Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Mkuu umewahi kusoma kisa cha watu wawili walioenda hekaluni,mmoja aliungama dhambi zake kwa kunyenyekea mbele ya Mungu na mwingine alijivuna kwa wema wake,na Yesu akasema yule aliyenyenyekea alipata msamaha wa dhambi zake.Mbona alisamehewa bila kwenda kwa padri?
 
Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"

Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.

Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.

Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani

Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani

Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo

Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo

Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote

Kwa hiyo, tueleze Yesu alipotoa agizo la kuwaondolea watu dhambi alimaanisha nini?
 
Hivi wazazi wa wale watoto kule Ireland nao wanaenda kuungama kwa mapadre? Kama wanafanya hivyo imani yao ni kubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu akinambia wenye biblia mi binafsi sijaona neno padre, kupitia hapo tu padre simtambui. Au padre ndo mchungaji??

Nikakosa jibu.

OK Nije kwenye mada ya kuungama kwa padre,swali langu ni hili, nikiungama kwa padre Mwenye dhambi nasamehewa??

PILI, Niliwahi kuungama kwa padre,huku padre akiwa anasinzia,,niligundua baada ya kumaliza ye akiwa kasinzia badae akashtuka akanipa sala za kusali,,je pale nilisamehewa?? Mana msameheji alilala

TATU, padre akiwa kanitongoza naweza kwenda kuungama kwake??
 
Mkuu umewahi kusoma kisa cha watu wawili walioenda hekaluni,mmoja aliungama dhambi zake kwa kunyenyekea mbele ya Mungu na mwingine alijivuna kwa wema wake,na Yesu akasema yule aliyenyenyekea alipata msamaha wa dhambi zake.Mbona alisamehewa bila kwenda kwa padri?
Akikujibu unitag au tukio la mwiz Mwizi Msalabani alikuwepo Padre nan?
Mbona mnaacha mafundisho ya Mungu ili mtimize matakwa yenu?.
IMG_20180829_182546.jpg
IMG_20180829_182503.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na nafikiri kwenye uzi ule kuna baadhi ya watu waliowahi mwanzo walihoji kwa nini na niliwapa jibu na wala hakuna mtu aliyezuiliwa kwenda kuomba msamaha kwa Mungu kupitia mapadri. Ila si mapadri wote siku hizi wanatenda kazi zao katika maadili yanayokubalika. Mengi nilieleza ndani ya uzi ule kwa walionihoji hivyo siwezi kurudia hapa maana si muda muhafaka kwa hilo. Kila mkatoliki ana haki ya kwenda mbele ya padri kwa maungamo ila mtu huwezi kwenda pale huku ukiwa unakumbuka kitu kilichowahi tendeka nyuma na padri mwenzie ukaondoka kwenda kwenye malipizi ukiwa bado una wasiwasi. Binafsi siwezi sijagusia mtu mwingine.

Kukosa kwa Petro hakukuwahi kumuondolea mamlaka na madaraka(ukulu) ambao alishapewa naYesu.Kwa hiyo,Padri kushindwa kuzingatia siri za maungamo hakumuondolei mamlaka hayo ya kukuondolea dhambi.
 
Kuna mtu akinambia wenye biblia mi binafsi sijaona neno padre, kupitia hapo tu padre simtambui. Au padre ndo mchungaji??

Nikakosa jibu.

OK Nije kwenye mada ya kuungama kwa padre,swali langu ni hili, nikiungama kwa padre Mwenye dhambi nasamehewa??

PILI, Niliwahi kuungama kwa padre,huku padre akiwa anasinzia,,niligundua baada ya kumaliza ye akiwa kasinzia badae akashtuka akanipa sala za kusali,,je pale nilisamehewa?? Mana msameheji alilala

TATU, padre akiwa kanitongoza naweza kwenda kuungama kwake??
😀😀 umenichekeshaa sana point yako ya pili. ulimsubiri mda gani mpaka alipomka.
 
Kukosa kwa Petro hakukuwahi kumuondolea mamlaka na madaraka(ukulu) ambao alishapewa naYesu.Kwa hiyo,Padri kushindwa kuzingatia siri za maungamo hakumuondolei mamlaka hayo ya kukuondolea dhambi.
Basi kwa padri kama huyo utaendelea vipi kwenda kwake!? Wengine naweza kufikiria ila siwezi rudia kosa.
 
Mkuu umewahi kusoma kisa cha watu wawili walioenda hekaluni,mmoja aliungama dhambi zake kwa kunyenyekea mbele ya Mungu na mwingine alijivuna kwa wema wake,na Yesu akasema yule aliyenyenyekea alipata msamaha wa dhambi zake.Mbona alisamehewa bila kwenda kwa padri?

Nadhani ndio nasema watu tuna matatizo ya kuchakata maudhui. Yesu kwa mfano huo alitaka kufundisha jinsi ya watu tunavyoweza kujiona wakamilifu na wengine wanaotambua kwamba ni wakosefu na hivi wanastahili msamaha.Ingalikuwa ni hivyo kwamba hakuna haja ya kuungama dhambi basi Yesu asingaliweza kuacha huo muundombinu wa kuwaondolea watu dhambi. Mungu hawezi kujipinga hata kidogo.
 
tangia zamani nilikuwa nawahoji wazaz wangu ambao ni wakatoliki ujasiri huo unatoka wapi kuungama kwa padre?jibu ni kwamba haifai hata kidogo kwako mwenyewe usalama wako ni mdogo napia hata kwa mungu pia utakuwa umenyanganya mamlaka ya yesu
 
Umeandika meeeengi hoja no padri no binadamu,naye ana mapungufu ,vipi uunhame kwake usiungame Kwa mungu?

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Kwa hiyo umeambiwa Binadamu hawezi kuondoa dhambi? Kajisomee
Zaidi ya Yote, Marko 2:5-10. Baadhi ya watu walipotilia shaka suala la Yesu katika ubinadamu kuwaondolea watu wengine dhambi, Yesu aliwathibitishia kuwa mwana wa mtu anao uwezo huo wa kuondoa dhambi za walimwengu:

“5Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza,“Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.” 6 Baadhi ya waalimu wa sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao, 7 “Anathubutuje kusema hivyo? Anamkufuru Mungu! Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake.” 8 Yesu alitambua mara mawazo yao, akawaambia, “Mbona mnawaza hivyo mioyoni mwenu? 9 Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’ 10 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anayo mamlaka ya kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, 11 “Nakuambia simama; chukua mkeka wako uende nyumbani!”

2. Vile vile, kupitia Luka 5:24, tunaelezwa pia kwamba katika suala la uwezo wa Yesu kuwaondolea watu dhambi alifanya hivyo katika ubinadamu wake na sio kwa ule Umungu wake.

3. Mwinjili Matayo tena katika sura ile ya 18:15-20, anatudokeza jinsi Yesu kabla ya kuwapatia Mitume rasmi uwezo wa kuondolea watu dhambi, alipata kuwadokeza jambo hilo.Uwezo wa kufunga na kufungua ndio kule kuwaondolea watu adhabu za muda mfupi, zitokanazo na dhambi:

“15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.18 Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”
 
tangia zamani nilikuwa nawahoji wazaz wangu ambao ni wakatoliki ujasiri huo unatoka wapi kuungama kwa padre?jibu ni kwamba haifai hata kidogo kwako mwenyewe usalama wako ni mdogo napia hata kwa mungu pia utakuwa umenyanganya mamlaka ya yesu

Ubatizo huondoa dhambi na maungamo huondoa dhambi.Kwani hujawahi kujibatiza mwenyewe kwa maana si unajua maji ndiyo yanaondoa dhambi na unafahamu fika yanapatika kwenye mito na maziwa au baharini?
 
Basi kwa padri kama huyo utaendelea vipi kwenda kwake!? Wengine naweza kufikiria ila siwezi rudia kosa.

1.Kwani umeambiwa lazima uende kwa padri yule yule tu? Ndivyo kanisa Katoliki linavyofundisha?

2. Kwa nini unauona tu upungufu wa Mapadri katika kuungama dhambi ila kukubatiza bado unaendelea kwenda kwao na bado hata watoto wako bado unampelekea padri yule yule?

3. Mtu yeyote "anayemtunishia" Padri kuungama dhambi hana tofauti na Adamu na Eva kutokuwa tayari kukiri makosa yao na badala yake waliishia kutafuta visingizio.Ni dalili ya kukosa unyenyekevu.Ni dalili ya kujiona sisi tunafahamu zaidi kuliko wengine au kwamba sisin tuna hadhi sana kuliko wengine.
 
Catholism is ant Christ by nature

Ndivyo "roho wa unabii" wa William Miller na Ellen (aliyewafanya wahangaike na tarehe ya kurudi Yesu badala ya kuwahimiza watu namna ya kumsubiria Yesu) alivyokujalia?
 
Back
Top Bottom