SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,676
- Thread starter
-
- #321
Ukristu na ukristo ni sawa? Kama ulikuta neno la Mungu kwenye agano jipya imeandikwa Kristo kwa nini humkuacha kama ilivyo? Mbona mnajitoa ufahamu wako?
Sent using Jamii Forums mobile app
kwanza, UISLAMU WANGU UKO PALE PALE.
haya, kinachonifanya nidhani kwamba msamaha huo ulitolewa kwa mamlaka ya Uungu, ni saabu kwa wakati ule Yesu alikuwa katika nafsi ya Uungu, ona alivyo ponya, alivosoma roho zao zote zikiashiria mamlaka ya Kiungu, na wakati huo huo bila shaka kwa imani ya Kikristo, nafsi ya ubinadamu hapo ilikuwepo sababu alikuwa amesimama nao kwa uwepo wa mwili na nyama..
hata hivo, huoni ni wazi kuwa hata hao Wayahudi ambao ni uzawa wa Nabii Ibrahim walitamka wazi kuwa "mwanadamu kusamehe dhambi ni kufuru"?!
bado nna wasi hapa na mamlaka mnayompatia Padre
Sent using Jamii Forums mobile app
aliwaambia kuwa "Mwana wa Adamu" anayo mamlaka ya kusamehe dhambi..,Sasa wayahudi waliposema mwanadamu kusamehe dhambi ni kufuru, Yesu aliwajibu vipi? Kwa aya yako hiyo,baada ya wayahudi kuona jambo hilo haliwezekani Yesu alikubali kwamba walichokisema ni kweli? Je, Yesu Aliwakubalia kwamba ni kweli mwanadamu hawezi kusamehe dhambi?
aliwaambia kuwa "Mwana wa Adamu" anayo mamlaka ya kusamehe dhambi..,
swali langu, kwani huyo mwana wa Adam ni binadam yoyote yule?!
Sent using Jamii Forums mobile app
mbn Biblia inamuelezea Yesu tu kuwa ndo Mwana wa Adamu na sio watu wengine, na kama basi ni kwa watu waliopewa mamlaka, kwann kwa kipindi cha zamani wale makuhani waliokuwa na jukumu la kuwakilisha dhambi za watu kwa Mungu kwenye mahema (kama nilivyosoma kwenye huu uzi maelezo ya 3 Angels message) wasiitwe Wana wa Adam?Mwana wa Adamu maana yake wanadamu wote wanaotokana na wazazi wa kwanza lakini waliokasimiwa hayo mamlaka kama mapadri.
Mkuu bila shaka wewe ni Msabato....Kazi kweli kweli. Kasomeni kitabu cha Daniel Na ufunuo. Ila kabla ya kusoma omba roho mtakatifu
Mkuu bila shaka wewe ni Msabato....
Tunamalizana na uongo wa wapinga Kristo (Waislam) kisha tutafuata na uongo wa Wapinga Kristo (Wasabato)......
Kaa mkao wa kukata nyama[/QUOTE
Mkuu kasome . shida hatutaki kuwa kama mberoya .chunguza maandiko. Usiamini kila unaloambiwa. Jikite katika kusoma vitabu vya Mungu Na mwisho atakufunulia ukweli
Kazi kweli kweli. Kasomeni kitabu cha Daniel chote Na ufunuo chote. Ila kabla ya kusoma omba roho mtakatifu
Hakuna shaka rafiki kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho. Ila uje ukiwa unaielewa biblia vema. Sio kupapasa maana ukilianzisha Na wasbato use sawa. Tahadhari tu. Kwani wao ni waberoya chakula chao ni neno LA Mungu. Usijitumainie we we mwenyewe Bali mueke Mungu kwanza akuongoze Na akupe hekima ya kimbingu. BarikiwaMkuu bila shaka wewe ni Msabato....
Tunamalizana na uongo wa wapinga Kristo (Waislam) kisha tutafuata na uongo wa Wapinga Kristo (Wasabato)......
Kaa mkao wa kukata nyama
Huna ulichopinga zaidi umetokea details ya proceedure za zamani walikua wanafanya niniNitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"
Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.
Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.
Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani
Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani
Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo
Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo
Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote