Wanaosherekea kifo cha Magufuli wanafukuza mwizi huku wameacha mlango wazi

Wanaosherekea kifo cha Magufuli wanafukuza mwizi huku wameacha mlango wazi

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kuna wengi wanaolalamika kwamba walipatwa kuumizwa na utawala wa magufuli. Kuumizwa huko kunahusishwa kibinafsi na utawala wa Magufuli, ikimaanisha walipitia waliyoyapitia tu kwa kuwa Magufuli alikuwa rais.

Wanaolalamika sio wapinzani pekee bali pia wako wanachama wa chama cha mapinduzi ambao wanaona kwakweli Mungu aliwatetea Kwa kumtwaa Rais.

Sehemu kubwa ya malalamiko haya yanatokana na ukweli kwamba katiba ya Tanzania inampa rais madalaka makubwa sana, Kwa kiwango ambacho ana ruhusiwa kuyatumia hata kwenye mitazamo binafsi hakuna mamlaka ya kumuingilia.

Kwa msingi huo nawashangaa sana hasa makada wakubwa ndani ya chama tawala ambao wako bize kufurahia kifo cha marehemu badala ya kuondoa mianya inayoweza kuwaletea Magufuli mwingine au hata zaidi ya Magufuli.

Kwa sababu kwa katiba ilivyo sasa ina mfanya rais kufanya chochote anachoona na asiulizwe wala kuzuiwa na mtu yeyote.

Mnaweza mkawa mmekomaa na kufurahia mkajikuta mara ghafla akapenya mtu wa kaliba ya Magufuli akaikatisha furaha yenu kabisa.
 
Duu ngoja tuendelee na mtori nyama zipo chini...!
 
Kwa hiyo walichotaka ni rais anayetumia madaraka yake ya kikatiba kutetea maslahi ya walio wengi.

Mtu anayetumbua fisafi popote walipo na wazembe kwenye utumishi wa umma.

Hiki ndio walio wengi wanataka. Kwa hivyo hata msipolala mlango wazi wananchi watatafuta magufuli mpya.

Kutokana na roho zenu mbaya hamuwezi hata kusema kwa nini mnachukia kiongozi kama magufuli.
 
Back
Top Bottom