja, lenyewe ndilo lililo waua wakina petro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…