Wanaosema tafuta hela kila Post

Ni hivi kila mtu anayepost kaumizwa na mapenzi wadau wanasema atafute hela, mie nauliza hizo hela inatakiwa ziwe kiasi gani?
Tena waambie kuwa kila mtu anazo zake kulingana na kupambana na kuwajibika kwake.Wasitunyanyase.Hizi kidogo tulizo nazo zinatusaidia na hizo nyingi zitakuja tu.




"Hata watu wa chini tunahitaji faraja"
 
Mwenye pesa mapenzi hayamuumizi kama asyekuwa nazo kabisa" ukitaka kuamini hilo we zitafute tu uwe nazo nyingi ...
 
Watu wasio na hela ndo maswala yao hayo hua wanaamini wakiwa na hela mambo yatawaendea vizuri..kwenye maswala ya mahusiano wanashindwa kujua kwamba mwanamke anaekufata kwa ajili ya hela huyo ni golddigger...ndo hao hao hua wanashangaa mwanamke nampa kila kitu lakini amemsaliti etc...kwanza unazitafuta hizo hela nani aliezipoteza? ....
 
We tafta ela ili asipokuheshimu wewe aheshimu pesa zako
 
Endelea kutokutatafuta ipasavyo the ndio utaelewa. Halafu usikubali ama kutoa nafasi itakayofanya mapenzi yakupelekesha ama kukuumiza. Jifunze vizuri psychology inayotawala hawa viumbe itakusaidia.
 
Nyie ndio wale wa machupa ya soda?..pesa sio kila kitu hapa duniani niamini mimi ninachokuambia.

Machupa gani ya soda? Basi mimi bado sijafika hatua ya kuelewa pesa sio kila kitu nadhani nikifika hapo ntakuelewa
 

Tukifanya tu conclusion ya ulichoandika
Tutafute tu hela mkuu au[emoji23]
 
Mwenye pesa mapenzi hayamuumizi kama asyekuwa nazo kabisa" ukitaka kuamini hilo we zitafute tu uwe nazo nyingi ...

Embu mwambie tu mkuu
Ukiwa na hela akaondoka Amina akikohoa tu anakuja Zubeda [emoji23][emoji23][emoji23]
Nasema uongo kwan?
 
Ni hivi kila mtu anayepost kaumizwa na mapenzi wadau wanasema atafute hela, mie nauliza hizo hela inatakiwa ziwe kiasi gani?

Tafuta hela na usikilize Wenye uzoefu; wana nia nzuri; we tafuta tu mpaka uwe top and comfortable, vitu muhimu: 1. ibada na kutumika Kwa Mungu:

2. Tafuta hela.
3. Lea familia
4. Tafuta hela
5. Tafuta hela tena
6......
1000000. Tafuta hela .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…