Wanaosababisha mgongano CCM kung'olewa


Karamagi aliposaini mkataba wa Buzwagi alikuwa yeye, Lowasa na Executives wa Barrick.......... Nani alivujisha habari?????
 
Hakuna sehemu duniani ambako mafisadi hakuna. Inategemeana ni mafisadi gani. Usiote ndoto chovu kwmaba kuna siku mafisadi wataisha Tanzania. No way!
Ufisadi upo sehemu nyingi duniani lakini siyo wa kiwango cha kijinga na kipuuzi kama huu wa Tanzania. Kila kitu kina mwisho hawa mafisadi wana mwisho wao, Mwisho wa muda wao haujilikani, inaweza ikachukua muda mfupi au mrefu.
 
Mimi sijui ni kwa nini haya maamuzi yanacheleweshwa hivyo.
FUKUZA FUKUZA FUKUZA tena haraka sana, sio tu kwenye chama hata ingewezekana tufukuze hii mijitu hapa nchini. Longo longo zimezidi mimi nasubiri actions hapo ndipo nitajua kweli kuna hata chembe ya dhamira. Tuache bla bla..
 
nasoma kati ya sentensi zenu, nagundua ni hisia za ndani ambazo mtu anaweza toa juu ya mustakabalai wa maisha yake ndani ya eneo lake na jinsi gani angependa mammbo yaende.

huu ni mtazamo thabiti na kwamba sina kipingamizi nao. ni mtazamo ambao kwa kweli ingekuwa katika nchi zile ambao responsibility ya ofisi inaenda kugusa hata maisha binafsi ya kiongozi . ni sehemu nyingi sana kwa mfano japan, nimekuwa nasikia mara nyingi viongoai wakifanya hivyo. kwa mara ya kwanza ikiwa baada ya yule Gen.Takinawa aliporuhusu kulipuliwa bandari ya pearl harbour, miami.

turudi kwenye article yetu.

ni ukweli kwamba said kubenea kaandika na si vizuri kuanza kuangalia kaitoa wapi habari hii. kama imevija kweli kutoka kwenye kamati au la , hilo sio letu . kubwa zaidi hebu tuangalie na kujadili kama hili lisemwalo katika habari hii likawa kweli.

KUFUKUZWA KWA WALE WANAITWA MAFISADI

kama kamati ya mzee mwinyi imeona hili ni jambo la kufanyika mie mawazo yangu, yanaungana naye moja kwa moja lakini nina mambo ambayo ningependa kama kamati iyaangalie.

je , kuwafukuza chama ni hatua ya kuonyesha kuwa wamethibitisha tuhuma hizo..................

na je maamuzi au maoni ya namna hii hayana shindikizo lolote......

kama maswali hayo mawili yana majibu ambayo hayaonekana kusukuma matokeo ya kikao cha kesho kutwa.mie ushauri wangu ni kwamba viongozi hawa ni vyema wangekubalia wenyewe kujiuzulu kabla hawajafukuzwa kwa kweli.

mie nilikuwa nafikiri ili kulinda heshima zao, ni vyema wakaamua kujiuzulu. maana angalia leo hii mh.lowasa baada ya kujiuzulu....

hawajifunzi hapo.mie nafikiri kama hawataki kufanya hivyo basi vikao vikae na kujadili.

lakini kama walivyosema baadhi ya wang'amuzi hapo juu, vipi kuhusu ukweli wa habari yenyewe... mie pia naomba nimuachie mzee mwinyi na kamati yake watuleteee mambo hadharani.

pia ningesikia raha sana kwa chama hiki tulichokiasisi wakati tukiwa shuleni na mwalimu julius kinawapa onyo au adhabu stahiki wale wanaopiga kelele ovyo , ambao wamefika sehemu wamesahau kuwa chama ni vikao na vikao vyenyewe ndiyo kama hivi wanavyokutana keshokutwa.

ni muhimu nec ikawafunga mdomo.

haya ni maoni yangu.sidhani kama kutoka kwenye chama au kujiunga na chama chengine ni suluhu.
 
Best option ni kuyapatanisha makundi hayo mawili. Nionavyo mimi kundi la akina Seleki na wenzie ndiyo watakaokataa. Basi wakatae na kama wanataka wajitoe CCM na wakaanzishe au wajiunge na vyama vilivyopo. Kama wao ni maarufu kwenye majimbo yao tutaona baada ya uchaguzi mkuu. Hao wakitoka CCM haiwezi kusambaratika.Kwani akina Seleli hawatakuwa wa kwanza. Mbona CCM siku nyingi imekuwa inakimbiwa na watu wa maana wengi tu lakini wanajikuta nje ya CCM hawana bao. Halafu wanarudi tena. Kwani hilo kundi la akina Seleli mnafikiri wote watashinda ubunge? Hakuna kitu. Wao waacheni waende. Kuwafukuza akina EL, RA, AC na NK is not a panacea. Kama hao ni mafisadi hao waliobakia siyo mafisadi? Hebu acheni hizo bwana.!!!

Ndugu zangu siku za karibuni wamekuwepo baadhi ya wanasiasa na hata Watanzania wenzetu wakiwalaumu wale wote waufanyao ufisadi. Kiasi kwamba unapata picha kuwa hao watu wanawaowalaumu wenzao ni wasafi kuliko. Ninakumbuka Yesu alipopelekewa yule mwanamke mzinzi na mafarisayo wakitaka apigwe mawe, Yesu akawauliza kama na wao walikuwa hawana hatia ya dhambi ya uzinzi. Maajabu ni kuwa walishindwa kumtupia mawe kwa sababu na wao hawakuwa safi. Naye mtakatifu Paulo kwenye Warumi 2:1 anasema.."kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia (kwa nini?) kwa sababu wewe uhukumuye wayafanya yale yale". Hao hawatajiepusha na hukumu ya Mungu(2:3).
Wabunge hao wanaowasakama wenzao kuwa ni mafisadi bila ya kuwaeleza Watanzania ufisadi wao ni nini na ni upi, wao wenyewe ukifuatilia jinsi walivyopata ubunge utagundua wote walitumia njia za ufisadi kupata nafasi hizo. Wanafiki wakubwa hao hawana agenda nyingine zaidi ua kuiingiza nchi kwenye machafuko.
 
yetu macho yakhe
majambazi majambazi tu
 


One can ask himself, kweli mwinyi, mwasisi wa ufisadi, ambaye katika kipindi chake Lowasa, rostam na wengi walianza harakati za kujitajirisha kupindukia anaweza kuja na suluhu ya kuisafisha sisiemu ili hali yeye ndiye aliyeasisi uvunjanji wa miiko ya uongozi alipofutilia mbali azimio la arusha lote? (heri baadhi ya vipenge angevibeba)
leo hii anaweza kuwa mtume airekebishe ccm??????? WHAT A JOKE!!!!!!

CCM HAS LOST ITSELF IN A JUNGLE, THIS COUNTRY NEEDS ANOTHER PARTY. period
 

lazima uko katika payroll ya mafisadi, si bure. your comment stinks!!!!!
 

Be careful when you quote anything from the bible my friend
 

nitajie vijana watano tu (under 45) amambo ni mawaziri au wabunge toka vyama vyote wamefanya kazi as example ku justify mawazo yako.

usipoweza basi ondoa hicho kipengere haraka sana.
 
These Four guys are very powerful inside CCM, untouchable in other worlds. kuwafukuza hawa jamaa wanne lazima CCM itameguka makundi 2 na ndiyo utakuwa mwisho wake. Believe me.

Mfano mdogo tu kukuonyesha Lowassa ana nguvu kwenye CCM kwamba akiamua kugombea Uraisi kwa CCM 2010 na Kikwete, nomination ndani ya CCM lazima lowassa amgalagaze mukulu wetu sababu jamaa kasheheni wajumbe kibao Kamati Kuu, NEC na wanachama kwa ujumla wanaomsapoti, kumbukeni hawa jamaa wali pray great role kwenye mtandao wa 2005. hizi ni number mbaya hasigusiki hata Yusuf anajua hilo.

Kukuhakikishia hilo fuatilia kikao cha Halmashauri kuu miezi kadhaa iliyopita yaliyotokea wakati Samweli anataka kupokwa kadi yake.

Kwa hiyo kuna mawili
a) Hawa jamaa hawatafanywa chochote kukinusuru chama chao, ingawa kufanya hivyo chama kitazidi kupotea imani kwa wananchi wake.
b) In case wakiamua kuwatimua ujue CCM ndiyo mwisho wake umefika, na vyama kama CCJ na
Chadema vitaibukia hapo kuwa na nguvu za kuchukua dola.

Sasa mimi naona watachagua A.
 


Ukiacha ubunge ambao hawata poteza ila iwapo tu watavuliwa uanachama wa CCM, je wanne hao wana madaraka gani tena ndani ya chama ukiondoa ujumbe wa NEC?
 
CCM haihitaji mabadiliko kwani haijawa na sera mpya ambayo haikuwa nayo tangu kuundwa kwake. Kwanza CCM kama chama ndiyo fisadi anayejilimbikizia mali. Angalia baada ya kusoma upepo wa vyama vingi imejimilikisha viwanja vya mpira na maeneo yote ya wazi. Vyote hivi vilichangiwa na watanzania wote kabla ya vyama vingi kwa sababu wakati huo chama kimeshika hatamu na chama ndiyo serikali. sasa iweje CCM kama chama wanyang'anye mali zote hizo kwa kubatiza kuwa ni za kwao (CCM ni mnyang'anyi). Tuache "individualism" CCM kama chama ndiyo kimeoza pamoja na sera zake za ubinafsi na kudanganya na kutia hofu kwa wananchi eti kuwa chama kingine kitashindwa kulinda amani yetu, ukijiondoa CCM utakuwa maskini, etc. hapa inaonyesha wazi kuwa CCM kama chama inaingilia serikali katika utendaji wake na ndiyo maana wanaweza kutoa kauli kuwa hapa hamna maendeleo kwa kuwa mmechagua upinzani..rejeeni kauli za mropokaji makamba na wenzake...
Tufike wakati tufikirie kwa kina na kufanya maamuzi yenye kuleta tija na tuachane na kunyooshea mtu mmoja mmoja kidole. Tufanye "overhaul" ya system, na hii hutaweza unless ung'oe mizizi yote na mizizi yenyewe ni CCM.
 
Ukiacha ubunge ambao hawata poteza ila iwapo tu watavuliwa uanachama wa CCM, je wanne hao wana madaraka gani tena ndani ya chama ukiondoa ujumbe wa NEC?
Ukiangalia hao wanaojiita vinara ndiyo usisema kwanza wanakula rushwa na ufisadu wao ni wa kijinga kama ule wa Ole..ambaye anang'ata na kupuliza, mbona nasikia alipewa mchanga tanzaniteone ili fedha itakayopatikana apelekee maendeleo kwa wananchi wake lakini kachikichia yote mwenyewe...kuna mengi sana lakini unahitaji kutumia jicho la tatu..
 
si sahihi Nanu kusema kua hao wanaojiita vinara wa ufisadi ndio wa kwanza kula Rushwa, ,.......kama unakubali kua rushwa mbaya, sema usiogope, simama sema, kama unao ushahidi kuwa wanakula rushwa waseme, toa taarifa sahihi kabisa , uone kama hawafuatiliwa.
kama Lowasa . na kina Rostam si mafisadi leta ushahidi wako hadharani, watetee kwa hoja sii kusema kuwa wanaosema hao ni wezi wankosea kwa sababu nao ni wezi...jibu hoja kwa hoja ,acha utetezi rahisi Mtanzania mwenzangu
 
Nguvumali, hatetewi mtu hapa ng'o!!!! Ninachosema CCM yote imeoza hata hao wanaosema wapambanaji wa ufisadi pia ni mafisadi.... tunahitaji "overhaul" ya system na hii ni kwa kuwapa wapinzani viti vingi bungeni!!!!
 

Naungana na wewe kabisa mkuu hawa watu wanne wana mizizi tena mikubwa ndani ya CCM na kama CCM wakikosea step katika maamuzi yao ndiyo CCM bye bye

Kama ninavyosema kwa hili CCM imeshikwa pabaya option yeyote kwa hawa jamaa ina madhara kwa CCM kwamba wakiamua kuwafukuza jamaa hawatakubali kukaa kimya lazima watarudi tu kwenye siasa kwa staili nyingine ama kuanzisha chama au kusabotage CCM

Kama CCM wata opt kutowafukuza tuseme kuwafumbia macho kitu ambacho nafikiri ndiyo lengo la CCM humo ndani hakutakalika lazima dume moja atafute zizi jingine hali ilivyo sasa CCM ni kama msemo wa kule kwetu kusini ukikaa nshale ukichimama nshale sijui utaamua nini kukimbia sasa CCM ikimbie na tuone mbio zake.
 


kifeeeeeee!!!
 

some corrections
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…