Nimesikitika na ninaendelea kusikitika sana hasa ninapowaona watanzania wenzangu wakitaka kuiangamiza nchi yao wenyewe, kwa sababu tu ya ubinafsi,uchoyo na urafi.
ARE WE REAL TANZANIANS?
- Haiingii akilini mwangu kuona mtanzania unakataa elimu ya bure!!
- Haiingii akilini kuona mtanzania huna uchungu na fedha (BILLIONS) zilizoibwa na watuhumiwa wa ufisadi
- Haingii akilini kuona watu wanamshangilia kikwete hata baada ya kusema uongo(anapowasifu mafisadi, anapokataa elimu ya bure)
- Haingii akilini Kikwete anasema nisingeenda ulaya watanzania mngelala njaa!! watanzania wanashangilia(kama utakumbuka kuna watafiti walifanya utafiti wao katika bonde la mto rufiji wakapeleka utafiti wao serikalini, wakasema bonde hilo likitumiwa vizuri katika kilimo cha umwagiliaji tanzania haitakuja kuwa na shida ya chakula, itaweza kuzalisha chakula ndani na kingine kuuza nje ya nchi. Nakumbuka kabisa serikali ya CCM ikakataa, kwa sababu kulikuwa kuna vigogo wa CCM wanapata faida kubwa kwa kuagiza chakula nje na baadhi yao leo hii tunawashangilia)
ARE WE REAL TANZANIANS?