Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Si vyema kuwa na mahaba na dini yako mpaka unapitiliza mipaka ya utimamu wa kawaida wa akili(common sense) na kugeuka kituko.
Naona mitandaoni baadhi ya watu wanakazana kusambaza taarifa ya Kim Kiduku wa Korea Kusini kusilimu na kuwa muislamu, kwanza kwa kiasi kikubwa taarifa hii inaonekana ni uzushi ukizingatia Wakorea wanavyopenda kitimoto, sidhani kama unaweza kumuambia Kiduku aache kula kitimoto akakuelewa .
Huu mtindo wa kutangaza habari za watu kusilimu mara kwa mara au kukumbushia historia za watu waliosilimu ni aina fulani ya ujuha. Mfano wiki kadhaa tu zilizopita kulikuwa na taarifa ikisambaa sana ya Pierre Liquid akisilimu. Hadi na vi-online TV vilikuwa vinarusha matangazo live ya hilo tukio! Nashangaa sana kwamba bado kuna watu wanaishi zama hizo za kijima za kutambiana kubadilisha watu dini kwa kuonyesha mtu fulani maarufu amebadilisha dini, sijui huwa wanalenga nini wanaofanya matangazo ya aina hiyo karne hii.