Wanaosoma shule za binafsi kuchangia madawati kwenye shule za umma

Wanaosoma shule za binafsi kuchangia madawati kwenye shule za umma

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Nina wazo "jipya" kidogo, tulijadili... Ingawa nimetumia neno madawati katika title, hapa namaanisha kuwa maendeleo kwa ujumla, (lakini ya manunuz tu, sio vikao), kama vile vitabu, vifaa vya maabara, madawati, ujenzi wa maabara nk...

Katika kujaribu kuongeza ubora wa elimu kwenye shule za serikali, napendekeza kuwa serikali iweke utaratibu wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule za watu binafsi au mashirika, wachangie fedha kuendeleza shule za serikali. Hii ni kutokana na:

1. Pamoja na madhaifu mengine, uboreshaji wa shule za umma unalegalega kutokana na wadau wengi wenye uwezo kifedha na kielimu kupeleka watoto wao shule za private, hivyo kukosa "uchungu" na shule za umma ambazo zinakuwa na wanafunzi zaidi ya 95% kutoka familia masikini. Kutokana na hilo, maboresho ya shule za umma ambayo kwa siku za nyuma yalikuwa yanasimamiwa na bodi za shule na wadau wengine kama walimu, viongozi wa serikali, wafadhili na wanasiasa yanasuasua kwani siku hizo hao wote hawana watoto wao huko...

2. Kuweka "tozo" kwa mfano la asilimia fulani ya ada na michango ya kila mwaka kwa kila mtoto anayesoma shule ya private ziende moja kwa moja kuchangia shule za umma, kutawafanya wazazi na wadau wote wanaopeleka watoto wao huko wawe na uchungu na shule za umma kwani. Asilimia zitakazochangiwa ziongezeke sambamba na kiasi cha ada (kama PAYE). Yaani kwa mfano, kama shule michango yake ni chini ya 1,000,000 basi tozo liwe 10%. Kama ni m 1 - m <1.5, iwe 15%, kama ni m 1.5 - < m2.0, iwe 20% na kadhalika...

3. Kuweka tozo la namna hii, kutafanya wamiliki wa shule za private wasitoze michango mikubwa sana kwani watajua kwamba michango inapozidi kuwa mikubwa, na tozo linazidi kuwa kubwa, hivyo kuhatarisha kukosa wanafunzi. Hii itapunguza ada kubwa sana tunazoona kwenye shule za private sasa...

4. Kama michango hiyo itasimamiwa sawa sawa, miaka kadhaa ijayo shule za umma zitakuwa level moja kiubora na shule za private, na hii itasaidia kupandisha kiwango cha taaluma ya wanafunzi, bila kujali kama mmoja anatoka familia masikini na mwingine tajiri...


Hata hivyo, ili kuwezesha mpango huu usiingiliwe na ufisadi, ni lazima sheria iwekwe kuwa fedha zitakazopatikana kwenye mpango huo zinakwenda moja kwa moja na kwa 100% kwenye manunuzi au ujenzi wa vifaa vilivyoanishwa. Na katika kuwezesha hili, uwekwe utaratibu kuwa fedha zinazotoka kwenye shule za private zitachangia mathalani 40% ya manunuzi specific kwenye shule za umma huku 60% zikichangiwa na ada inayopatikana kwenye shule hizo za umma. Ikumbukwe kuwa shule za sekondari kwa mfano zina ada ya sh 20,000 kwa mwaka, hivya kwa mpango huu, unavyokusanya zaidi, ndivyo unavyopokea zaidi. Wakuu wa shule wapewe changamoto katika hili...


Ingawa najua wazo hili lina changamoto nyingi, nakaribisha mjadala, na nitafurahi kama watu wakija na maboresho pia...
 
Back
Top Bottom