Ndio, kwa ajili ya uzima wa milele. Si unajua duniani sisi ni wapitaji?Sasa mimi sijui utanisaidiaje, nakula mtungi tangu 1988 nikiwa shule ya msingi (ilikuwa inapikwa nyumbani) mpaka sasa. Lakini nimejenga na watoto nawalipia ada vizuri kabisa. Familia iko na furaha kabisa, tena nikinywa huwa napenda kuwapa surprise ya vijizawadi. Kwa hiyo niache pombe?
Tunaposoma Biblia tunatakiwa tuisome huku tukijiuliza ni nani aliyesema hicho kifungu au mstari tunaousoma? Je ni Mungu mwenyewe au ni Mtumishi wake? Ni muhimu kujiuliza hivyo kwa kuwa Biblia ina maneno yaliyosemwa pia na shetani, mapepo, makahaba nk. Huo mstari ulioutaja upo katika Mithali 31:6-7. Ukianzia kusoma mstari wa 1 ndio utajua ni nani aliyeyasema hayo maneno. Ni maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. Je sasa tufuate ushauri wa mama mzazi wa Mfalme Lemueli au tufuate maagizo ya Yesu, Mfalme wa wafalme yanayotukataza kunywa kileo?Mbona sasa mnatuchanganya watu wa Mungu, imeandikwa pia ....usimpe mfalme kilevi kwa maana atasahau majukumu yake, bali mpe mwenye shida anywe asahau shida zake
Sa itakuaje...
Divai aliyotengeneza Yesu kwa muujiza ilikuwa divai njema. Yesu hakuongeza kilevi(alcohol). Watengenezaji wa divai siku hizi wanaongeza hiyo alcohol. Kwani wewe ukikamua zabibu ukanywa juisi yake utalewa?Divai haina kilevi? Kwanini asingebadili maji kuwa juice ya matunda moja nzito tamu yeye akabadili kuwa divai
Ukiugua tumbo na magonjwa mengine ya mara kwa mara ukaenda kwa daktari akakuambia tumia mvinyo tu kidogo utapona, utamwelewa? Kusoma mstari wa Biblia na kujua maana yake ni vitu viwili tofauti1Timotheo5:23″ TOKEA SASA USINYWE MAJI TU LAKINI TUMIA MVINYO KIDOGO,KWA AJILI YA TUMBO LAKO,NA MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.
Ni mstari gani wa Bibilia mnaosomewa na Paroko/Padri kuwa mnaruhusiwa kinywaji?Sasa kwa mimi Mkatoliki ambaye nimemkabidhi Yesu maisha yangu na kinywaji naruhusiwa inakuwaje?
Huwa sijibu maswali ya hivyo Mimi!Ni mstari gani wa Bibilia mnaosomewa na Paroko/Padri kuwa mnaruhusiwa kinywaji?
Yaani ni ujinga mtupuInakera unasoma uzi mrefu kama huu halafu unakutana na hitimisho la kijinga.
Daktari awe mganga was kienyeji au huyu was elimu ya kizungu akinipa huo ushauri nitamuelewa ni Taaluma yake Mimi ni Nani nimpinge.Ukiugua tumbo na magonjwa mengine ya mara kwa mara ukaenda kwa daktari akakuambia tumia mvinyo tu kidogo utapona, utamwelewa? Kusoma mstari wa Biblia na kujua maana yake ni vitu viwili tofauti
Baba yako asisingizie Pombe,hakuwa responsible tu.Baba yangu alikuwa anakunywa pombe kiasi kwamba akirudi anapaki gari na hawezi kushuka kutembea kuingia ndani.Kaka zangu walikuwa na kazi ya kumbeba kila siku kuingia ndani.Hajawahi kutulaza njaa wala kuacha kulipa ada kwa kuwa alikuwa anajielewa.Msipende kusingizia pombe kumbe uzembe wenu tu.Hilo hitimisho ndilo lililomsaidia baba. Na kwa msaada huo alioupata na mimi mtoto wake nikaweza kupata hata ada za masomo
Baba yako asisingizie Pombe,hakuwa responsible tu.Baba yangu alikuwa anakunywa pombe kiasi kwamba akirudi anapaki gari na hawezi kushuka kutembea kuingia ndani.Kaka zangu walikuwa na kazi ya kumbeba kila siku kuingia ndani.Hajawahi kutulaza njaa wala kuacha kulipa ada kwa kuwa alikuwa anajielewa.Msipende kusingizia pombe kumbe uzembe wenu tu.