Guys, hapa si suala la Mahakama ya Kadhi kama ilivyo. Waislamu tunahaki ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, but kinachopingwa, naomba ifahamike ni kuhusu kuihusisha Serikali katika mchakato huo. Serikali haiwezi kutamka kuwa mahakama ya Kadhi ianzishwe au isianzishwe! La pili linalopingwa kisheria ni namna mahakama ya kadhi itakavyoingiliana mamlaka na mfumo wa mahakama zilizopo kiserikali.
Kwa hiyo basi;
Iwapo kwa Waislamu mahakama ya kadhi inahitajika katika mfumo wa Dini, ni ruksa kuianzaisha, lakini Kikatiba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haina Dini na hivyo haitajihusisha na masuala ya Dini mija kwa moja, kama katika uanzishwaji wa Mahakama hiii muitakayo.
Pili,kama mnaitaka mahakama hii ianzishwe, basi ianzisheni kwa kutumia uhuru wa kuabudu( Freedom of Religion/Freedom to Worship). Na ianzishwapo, ni lazima muhakikishe kuwa haiingiliani na mfumo wa Sheria za nchi hasa katika mpangilio wa mahakama(Court's Hierachy). Kwa mfano inazishwe kama ni ngazi ya usuluhishi awali wa masuala yahusuyo Uislamu, kwa maana ya kwamba jambo litasuluhishwa kwanza huko, ikishindikana ndipo mtu aende mahakamani.
Zaidi ya namna hizo mbili, mahakama ya Kadhi muisahau katika Tanzania, labda katiba itakapoandikwa upywa, suala hili likiwekwa katika katiba,la sivyo; ieleweke kwamba kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini ni unconstitutional and hence an illegal concept. That is why JK amefeli kuitimiza,japo aliwaahidi kulishughulikia,si aliwajibu?
Being intellectual ni pamoja na kuzielewa vizuri sheria za nchi unayoishi. What sort of an intellectual are you that you dont?
Nawasilisha.