Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Nafikiri wakristo wa Tanzania ndicho wanachotegemea waislamu wafanye vurugu ili waseme kuwa waislamu wameleta fujo nchini kumbe wameomba miaka nenda rudi lakini wananchi wenzao wakristo wenye madaraka wamekataa kwasababu ambazo hazina mshiko bali kuinyesha kiburi na mashindano...unafikiri wanigieria walipenda, unafikiri mataifa mengine walipenda na Tanzania ni tofauti sana??? BIG time NO ufa unaojengwa kwa mashindano ambayo yapo kwenye hoja ya gharama ni dhaifu sana...

Nimekuuliza wewe kama mkristo unakosa nini waislamu kuwa na mahakama ya kadhi???Tanzania

Hivi kila anayepinga mahakama ya kadhi automatically anakuwa Mkristo?
Ask around pal, there are learned Muslim lawyers who know and understand that Kadhi courts cannot be funded or kick-started by the Government.
Mimi si muislam lakini naunga mkono kadhi court ianzishwe, ila iende sambamba na mfumo mzima wa sharia law kwa waislam watakao ridhia ili kupunguza watoto wa mitaani watakaokuwa wamezaliwa na vijana wenu lakini hawatambuliki na mahakama hizo za Kadhi. Sharia law inatakiwa iwepo ili kuwashughulikia wazinzi wanaozaa zaa ovyo nje huku wakijua watoto hao hawana chao kwenye mirathi. Na zaidi, mahakama hizo zianzishwe na waumini wenyewe wanaotaka.
 
Inaonekana hujasoma majibu yangu ambayo nimeanza kuyaandika miaka minne iliyopita - hakuna kitu ambacho Mkristu anahofia kuhusu mahakama ya kadhi kuwepo. Ndio maana sisi wengine tunawapigia debe muianzishe na utaona hakuna Wakristu wanaokataa uwepo wa mahakama ya kadhi.

Ila pia inaonekana hujafikiria vya kutosha jinsi gani mahakama ya kadhi inawahusu Wakristu vile vile. Mahakama ya kadhi haitaathiri Waislamu peke yao.

a. Kama wanataka serikali ilipie gharama za kuendesha mahakama ya kadhi kwa kodi za wananchi basi walipa kodi (wakristu wakiwemo) wanayo haki ya kutoa kauli yao. Kama vile tunavyosikiliza hoja za Waislamu wanaopinga serikali kutoa ruzuku kwenye hospitali za rufaa zinazoendeshwa na makanisa. Waislamu hao wanayo haki kabisa ya kuhoji matumizi ya fedha hizo na kama wanaona kanisa linapendelewa wanayo haki kabisa ya kupinga fedha hizo kwenda kwenye mahospitali hayo na kutaka makanisa yaendeshe mahospitali yake kwa gharama zake. Sasa kama WAislamu wanaweza kujenga hoja hiyo kuhusu gharama kwenda kwa makanisa (japo utaona mahospitali yanahudumia na kuajiri watu wa dini zote). Lakini hoja ya Wakristu inaweza kuwa na nguvu zaidi kwa sababu mahakama ya kadhi si kwa ajili ya wananchi wote na wale haiwezi kuwa na kadhi Mkristu au Mhindu (hata kama atakuwa amesomea sharia!). Kwa hiyo wanayo haki ya kuzungumzia jinsi fedha zao zinataka kutumiwa.

b. Mahakama za kadhi zitagusa familia za Wakristu vile vile. Fikiria mahali ambapo mwanamme ni Muislamu na Mke ni Mkristu. Je, Mkristu akitaka kutafuta haki kwa njia ya mahakama za kawaida na Muislamu (mume) anataka kwenda mahakam za kadhi ni nani anakuwa muamuzi? Je, mirathi ambapo baba na mama walikuwa Waislamu lakini mtoto wao mmoja ni Mkristu na hatambui nguvu ya mahakama za kadhi ataomba haki yake wapi? Kwa hiyo kwamba Mahakama ya kadhi inawahusu Waislamu peke yake utaona haina mshiko vile vile kwa sababu kwa jinsi jamii yetu ilivyo Wakristu watajikuta wanaingizwa humo isipokuwa kama kuna kipengele ambapo mtu hata kama Muislamu ataamua yeye mwenyewe kesi yake iende wapi (state court system au islamic courts). Je, mahali ambapo Waislamu wawili wanaamua kwenda katika mahakama ya nchi (kama ilivyo sasa) itakuwaje?

c. Bahati mbaya Waislamu wanataka serikali iwasikilize na hata kupitisha sheria ya kutambua uwepo wa mahakama ya kadhi. Bahati mbaya zaidi hatuna bunge la Waislamu peke yao. Sheria yoyote ambayo itataka kujadiliwa na kupitishwa ni LAZIMA wabunge Wakristu wahusishwe. Vinginevyo, itabidi mtake Wabunge Wakristu wasishiriki mjadala na wala wasipinge wakae kimya na kuwaacha wabunge Waislamu wajadiliane wao wenyewe na kupitisha sheria hiyo. Hakuna NAMNA YOYOTE ambapo mahakama ya kadhi inaweza kuanzishwa Tanzania pasipo kuwashirikisha Wakristu kama serikali inatakiwa ihusike. Njia PEKEE ya mahakama ya kadhi kuanzishwa bila kushirikishwa Wakristu ni kwa Waislamu kuianzisha yenyewe. Kama tatizo ni uwezo wa fedha nina uhakika wapo watu wengi tu wanaweza kusaidia kuanzisha mahakama hiyo - Wakristu na Waislamu.

Mkuu nimekusoma lakini nasisitiza ni chuki, kiburi na mashindano ya bure dhidi ya waislamu wa Tanzania ndio inayokusumbua bila kujali hasara ambayo taifa litapata kadiri jambo hili linavyopigwa danadana miaka nenda rudi kwa hoja dhaifu kama hizo unazosema; mfano:

a. Unarudia issue ya gharama nimesema gharama inazugumzika kama ambavyo imezungumzika swala la MoU ya kikristo bila hata tatizo lolote labda wakristo waamue kuwa wachoyo kwa wananchi wenzao wanaotaka kuabudu vema dini yao. Pia sidhani kama kadhi courts inakataza mwanasheria aliyesomea sharia hata kama si muislamu kuwa kwenye jopo hilo ingawa nadhani kuwa kadhi mkuu itakuwa ngumu kutokana na kwamba jambo hilo ni kiislamu inabidi uamini katika uislamu..kwa hiyo gharama za kuendesha kadhi courts ni hoja dhaifu sana na ni uchoyo uliopita kiasi kwani hata sasa state courts zinahudmia waislamu je waislamu hao wakihudhumiwa na kadhi courts, state obligation inakwisha??

b. Pili unaongelea mgongano ikiwa kuna muislam mume na mkiristo mke, au ikiwa mtoto ni mkiristo na baba na mama ni waislamu itakuwaje?? mkuu unachoshindwa ku-acknowledge ni kwamba katika kadhi courts kuna wanazuoni, wataalamu ambao watakuwa wanatoa tafsiri na haki kwa wahusika wote. na ikiwa kuna mgongano wa hivyo lazima watatoa hukumu yao in case mwananchi hajaridhizika kuna options za kufanya..kwa ufupi ni kwamba KUNA MAJAWABU TUWAHESHIMU WANAZUONI WETU.

c. Swala la bunge: yes hilo ndio hasa ombi letu kwa wabunge wakristo wanakosa nini kwa waislamu kuwa na mahakama ya kadhi hadi wawe wachoyo na kushindwa kuangalia maslahi ya Taifa na umoja wa kitaifa na kuacha mashindano, kiburi na kuangalia umoja wetu?? hivi hawaoni hata aibu kama kenya ambayo waislamu ni wachache (wanalipa pesa kidogo serikalini) wanalipiwa na serikali yao ili kulinda umoja wao?? hivi hapa kwetu Tanzania tumekuwa wakristo sana kuliko nchi za kikristo?? kwa hiyo hoja si kujadiliwa na wakristo no, waislamu hawana cha kuficha kwenye mahakama ya kadhi, kujadiliwa na wakristo lakini tunashangaa wakristo kukataa mahakama ya kadhi kwa hoja dhaifu.. sana bila kungalia athari zake kitaifa??
 
Utasubiri sana. Wenye mada na washika mapembe wameikimbia mada yao baada ya wanawake wenye akili zao kumwaga ya moyoni. Mi nilifikiri kuna la maana wanataka kumbe ni ufukunyuku tu wa kutaka kudhulumu wajane urithi ili wasifanye kazi saa zote wawe wanacheza bao.

Kiukweli wanawake wa kiislamu wanatakiwa wasimame hasa ili kupata haki. Kumbe ukimuoa ukamla uroda ukikinai unaweza kumpa likizo kwa talaka 2, wewe unaoa mwingine yeye anasubiri. Ukipata hamu tena unamrudia, unaanza tena wallah mbona raha! Ngoja nitafakari other merits, kama vipi na mimi niingie kundini niwe nagonga tendegu naacha, nikipata hamu narudi tena naacha, hivyo hivyo kama mwongozo unavyosema. Haka kamchezo katamu, lazima tukaundie mahakama

Ukiacha ushabiki ukajifunza na kutafuta ukweli itakuwa bora kwako kuliko kupotosha watu kwenye mambo ambayo huyajui..

Nakushauri jiepushe kujibu "mambo ambayo hauna elimu/ujuzi nayo" maana unaonekana kituko mbele za weledi ..
 
Sijakuelewa una frustation yeyote na mume wako katika mahusiano yenu au??

Maana sijaona uhusiano wa mahakama ya kadhi na unachoongea wewe, kama mume wako ameshindwa 6X6 waweza kutafuta mwingine ..

Makubwaaa.sasa haya si matusi jamani???toa hoja kama alivotoa mwenzio...
 
Hivi kila anayepinga mahakama ya kadhi automatically anakuwa Mkristo?
Ask around pal, there are learned Muslim lawyers who know and understand that Kadhi courts cannot be funded or kick-started by the Government.
Mimi si muislam lakini naunga mkono kadhi court ianzishwe, ila iende sambamba na mfumo mzima wa sharia law kwa waislam watakao ridhia ili kupunguza watoto wa mitaani watakaokuwa wamezaliwa na vijana wenu lakini hawatambuliki na mahakama hizo za Kadhi. Sharia law inatakiwa iwepo ili kuwashughulikia wazinzi wanaozaa zaa ovyo nje huku wakijua watoto hao hawana chao kwenye mirathi. Na zaidi, mahakama hizo zianzishwe na waumini wenyewe wanaotaka.

Mkuu kwani kila muislam lazima aunge mkono??

Kuna idadi kubwa zaidi ya waislamu wanaunga mkono mahakama ya kadhi, inatosha kwa serikali kusikiliza madai yao muda mrefu kulinda umoja wa kitaifa kuliko kupiga danadana jambo ambalo naona litahatarisha amani ya Tanzania.

Swala la gharama ni hoja dhaifu sana iliyoegemea katika uchoyo, chuki na ukosefu wa upendo kwa wananchi wenzako wenye kutamani mahakama ya kadhi
 
Makubwaaa.sasa haya si matusi jamani???toa hoja kama alivotoa mwenzio...

Sijatukana mkuu, ila sijaona uhusiano wa mambo 6x6 na mahakama ya kadhi, besides this courts siyo mandatory ni choice so anaweza kutumia state courts if she so wishes.
 
Nafikiri wakristo wa Tanzania ndicho wanachotegemea waislamu wafanye vurugu ili waseme kuwa waislamu wameleta fujo nchini kumbe wameomba miaka nenda rudi lakini wananchi wenzao wakristo wenye madaraka wamekataa kwasababu ambazo hazina mshiko bali kuinyesha kiburi na mashindano...unafikiri wanigieria walipenda, unafikiri mataifa mengine walipenda na Tanzania ni tofauti sana??? BIG time NO ufa unaojengwa kwa mashindano ambayo yapo kwenye hoja ya gharama ni dhaifu sana...

Nimekuuliza wewe kama mkristo unakosa nini waislamu kuwa na mahakama ya kadhi???Tanzania

Umesha elezwa kwamba serkali haija leta uislamu wala ukristo! Kwa hiyo haiwajibiki kwa lolote kwenye kutekeleza ibada zenu! Mbona kwa maksudi hutaki kuelewa? Unaye mtisha nani? Lianzishe shetani akutie adabu umjue MMungu, anaye wapa wema na wabaya! unasubiri nini? unachelewa!
 
Naona wewe ndio unaanza kutisha watu eti tutiwa adabu?

Pamoja na kwamba serikali haijaleta dini lakini serikali inaamini kuwa wananchi wake wanazo dini..

Na wanatakiwa wafanye ibada kikamilifu..
 
@shizukan
Wanawake waislam wanapenda hukumu za kiislam sana tu, na katika jamii inayoongoza kwa kuingia katika haki ni wanawake duniani ..

naomba ujibu yale maswali with intellect, siyo ushabiki bearing in mind tuna waislam 50% in Tanzania ok
Acha kudanganya jamii wewe!
 
Sijakuelewa una frustation yeyote na mume wako katika mahusiano yenu au??

Maana sijaona uhusiano wa mahakama ya kadhi na unachoongea wewe, kama mume wako ameshindwa 6X6 waweza kutafuta mwingine ..

ahahahaaa!
Hapo peke yakn umeshindwa subra! omba ffu wakusaidie kulazimisha unacho amini wewe!
 
Naona wewe ndio unaanza kutisha watu eti tutiwa adabu?

Pamoja na kwamba serikali haijaleta dini lakini serikali inaamini kuwa wananchi wake wanazo dini..

Na wanatakiwa wafanye ibada kikamilifu..

Wajibu wa kufanya ibada kikamilifu ni wa muumini muhusika na si wa serkali! kama umeshindwa kuwaaminisha, wafuasi muombe msaada allah wako! au hawezi! sio serkali haina wajibu wa kuchonga misalaba, wala, kuwapeleka hija maka! badala ya kuidai serkali, Elimu, Tiba, hata angalau tupate rakaa1! unadai kisicho wahusu!
 
Topica turudi nyuma Hii ni commnet no 9 ambayo nina hakika ulijibu kisiasa saabu thread ilikuwa kwenye jukwaa la siasa sadly bila kufuta vigezo vya tiitle ya thread yako ( intellectual). Kwa kuwa sasa imekuja kwenye jukwaa la sheria Tuutoke kwenye kwenye kona ya dini tulizopo. Then naomba tena majibu yako ya ki- intelectual kwa mara ya tena

Fahari said:
.......Kama kweli unataka so called "Intellectual Arguments" basi ungeweka hii mada kwenye jukwaa la sheria ili watu wajadili kisheria sheria na kikatiba katiba. Zaidi ya hapo itakuwa n ihisia na ushasbiki wa kidini. ukichanganywa na siasa.

je wewe kama ungekuwa mwanasheria mkuu wa serikali uko tayari kurushu na kumshauri raisi akubali kuingiza rasmi mfumo wa mahakama za mila za wajaruo, wahaya, na makabila mengine kwenye mahakama ya JMT.

Topical said:
ni makosa kulinganisha wahaya na uislam ok..

Je intellectual argument yako kwa hoja yangu bado ni kuwa ni makosa kulinganisha tarataibu za mirathi za wahaya , wajaruo wazanaki na wengina na za waislam au wakristu? Kama ni Makosa kivipi.? ok fafanua
 
Kwa jinsi nielewavyo mimi kuwa hiyo Mahakama ya Kadhi wanayoitaka Waislam waTanzania itakuwa inashughulikia masuala mawili kwa sheria zake nayo ni (1) mambo ya ndoa na (2) Mambo ya Urithi (Mirathi) tu mambo mengine ya Sheria itahusu ni Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndugu zangu Wakristo na wale wasiokuwa wakristo musiogope, hiyo Mahakama ya Kadhi kuanzishwa na waislam hakutokuwa na mambo ya vurugu wala Vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vilivyotokea Nigeria musiogope wapeni Uhuru Waislam wajiamulie kivyao katika mambo yanayohusu Sheria za dini yao asanteni natanguliza hivyoo.
 
Unajua watu hawaelewi..Waislamu hawajakatazwa na wala wakristo hawaogopi..si wameambiwa waanzishe lakin serikali haihusiki wla hela za wavuja jasho makafiri hazitahusika????????
 
Unajua watu hawaelewi..Waislamu hawajakatazwa na wala wakristo hawaogopi..si wameambiwa waanzishe lakin serikali haihusiki wla hela za wavuja jasho makafiri hazitahusika????????
Kama ni hivyo basi Waislam watanzisha hiyo Mahakama ya Kadhi na wala hawata tegemea hela za hao wavuja jasho na hao makafiri, katika hii dunia Waislam ni matajiri sana ukiangalia wewe huko Uarabuni kuna nini kama sio Mafuta? na hayo mafuta ndio yanayoendesha hii dunia ya sasa bila Mafuta hakuna

viwanda wala magari wala mashine wala hakuna kitu kitakachokwenda wakianzisha hiyo mahakama ya kadhi waislam wa Tanzania watapata misaada toka kwa wafadhili toka nje IRAN,SAUDIA ARABIA na nchi nyingine nyingi za kiislam upo pamoja na mimi?
 
Kama ni hivyo basi Waislam watanzisha hiyo Mahakama ya Kadhi na wala hawata tegemea hela za hao wavuja jasho na hao makafiri, katika hii dunia waislam ni matajiri sana ukiangalia wewe huko uarabuni kun anini kama sio Mafuta? na hayo mafuta ndio yanayoendesha hii dunia ya sasa bila Mafuta hakuna

viwanda wala magari wala mashine wala hakuna kitu kitakachokwenda wakianzisha hiyo mahakama ya kadhi waislam wa Tanzania watapata misaada toka kwa wafadhili toka nje IRAN,SAUDIA ARABIA na nchi nyingine nyingi za kiislam upo pamoja na mimi?
Sasa wanalialia nini?si wameruhusiwa waanzishe wenyewe?vinginevyo huu mjadala hauna maana....hela za mafuta si mnazo???????
btw...nimegundua sio waislamu wote wanaitaka hii mahakama..kuna kundi la wanawake wapo AGAINST na hii kitu..nadhani hata ndani ya uislamu mnalazimisha mambo...
 
Tunachotaka ni kuwa serikali iruhusu tu Sheria yetu ipitishwe kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano na Rais Atie saini yake. Wanawake wanaopinga wanapinga Sheria ya Dini na hao wanaopinga watakuwa wengi wao hawajuwi nini maana ya sheria ? Na Sheria ya dini ya kiislam haimkandamizi Mwanamke sheria itakayotumika ni ya mambo ya Ndoa na mirathi tu hakuna mambo ya kulazimishana kuvaa kininja kujifunika gubi

gubi Mwanamke wa kiislam anatakiwa avae kiislam na kujifunika mwili wake aache viganja vya mikono na uso wake. Tunachotaka sisi Waislam hakiyetu kuhusu hizo sheria mbili ndoa na Urithi tu mambo mengine tunaiachia Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano. Mimi ninakuona wewe unakuwa kam msemaji wa hao wanawake wa Kiislam vile ? Nalog off
 
Uislaam haufuati maoni wala maelezo ya mtu ! Haya mambo yote ya refence tunafuata (Quran) hivyo wewe huna expertise yeyote ya kufanisha hili wala lile ! Dhulma ni dhambi kama kuabudu msalaba!

kwa hiyo kwa akili yako huoni ni dhulma kuchukua kodi ya wasio waislamu kutegemeza uislamu?
 
Tunachotaka ni kuwa serikali iruhusu tu Sheria yetu ipitishwe kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano na Rais Atie saini yake. Wanawake wanaopinga wanapinga Sheria ya Dini na hao wanaopinga watakuwa wengi wao hawajuwi nini maana ya sheria ? Na Sheria ya dini ya kiislam haimkandamizi Mwanamke sheria itakayotumika ni ya mambo ya Ndoa na mirathi tu hakuna mambo ya kulazimishana kuvaa kininja kujifunika gubi

gubi Mwanamke wa kiislam anatakiwa avae kiislam na kujifunika mwili wake aache viganja vya mikono na uso wake. Tunachotaka sisi Waislam hakiyetu kuhusu hizo sheria mbili ndoa na Urithi tu mambo mengine tunaiachia Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano. Mimi ninakuona wewe unakuwa kam msemaji wa hao wanawake wa Kiislam vile ? Nalog off

kwani Mkuu Mmkavu! kwa nini msiidai serkali kuboresha maisha bora, tupate angalau rakaa1, badala yake tunajitaahidi kukamua beberu maziwa? utapasua pumbu za beberu na maziwa hupati!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom