Wanaotajwa kurithi mikoba ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa Raymond Mangwala

Wanaotajwa kurithi mikoba ya Katibu Mkuu UVCCM Taifa Raymond Mangwala

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
1,932
Reaction score
4,403
WANAOTAJWA KURITHI MIKOBA YA Katibu Mkuu UVCCM TAIFA (SG) Raymond Mangwala

Baada ya uteuzi wa viongozi wakuu wa UVCCM - Taifa kupewa UDC. Chombo hicho kimebaki bila uongozi wa juu. Ukiachilia suala la Mwenyekiti wake Kheri James ambaye alichaguliwa kwa kura kupitia Mkutano mkuu, UVCCM kwa sasa inabaki bila Katibu Mkuu na ambaye aliyekuwepo kateuliwa kuwa DC Ngorongoro. Na Naibu katibu Mkuu Bara ambaye awali mabadiliko yalifanyika na nafasi hiyo kubaki wazi. Naibu Zanzibar kwa namna moja au nyingine ndio atakaimu mpaka safu mpya ya uongozi itakapopatikana.

Huku vikao vya chama vikitarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii. Majina kadhaa yamesikika yakitajwa kurithi mikoba ya SG Mangwala.

1. Hassan Abduli Nyange - DAS wilaya ya Pangani anasemaa kua miongoni mwa vijana wanaokipenda na kukipigania chama

2. Christopher Ngubi agai - Mpaka juzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa huyu kabla ya kuwa DC alikuwa katibu mkuu wa shirikisho la vyuo vikuu CCM Taifa na ndio akiyepigania kuundwa kwa chombo hicho cha wanafunzi

3. Mussa Haji Mussa - Naibu Katibu Mkuu UVCCM Taifa - Zanzibar anazungumzwa sana kurithi mikoba ya Mangwala kwa kua ndio Naibu pekee aliyebaki na kwakua alikuwa mjumbe wa baraza kinachombeba kwa sasa ni uzanzibar wake

4. Hassan Bomboko - Aliyekuwa Mkuu wa idara - Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa .... Ni moja wa vijana waliokulia ndani ya Jumuiya kuanzia ngazi ya chipukizi. Amekuwa mjengaji hoja mzuri, hodari wa falsafa na itikadi za Chama!. Ni katika kipindi chake UVCCM aliibua dhana ya "UVCCM ya Kijani" na hamasa ya kupandisha bendera mitaani "Operesheni Bendera" dhana ambazo baadaye zilichukuliwa na chama na kuwa kampeni za kitaifa

5. Mohamed Aliani Abdallah - Aliyekuwa Mkuu wa idara - Maadili UVCCM Taifa huyu ni miongoni mwa vijana waliokulia katika nafasi mbalimbali chamani na alikuwa Mkuu wa idara ya Organization na baade Mkuu wa Maadili UVCCM Taifa kwa sasa yuko chama kama Katibu Msaidizi Mkuu

6. Suleiman Mwenda - Mtumishi CCM na miongoni mwa vijana wenye uzoefu mkubwa amekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM taifa Mzee Jakaya Kikwete amekuwa msaidizi wa Mzee Mangula na sasa yuko ofisi ya mwenezi wa ccm Taifa kama Katibu Msaidizi Mkuu, anapigiwa chapuo na kundi la watu wa Jakaya

7. Peter Kasera - Aliyekuwa Mkuu wa idara - Organization, na Uhusiano wa Kimataifa UVCCM Taifa ... Ni kijana mtulivu, makini na msikivu!. Ni kipindi cha miaka miwili alipokuwa Mkuu wa idara alifanikiwa kuendesha mafunzo kwa watumshi wote wa Makao Makuu, semina kwa makatibu wote wa Mikoa, semina kwa Hamasa wote wa mikoa, na kuandaa makongamano kadhaa ya taasisi za umma na taasisi za AZAKI.

7. Nelson Lusekelo - Mkuu wa idara Uchumi na Fedha UVCCM Taifa huyu ni miongoni mwa vijana ambao waliaminiwa sana na mfumo uliopita inasemekana ni kijana mtiifu sana wa aliyekuwa katibu mkuu Dr. Bashiru Ali kakurwa hata idara zilipovunjwa Bashiru alimbakisha ili aendelee kuwa sehemu ya wajumbe wa secretariety ya vijana Taifa
 
1624275446773.png
 
Hapo ni bora comrade Hassan Bomboko anafaa sana kuiongoza jumuiya ya umoja wa vijana.
 
Ccm lolote laweza kutokea, si ajabu wakamchukua muunga juhudi
 
Back
Top Bottom