Kanisa Katoliki halikuanza kushambuliwa leo mkuu lilianza kushambuliwa na Dola ya Kirumi karne ya Kwanza. Kama Yesu alivyokuja kuwaita wenye dhambi basi anajua ndani ya Kanisa kuna wenye dhambi na wema na polepole wakiwa katika njia za dunia wanapokea huruma yake. Kuna mapadre wema na wenye dhambi kama binadamu wengine, kuna waumini wema na wadhambi na hili ndilo Kanisa Katoliki ili Yesu aliye kichwa cha Kanisa na sisi sehemu ya mwili atusafishe.
Yesu alimuambie Peter aliyemkana achunge kondoo wake hakwenda kuwafuata malaika walio wasafi mbinguni wachunge kondoo wake. Na wale wadhaniao wokovu ni wa mtu mmoja mmoja wawe makini na roho zao kwani Yesu alikuja kuwaokoa wanadamu na angekuwa anadeal na mtu mmoja mmoja tungesema alikuwa anabagua.
Kama unadhani utaenda mbinguni kwa nguvu zako mwenyewe endelea. Yesu alivyoita mitume na kuwapa mamlaka ya kuongoza hakuwa taahira asiyejua la kufanya. Ingekuwa hataki Kanisa angempa kila mmoja mamlaka ya kujiongoza bila kuwasikiliza mitume.
Sent using
Jamii Forums mobile app