Wanaosema lile ni goli na wanaosema sio goli wote wana hoja, matusi ya nini?

Wanaosema lile ni goli na wanaosema sio goli wote wana hoja, matusi ya nini?

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kumeibuka mabishano makubwa baada ya goli la Aziz Ki kuonekana halikuwa goli, hasira na ghadhabu za wanayanga ni za kiwango cha kimataifa, sijui ingekuwaje kama ngoma ingepigwa kwa Mkapa na matokeo yangeishia kwa Yanga kutolewa kwa penati.

Wapo wanaosema lile ni goli kabisa, limevuka mstari wa goli, kwamba refa kawanyonga, tena wamekwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa Rais wa CAF ndio RAIS wa Mamelod, hivyo refa alikuwa na maelekezo.Wanaosema lile ni goli wamehoji kwanini refa hakwenda kuhakikisha mwenyewe kwenye VAR (sio Goal line technology) ili kumaliza utata? Mbona alienda kwenye tukio la Lomalisa? Imefikia hatua Kalikonji zungu pori ambalo linataka lionekane kuwa lina mahaba kweli kweli na Yanga likamtafa DM refa na kuanza kumshambulia kwa maneno makali kwanini ametenda uhalifu.Zungu pori ambalo limedhihirika kuwa limbukeni la wanawake likahitimisha kwa kumtaka refa aombe radhi.

Sasa kuna wale washabiki wengine wanaosema lile halikuwa goli kwa sababu mpira haukuvuka wote kwenye mstari kwenda kimiani.Matukio kama yale, wanaoshabikia hoja kuwa lile sio goli wamepost video mbalimbali zikionyesha kuwa mambo kama yale kwenye mpira ni ya kawaida sana, yameshatokea mara kibao, hivyo Yanga wasilie lie.Wao wanaiona Yanga kama wamepata sababu baada ya kuona mashabiki wao wameshaingia kwenye mtumbwi wa kibwengo kwa kuona refa kawaonea, mitandano mbalimbali ya kijamii imeonyesha wachambuzi na wataalamu wa masuala ya technology za VAR na Goal line technology wamechambua na kubaini dhahiri shahiri kuwa lile halikuwa goli, hata hivyo mashabiki wa Yanga hawaelewi hilo, wao wanajua wanacheza nusu fainali na Esperance ya Tunisia tu.

Kuna wengine hawa sasa ni kundi la tatu, hawa wanasema mzoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi, wao wanasema Yanga wameshabebwa sana kwa matukio kama hayo, washafunga goli vs azam wakati mpira umetoka, Lomalisa akaurudisha ndani akapiga krosi watu wakaweka kamba, azam kwa vile hawana baba wala mama wakaweka kati na walikufa siku ile, Yanga na Ihefu pia Max Nzengeli alipiga mashine ikapiga juu haukuvuka mstari refa akaweka kati.Matukio ni mengi lakini wenye kushadidia hoja hii wanaitaka Yanga ishukuru mungu kwa sababu wao ni wanufaika na kaya maskini za TASAF kwa mtindo huu.

Hawa wote kwangu wana hoja.Lile ni goli, nakubali, lile sio goli nakubali pia, Yanga na nyie mbona haya mambo mmeshanufaika nayo sana pia nakubali.

Sasa wajibiwe kwa hoja sio matusi kuwa wewe fala, wewe cjui mamako yuko hivi, wewe cjui taahira, yanasaidia nini? Kufanya hivyo kunaendelea malumbano na tunaonekana wehu waheed kama Zungu pori.
 
Watanzania hamjui mpira tulieni na ccm 😁😁😁😁
 
Mpira mzuri upo ulaya huko Hadi una enjoy 🤣🤣🤣 watu wanagusa Mali
 
Bado mnajadili ile mechi ya WABABE MASANDAWANA?

Utopolo wamefanya DHULMA ngapiii? Leo hii ni kama vile Malaika..
 
Hawawezi kuwa na hoja wote wawili wakati uhalisia ni mmoja. Fact ni moja tu kati ya mambo haya mawili: goli ama sio goli!

Maana yake ni kwamba, mmojawapo hapo ndiye anayeweza kuwa mwenye hoja. Sio wote wawili.
 
Back
Top Bottom