Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wanaopinga kuungama dhambi kwa Padri, ndio wapinga Kristo wanaohubiriwa na wasabato na ndio wale wanaosoma maandiko kwa kurukaruka.

Wakati wa agano la kale waisraeli walikua wakikosea wanaenda kwa nabii kumweleza awaombee msamaha kwa Mungu. Elewa sio nabii anayewaondolea dhambi bali alikua anawaombea msamaha lakini pia ukumbuke haikua sheria kwamba ni lazima uje kwa nabii akuombee usamehewe, walikua wanaangalia nani yupo karibu na Mungu ndio waombee msamaha kwa sababu wao walikua wanajiona wakosefu.

Wakati wa agano jipya baada ya ujio wa Yesu toba na kila kitu wanaomba watu wenyewe na Yesu lekee ndiye anayesamehe dhambi. Ili andiko liende kwa udhibitisho onyesha sehemu Yesu alipotoa maagizo kwamba watu waende kuungama dhambi zao kwa mitume ili wasamehewe. Onyesha mfano ni wapi mtume petro au paulo au yoyote yule walisamehe mtu dhambi? Agano jipya mchungaji anakuongoza sala ya toba na unakiri kwa kinywa chako mwenye ila jukumu la kusamehe dhambi sio lake.
Mkuu hv hawa wakatoliki hujawazoea tu? Yaaan labda mbishane kwenye mambo mengine lakni kama ni maswala ya kutoa na maandiko hawana ujasiri hata siku 1 wa kuyatoa maana watayapata wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umesoma uzi vizuri utabaini kwamba uwezekano huo ungalikuwapo basi Yesu Kristu asingaliweka miundo mbinu hiyo ya Upatanisho.Kwa kuwa Yesu ni Mungu alijua watu kwa kujiungamia wenyewe wangaliishia kufanya sarakasi tu.Kuungama dhambi kunahusisha kufanya malipizi,waaidha kurudisha ulivyochukua kama alivyofanya Zakayo.

Ni kwamba tunalazimika kuungama dhambi ili mahusiano yetu na Mungu yawe mazuri.Dhambi ina madhara yafuatayo:mosi,inaleta mahusiano mabaya kati ya mwanadamu na Mungu.Pili,kati ya mtu mmoja na mwingine na tatu, kwa mtu mwenyewe.

Kumbe tofauti na Wakristu wengine wanavyoelewa, dhambi haiharibu tu mahusiano kati ya mwanadamu na Mungu, bali pia kati ya wanadamu na wanadamu.Mt.Paulo anatueleza mara nyingi sana katika barua zake kuwa sisi ni viungo katika mwili wa Kristu na kwamba yeye (nafsi ya Pili) na Mungu baba ni wamoja Rejea Warumi 12:5):

“Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.”

Kwa hiyo, ni mantiki hiyo kwamba kwa sababu sisi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake,basi dhambi ya mtu mmoja haiishii katika kumuumiza mhusika pekee, bali madhara yake lazima yamguse na mwingine katika mnyororo ule ule unaotuunga kwa Kristu.(Rejea 1 Kor 12:26):

“26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.”

UNACHOONGELEA WEWE UNAMAANISHA KUTUBU

Injili ya Marko 1:1-5, nayo inatueleza kuwa watu walikuwa wanamwendea Yohana Mbatizaji wakishakutubu na wakishaungama dhambi zao, walibatizwa ili kupokea ondoleo la dhambi zao:

“4 Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. 5 Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani”.

Katika ya aya 4 na 5 ya Injili hiyo ya Marko, tunapata maneno mawili “Kutubu” na “kuungama” ambayo yana maana tofauti.

Na mwinjili Marko, anapotuandikia hivyo anamaanisha kwamba kulikuwa na mambo mawili yanafanyika kwa mtaka ubatizo kabla hajabatizwa.Mosi, kutubu dhambi na pili,kuungama dhambi.


KUTUBU, kunatofuatiana na KUUNGAMA kwa sababu, kutubu ni hali ya kuugua moyoni.KUTUBU ni kitendo cha kujutia tendo fulani.Kutubu hufanyika moyoni, wakati kuungama kunafanyika nje ya nafsi ya mtu.

Kuungama ni kusema nje ya moyoni na mbele ya mtu mwingine kuwa umekosa.Kumbe, Marko anapotumia maneno hayo mawili sio kama anataka kutueleza maana ile ile moja ya kujutia dhambi moyoni bali kuweka wazi hizo dhambi zenyewe.

Yakobo naye katika 5:14-15, anatupatia picha halisi ya maana ya neno kuungama anapotumia neno “ungamianeni” dhambi zenu.Ikiwa Yakobo alitaka kumaanisha mtu kusema dhambi zake kimoyokimoyo, basi angalitumia neno jingine na wala sio ungamieneni:

“14 Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.15 Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.”
achankutulisha upupu bwana ! ni wapi walimpigia magoti yohane au wew unataka kujifananisha na Yesu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha.. Mjadala kama huu unatimia wakiwepo watu kama hawa, "ntu mbili" ndani ya track moja.... Otorong'ong' na huyu SANCTUS ANACLETUS

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wapuuzi mpk leo wanatetea ujinga huu? Kweli shetani bado hajafa loh! Padre yeye ni “mtu” kama Yesu? Kuomba msamaha kwa uliyemkosea (mtu mwenzako) ni sahihi. Tatizo nnaloliona ambalo walokole tungependa kujua ni maombi ya ‘via’ kw Padre ndipo akupelekee kwa Mungu.

Ikiwa binadam baada ya dhambi amepungukiwa, padre ni nani mpk asiwe ‘binadamu?’
 
Tatizo nnaloliona ambalo walokole tungependa kujua ni maombi ya ‘via’ kw Padre ndipo akupelekee kwa Mungu
Umekuwa mlokole siku hizi....


Vipi umemkacha Nabii Ellen G White sio ....au bado unang'aa macho angani kusubiri vishondo vya ujio wa Kristo...??
 
Mkuu kwenye uzi wako nimeona neno "YESU KRISTU"
Usahihi ni "YESU KRISTO" siyo "YESU KRISTU"

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hizo Ni lugha. Tunazidiana tafsiri tuu maana ni ile ile.
Ukumbuke neno Yesu Kristo/Kristu halijaanzia kwa kiswahili....kuna lugha kibao zimepita.....kirumi....kilatin....kigiriki....Klingereza...kiswahili.
Hebu rudi lugha ya kiyunani kaulize maana
 
Sasa nani kasema Padri hana dhambi duniani hakuna binadamu asiye na dhambi.. Sasa wote ni wadhambi wote wanauwezo wa kusamehe dhambi kama bwana alivyowapa huyo uwezo

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo Bwana aliyewapa huo uwezo sema kanisa katoliki ndiyo limewapa Mungu hawezi kumpa mwanadamu uwezo wa kumsamehe mwanadamu mwenzie dhambi kanisa katoliki mnafanya makufuru maana hiyo kazi ni ya Mungu pekee
 
Hahahaha mtoa mada nikajuaga dini yako imekamilika kumbe ni majanga tu hadi imekupasa kujipinda itetea. Hayo ndo maswala ya dini(imani) yalivyo, kwani hakuna dini(dhehebu) lililokamilika kwa ambae si muumini wake.
Jinsi unavyouponda uislam kwenye jukwaa lile sikutegemea nawe kwako kuna mapungufu.
 
Umekuwa mlokole siku hizi....


Vipi umemkacha Nabii Ellen G White sio ....au bado unang'aa macho angani kusubiri vishondo vya ujio wa Kristo...??
Jibu hoja kijana, huyo Padre yeye ni mungu na yeye? huo ni uzwazwa kuomba padre akuombee kwa Mungu dhambi zako na wakati mapadre hao hao ni wapiga pumbyu wa kueleweka kabs, wanywa pombe, waasherati, wachawi.

MTU ANAYEENDA KWA PADRE KUOMBA TUBIO LA DHAMBI ANAKUA HAJITAMBUI
 
Hapana, nitaumalizia ni mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alichoandika ningeweza kutengeneza summary ni kua anajaribu kutetea kuhusu kuomba msamaha kwa YESU ila kupitita kwa Padre ni sawasawa. Amechukua mfano wa Zakayo na Yesu, akaja kwenye vitabu vya torati na mwishoni akaingiza ishu zao za Katekisimu. Hakuna cha maana zaidi ni kutetea kuwa Padre anatakiwa akusikilize dhambi zako ndio ziendelee kwa Mungu.
 
RC ilikua serikali yakwanza duniani kwaio kuungama kwa padri ilikua ndo style yao ya inteligensia ....kujua watu wao wanafanya nn na wapi...mm ni RC...dini zote ni akili za binadamu so kama yesu alivo sema Amri kuu ni upendo.na ukifwata hutokua na shida yakwenda kuungama.
 
Kama unaamini kwamba ubatizo unaondoa dhambi ni kwanini mnawabatiza watoto wadogo??? Huwa wana dhambi gani hasa???

NB:
UBATIZO HAUONDOI DHAMBI.

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Kwani ile dhambi ya Asili uliyobatizwa ili kuiondoa, uliirithi wakati gani? Nakuuliza ile dhambi ya Adam na Eva uliirithi baada ya kuoa au baada ya kuanza Form one?

2. Kumbe na wewe unajiita mkristu lakini huelewi unabatizwa ili kuondoa nini? Basi, watoto wadogo wanabatizwa ili kuondoa dhambi ya asili ambayo by the time tu fertilization inatokea tayari na yenyewe unaipata.
 
Kama unaamini kwamba ubatizo unaondoa dhambi ni kwanini mnawabatiza watoto wadogo??? Huwa wana dhambi gani hasa???

NB:
UBATIZO HAUONDOI DHAMBI.

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Wewe kwa ukristu wako hauna tofauti na Nikodemo. Hivi "Ellen" White alipokubatiza hakukueleza maana ya huo ubatizo? Tuseme basi kwamba ulikuwa hujaoga toka uzaliwe na hivi ukaenda kwake ili akuogeshe?

2. SASA kwa kuwa Ellen Ellen alikudanganya kwamba alikuzamisha majini ili ujifunze kuogelea,tunakueleza kwamba alikudanganya. Ulizamishwa ili uondolewe dhambi ya asili (uliyoirithi toka kwa Uzao wa kwanza wa mwanadamu) pamoja na zile zingine ambazo ulikuwa umezitenda wewe mwenyewe. Hebu Msikilize hapo Yesu anavyomueleza Nikodemo:

"2 Siku moja Nikodemo alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.3 Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa tena hataweza kuuona ufalme wa Mungu.” 4 Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena!” 5 Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho. 7 Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya. 8 Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.” 9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?” 10 Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israeli na huyajui mambo haya?"

Na kama hiyo, haitoshi basi,sikilizia hii show ya Yohana Mbatizaji ilivyowaondolea watu dhambi baada ya kutubu na kuziungama.Rejea msisitizo katika aya ya 6:

“1Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; 6 “1Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. 3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi”. (Matayo 3:1-6)
 
Mkuu hv hawa wakatoliki hujawazoea tu? Yaaan labda mbishane kwenye mambo mengine lakni kama ni maswala ya kutoa na maandiko hawana ujasiri hata siku 1 wa kuyatoa maana watayapata wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app

Suala sio maandiko kutolewa.Suala ni kuyaelewa. Mantiki ingalikuwa ni kutoa maandiko basi hata William Miller na genge lake wasingaliweza kuhatarisha maisha ya watu na mali kiasi kile kwa kuelewa kwamba siku 2300 zinazoongelewa katika Ufunuo wa Yohana zililenga Yesu kurudi tarehe 22 Oktoba 1843/1844.Au kwamba Ellen White alifika mahali akawa Mungu na hivi akawa na uwezo wa kujua dhambi za watu.
 
Back
Top Bottom