mediaman
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 451
- 688
Baba yangu mzazi aliishi maisha ya dhiki sana. Alikuwa mfanyakazi aliyepata mshahara mzuri tu lakini mshahara ulikuwa haumsaidii kuishi vizuri kwa sababu ya ulevi. Mwisho wa mwezi, akishapokea mshahara tu alikuwa anakesha sehemu wanazouza bia akinywa na kuwanunulia bia marafiki zake. Wanawake walikuwa wanamganda sana, naye hakukosa kuwagawia pesa.
Saa anapokumbuka kurudi nyumbani pesa zote(noti) mfukoni zimeisha. Siku hiyo ya mshahara baba akifika nyumbani mama alikuwa anafurahi kwakuwa alijua atapata pesa za kununulia chakula na mahitaji muhimu kwakuwa baba amepokea mshahara. Furaha ya mama ilikuwa inageuka huzuni baba anapomtupia vijisenti vilivyobakia baada ya kutoka kwenye ulevi.
Baba na mama walikuwa wakigombana mara kwa mara kwa sababu ya maisha hayo na yaliendelea kwa miaka mingi hadi baba alipopata dawa iliyomwezesha kuacha ulevi. Baada ya kupata dawa hiyo, akipata mshahara alikuwa anakuja nao wote nyumbani na kupanga matumizi na mama. Maisha yalianza kuwa ya furaha.
Kuna watu wengi wanaishi hivyo. Wanapata pesa lakini hazikai, zinaishia kwenye ulevi huku watoto wao wakilala njaa na kukosa ada ya masomo. Na wengine wamepigwa chupa za bia na kusababishiwa majeraha. Wengine wamekutwa mitaroni kwa sababu ulevi uliwazidia wakajikuta wameanguka na kulala popote pale. Kwa ujumla ulevi umewasababishia watu wengi maisha ya dhiki, huzuni na majuto. Wasioyafurahia maisha hayo wanatafuta sana njia au dawa ya kuacha ulevi lakini hawapati. Baba yangu alipata mashauri mengi na mapendekezo ya dawa za kuacha ulevi.
Alijaribu yote lakini hayakumsaidia, hadi siku moja alipoipata "dawa" ya ajabu. Dawa yenyewe ni rahisii tu na hainunuliwi kwa pesa: Aliyakabidhi maisha yake kwa Yesu. Alitubu na kuamua kuacha kabisa maisha yote ya dhambi kisha akampokea Yesu moyoni mwake kwa imani awe Bwana na Mwokozi wake.
Kuanzia hapo alipata uwezo wa kushinda vishawishi vyote vya ulevi. Marafiki zake walipokuwa hawamuoni vilabuni, walishangaa na kujiuliza ni kweli ameacha ulevi? Siku zilivyoenda, waliamini kuwa ni kweli ameacha. Hiyo ndio dawa, tusitafute dawa nyingine zaidi ya hiyo.