Nimefuatilia kwa makini Hoja kwa ujumla, Mtoa hoja na wachangiaji.. Sijaona point zaidi ya Ubabe . By the way Hiki ndicho Shekhat ya kiislam inachokipinga kwa Nguvu Zote. Kwanini Baadhi ya Vijibaba vijifanye vyenyewe ndio vidume vya mbegu kwa kurundika Lundo la wanawake Ndani ya Ndoa kwa kisingizio cha Dini?... Ni kunyanyapaa wanawake, Hebu Tupashane au tuelezane ukweli jamvini bila chenga, Mwanaumme huchukua 2-15 minutes kwenye tendo la ndoa kabla ya kujiradhi ila mwanamke huchukua zaidi ya nusu saa, na kwa wapendanao inamgharimu mwanaume aende mbele zaidi ili amrdhia mkewe kwenye tendo la ndoa.. na Hii inamgharimu mwanaume kausumbufu flani, Nguvu pamoja na concentration. Sasa unapokuwa namke zaidi ya mmoja utawezaje kuwafikisha wote radhia, kwa mateso gani.. kama sio kuwachafuachafua na kuwatosa. Ni nani mwenye mke zaidi ya mmoja na ukawasikia wanawake hao wakiwa happy radhiani.
Kwani shahidia inasemaje, mwanamke wa kiislam anayo haki ya kumtaka mumewa mahaba muda wowote, sasa kama unao wawili au balaa zaidi watatu na wote wanataka mahaba kwa wakati mmoja Utawawezaje?.. kwanini kuendekeza mawazo mgando kwamba wanawake wa kiislam ni vyombo vya starehe kwa wanaume na zana za kufyatulia watoto??.
Tuseme Ukweli Kuoa mke zaidi ya Mmoja ni Tamaa tu za wababa ambao wanasingizia kwamba niAmri ya mtume. Mtume alikuwa na wake kadhaa, yes that is true, but yeye aliwaoa kwa misingi yasafari alivyosafiri kwenye kwa kuipigania dini kwa hivyo asingebeba familia zake zote, that is why akiwa mji mwingine alioa huko then alipokwenda another mji akaoa tena, sasa wewe mbaba wapi umekwenda kupigana vita gani mpaka urundike kinamama ndani.. Tamaa tu, Muone.. aiibu hata Ukimwi huogopi?
Shekhat ya Kiislam inachojua kuna agenda za siri zinazopelekea uundwaji wa mahakama za kadhi, sasa kwanini nyie wababa msizisemeeee mpaka mtumie mlango wa kudhalilisha wanawake this way?.. eti mtu anajitapa kabisa eti ana wake 3, hata aibu huoni.
unaposema kwa ajili ya mirathi, hiki ndicho shekhat ya kiislam haitaki kabisaaa kusikia, Kwenye mirathi mwanamke wa kiislam hana sauti kabisa, Hata kama Sheria za nchi zikaruhusu mahakama ya kadhi, humo ndani viwembe vitatembea kwa sana, mtueleze mnaiunda kwa mujibu wa sharia ipi, za sunni au shia, na kama ni suni, mnasemaje kuhusu mwanamke kuwa eda huku mali walizochuma na mumewe zikigawanywa??.. m kama ni shia mnasemaje kuhusu talaka komoa 2, na mume akafa, mke atakuwaje?!! Tunaiita talaka komoa kwa sababu ni ubabe tu wa mwanaume kumtaliki mkewe talaka mbili ati iko siku atamuoa tena kisha yeye huku anaendeleza libeneke na wanawake wengine anaowaoa. Mbona huu ni ujinga KAMILI?. Dini haisemi hivyo ni Ubabe tu wa vibaba vya kileo. Mmetengeneza Baaza la Maulamaa kimywakimya hata mwanamke hajuikani ndani ya uislam. Tulisemanini kuhusu Bakwata. Mbona watu mnatumia Kigezo Cha Dini mliyochakachua sheria zake kukandamiza wanawake???
Mwisho wa hoja umesema Tuache waislam tuelezee kwanini tunataka mahakama ya kadhi, kumradhi turnabal, badilisha semi yako mara moja, useme kundi Fulani la wababa wa kiislam wasiodhibiti hisia za tamaa zao zilizopindukia na kuoa rundo la wanawake kwa starehe ambao hufa mapema kwa tamaa hizo ndio wanataka waeleze kwanini wanahitaji mahakama ya kadhi, hapo ungeeleweka. Ashkhum