Mambo ya kidunia yako tofauti na mambo ya kiroho. Ndio maana hata wanaokemea pepo wanakemea kwa jina la Yesu. Kama walipewa mamlaka mbona hawakemei kwa majina yao na mapepo yakatoka?
Kuna sehemu wanafunzi wa Yesu wakamjia wakamwambia hata kwa jina lako, mapepo yanatutii. Pepo hatoki kwa jina la nabii/mchungaji/kuhani/padre japo wao ndio wamefanya kazi ya kuomba. Hata kubatiza walipewa maagizo wawabatize kwa jina la baba na mwana na roho na sio wabatize kwa majina yao kwa sababu wao ndio wametenda kazi ile.
Kwani lini ulienda kuungama kwa Padri akakuondolea dhambi zako kwa jina lake badala ya lile la "Kwa Jina la Baba,Mwana na Roho Mtakatifu"? Hivi tunajadiliana na "msukule"?
Haya ndiyo madhara ya watu wanaokaa muda wote wanaang'aza macho angani kuona kama Yesu anarudi upesi.Akili zako hazipo kabisa kwenye mjadala bali ziko zinasikilizia sasa huko nje kama kuna vishindo vya Yesu kurudi.
Sent using
Jamii Forums mobile app