Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Hayo yatajitokeza wakati wa uchangiaji.Kuna watu walidandia maandiko Matakatifu kwa mbele na hivi wanawapotosha kondoo wa Mungu.Ngoja tuwasaidie
Baba Paroko, tumsifu Yesu Kristu!! Asante sana kwa somo zuri amblo hakika limeshiba. Nimesoma kama na kukuelewa kama ninavyomwelewa Father Titus Amigu. Sina hakika kama yule mburura atarudi tena hapa!!
 
Nyie hamjasoma hilo bandiko...I'm sure 100%

Sent using Jamii Forums mobile app

Hawa hawana macho ya kuona mambo mengine zaidi ya maandiko yanayomuonyesha Yesu anarudi upesi.Bibi yao, Ellen White, ndiye aliyewapofusha hata wasiweze kuona kitu kingine chochote.Wanafikiria kurudi kwa Yesu ni sawa na Ziara ya Magufuli, kwamba itatolewa Press release ili wapeleke Tingatinga kulima njia.
 
Huna tofauti na wayahudi walioshangazwa na mtu (Yesu) kusamehe dhambi!

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Eti nao utawakuta siku ya Jumamosi wamebebelea Biblia vifuani wakidhani Biblia ikipata Joto,joto litapanda hadi vichwani mwao na hivi kuielewa Biblia.

2. Wanasoma vitu lakini hawana akili za kuelewa. Nina imani wangalikuwapo wakati wa Yesu wangaliungana na timu "wayahudi na mafarisayo" kumpinga Yesu kwamba hana uwezo wa kusamehe dhambi za wanadamu.
 
Wewe ukipewa kukaimu madaraka anayehesabika anatenda kazi hiyo ni nani? Ni wewe au aliyekukaimisha nafasi hiyo?
Mambo ya kidunia yako tofauti na mambo ya kiroho. Ndio maana hata wanaokemea pepo wanakemea kwa jina la Yesu. Kama walipewa mamlaka mbona hawakemei kwa majina yao na mapepo yakatoka?

Kuna sehemu wanafunzi wa Yesu wakamjia wakamwambia hata kwa jina lako, mapepo yanatutii. Pepo hatoki kwa jina la nabii/mchungaji/kuhani/padre japo wao ndio wamefanya kazi ya kuomba. Hata kubatiza walipewa maagizo wawabatize kwa jina la baba na mwana na roho na sio wabatize kwa majina yao kwa sababu wao ndio wametenda kazi ile.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma hilo andiko lako kwa lugha ya Kingereza utaona neno forgiven ambalo limetoholewa kutoka lugha ya Kigiriki ambayo ndio iliyotumika kuandika agano jipya neno forgiven kwa Kigiriki lina maana AMPHIEN ambalo kwa Kingereza chake halisi ni have been literally

John 20:23 is not saying that Catholic priests have the authority to forgive sins. It is saying that Christian disciples have the authority to pronounce what sins "have been forgiven

Imebidi nikupe uhalisia though the choice is yours

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba Paroko, tumsifu Yesu Kristu!! Asante sana kwa somo zuri amblo hakika limeshiba. Nimesoma kama na kukuelewa kama ninavyomwelewa Father Titus Amigu. Sina hakika kama yule mburura atarudi tena hapa!!

Asante.Tuko pamoja; na huyo "sangoma',mtembea na "hirizi" za kiimani, akafie huko mbali.
 
Yesu alimbatiza nani alipokuwapo hapa duniani?Je,kwa kutofanya hivyo ina maana si yeye anayewaondolea watu dhambi zao kwa njia ya ubatizo? Hivi ndio kwanza unajifunza reasoning?
Soma biblia yako katika andiko hilo la 1tim 2:5 kwamba mpatanishi kati ya wanadamu na Mungu ni mmoja naye ni Yesu kristo. Sio nabii wala mchungaji wala padre.

Ukija kwenye mada ya ubatizo ni pana tutakuja kwenye ubatizo upi ni sahihi, wa maji mengi (aliobatizwa Yesu) au maji machache (mnaobatiza nyie) na ubatizo upi sahihi, kubatiza watoto wadogo au kubatiza watu wazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Nataka fungu lolote kutoka kwenye maandiko matakatifu yanayo ruhusu hicho unachokitetea na mimi nitakupa verse zinazopingana mnachokiamini ni sahihi
21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
Yohana 20 :21

22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Yohana 20 :22

23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Yohana 20 :23



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kuungama kwa padri? Unaungama dhambi zako kwa yule uliyemkosea sasa unaenda kuungama kwa padri kwani umemkosea yeye? Acha kubeba imani bila kutumia akili
 

Unajaza server za JF bure tu.Kama ubatizo ni function ya Quantity badala ya Quality nendeni sasa mkaweke kabisa order viwandani, ya madebe ya sabuni ya Omo na Mshindi.
 
Kuungama kwa padri? Unaungama dhambi zako kwa yule uliyemkosea sasa unaenda kuungama kwa padri kwani umemkosea yeye? Acha kubeba imani bila kutumia akili
Mstari wa 23 hapo chini umeelewaje?

21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
Yohana 20 :21

22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Yohana 20 :22

23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Yohana 20 :23



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…