Wanaotafuta dawa ya kuacha ulevi tukutane hapa

Sasa kwa mimi Mkatoliki ambaye nimemkabidhi Yesu maisha yangu na kinywaji naruhusiwa inakuwaje?
 
Ni Amina na Kweli....ongera kwa uzi mzuri
 
Kumbe unahubiri dini na kupalilia imani yako? Yesu angekuwa dawa ya ulevi basi walevi wengi wasingekuwa wakristo. Badala ya kukataza ulevi alibadili maji kuwa divai halafu eti awe jibu! Acheni kutafuta kiki kijinga na kupotosha wengine. Dawa ya ulevi ni kupiga marufuku vilevi simpo.
 
Hii ni vita ya kiuchumi, mnataka TBL ifungwe? Nchi ikose mapato?
Hivi Mungu alipotuambia tusilewe kwa mvinyo kwakuwa ndani ya mvinyo kuna ufisadi alikuwa anataka nini? TBL ifungwe?
 
Yesu angekuwa dawa ya ulevi basi walevi wengi wasingekuwa wakristo.
Mkristo maana yake mfuasi wa Kristo. Anaishi kwa kufuata nyayo za Kristo. We ulisikia wapi Yesu ameanguka mtaroni kwa sababu ya ulevi? Divai aliyotengeneza ilikuwa njema, haikulewesha. Vinginevyo asingesema walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni
 
Unazungumzia nchi gani? Japan? Japan pato la taifa linachangiwa na viwanda gani? Viwanda vya bia vitaendelea tu kuwepo. Point hapa ni jinsi ya kuwasaidia wanaoteseka na unywaji.
Mkuu mbona unachanganya ma file,iko tofauti kati ya unywaji na ulevi.
 
Umemaliza vizuri.

Nilishaanza kuhisi unataka kutupiga hela.
 
Hivi Mungu alipotuambia tusilewe kwa mvinyo kwakuwa ndani ya mvinyo kuna ufisadi alikuwa anataka nini? TBL ifungwe?
Mbona sasa mnatuchanganya watu wa Mungu, imeandikwa pia ....usimpe mfalme kilevi kwa maana atasahau majukumu yake, bali mpe mwenye shida anywe asahau shida zake

Sa itakuaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…