The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Huko kaskazini mwa Tanzania, zaidi ya wakazi 70,000 wa jamii za Kimasai wanakabiliwa tena na kufukuzwa kutoka kwenye ardhi ya mababu zao baada ya serikali kuweka wazi mipango ya kukodisha ardhi hiyo kwa kampuni kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu - UAE, ili kuunda ukanda wa wanyamapori kwa ajili ya UWINDAJI wa NYARA na UTALII WA KIDOSI au UTALII WA WATU WENYE KIPATO KIKUBWA (Elite tourism).
Viongozi wa Wamasai wamewasilisha shauri katika mahakama ya mkoa, wakitaka kusitishwa kwa mipango yote ya kuwaondoa kwenye eneo hilo kwani ni sawa na uporaji wa ardhi yao.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Mkuu wa Mkoa aliwaambia viongozi wa Maasai kuwa ukodishaji wa ardhi ni kwa maslahi ya taifa ili kuongeza mapato ya utalii wa nchi na ni uamuzi mgumu kwa serikali kufanya.
Serikali inadai wakazi watakaofukuzwa kutoka Loliondo watahamishwa hadi eneo jirani la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA), ambapo wataungana na Wamasai wengine 80,000 waliofukuzwa hapo awali.
Mnamo mwaka wa 2018, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) ilitoa zuio kwa serikali ya Tanzania ilipotaka kuwaondoa Wamasai kutoka eneo la kilomita za mraba 1,500 (maili za mraba 580) zilizosajiliwa kisheria katika tarafa ya Loliondo, Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania.
Leo, wafugaji 70,000 wa kimasai wako hatarini tena kufukuzwa baada ya serikali kuweka wazi mpango wa kukodisha ardhi hiyo kwa Otterlo Business Corporation (OBC), kampuni yenye makao yake makuu katika Umoja wa Falme za Kiarabu, wanaotaka kufanya uwindaji wa nyara na utalii wa matajiri.
OBC ni kampuni ya uwindaji inayosemekana kumilikiwa na familia ya kifalme ya UAE. Kulingana na Taasisi ya Oakland, chombo cha wataalam wa sera kilichoko Marekani, OBC itakuwa ikidhibiti uwindaji wa kibiashara katika eneo hilo.
Siku za nyuma, kampuni hiyohiyo ilishawishi serikali kuwafurusha wamasai katika eneo hilo na kisha kufanya uwindaji wa maelfu ya wanyama adimu katika eneo hilo, wakiwemo simba na chui.