Story ina walakini kidogo,
Kwa kifupi Sakara alienda nchini Bulgaria kwenye miaka ya 1980 kusomea uhandisi, lakini hali ilimuendea vibaya mpaka kujikuta hana uwezo kabisa wa fedha na akiishi kwa shida mitaani. Angependa kurudi Tanzania lakini hana uwezo wa kujilipia nauli. Inasemekana baada ya kutangazwa amekufa, ndugu zake hawakuendelea kumtafuta, lakini ukweli ni kuwa yuko hai. Taarifa zake nyingine ni:
Amezaliwa mwaka 1961
Inakisiwa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1982 - 1984 halafu akaenda Bulgaria ambako alikuwepo mpaka kipindi napata taarifa hizi.
Mara kaenda Bulgaria miaka ya 1980, halafu tena kasoma UD 1982 - 1984.
Na pia miaka ya 1980s jamaa alikuwa na miaka mdogo sana, ina maana tayari alikuwa kaanza chuo kikuu mlimani?? au mie ndio sijalelewa mtiririko wa hii story??