Elections 2010 Wanaotaka Kikwete arudi madarakani si wenzetu

Elections 2010 Wanaotaka Kikwete arudi madarakani si wenzetu

kwa hiyo ulipomchagua kikwete mwaka 2005 ulikuwa mjinga sio? Sasa nani kakutoa huo ujinga wako?
Watu wengine kwa nyepenyepesi tu!!!!
Nani alikuambia nilimchagua kikwete. Mimi ni mtanzania halisi ninajua haki yangu, sidanganyiki na mashati ya CCM kama wewe
 
ushawahi kutembea angalau nchi moja wewe kabla ya kukurupka? nitajie nchi moja tu dunani iliopo salama kama unavyotaka wewe


Nikutajie nchi kivipi,hapa nilipo nipo wapi? kwa taarifa yako nimeishi ulaya zaidi ya miaka kumi na bado nipo.
 
Thread hii ni ya kijinga sana, unaposema si wenzentu unamaanisha nini? nyinyi ni akina nani? na kwanini unataka watu wote wawe nyie.
pili unapowashangaa watanzania kukataa elimu bure nakushangaa mwenyewe. Hivi ni nani alyefuta ada za mitihani mashuleni? hivi ada ya 20,000/= sio elimu bure? kujenga shule kila kata na kurahisisha watoto kutogharimia safari za mbali na kuepuka usumbufu sio elimu ya bure? tumieni akili mnabojenga hoja zenu.

kuhusu pesa zilizoibwa, huoni hata aibu? hivi ni Rais gani aliyethubutu kuwapeleka viongozi waandamizi kwenye vyombo vya sheria tangu tupate uhuru kama si JK. ningetegemea mmumiminie sifa za kuchukua maamuzi mazito lakini ndio mnalaumi. msiwe na porojo zisizo na maana na ushabiki wa kibubusa.

Binadamu kiumbe wa ajabu sana, Nyerere mlisema ametudumbukiza kwenye umasikini wa kutupwa (kutokana na ujamaa wake) lakini baada ya kuondoka tukamwita baba wa Taifa. Mwinyi mlimtukana hadi mkamaliza msamiati wa matusi lakini alipoondoka mkasema mzee wa busara (mzee wa ruksa). Mkapa mkamwita baba wa kuvunja mikataba, leo wengine wanasema ni baora ya mkapa. Leo hii JK ambaye mlimwita chaguo la mungu, ameonekana hafai, tusubiri akimaliza muda wake tuanze kumlilia. hii ndio hulka ya binadamu.

Mkuu naona unazungumza kama mtu aliyeshiba vile..!!!! Unasema karo ya shs 20,000 kwako ni kama kutoa elimu bure? Nadhani hujui hali halisi ya watanzania wengi huko vijijini na mijini. Na hilo ndio tatizo la watu wengi wakiwemo viongozi wetu, hawajui matatizo ya wananchi wao ama hawataki kujua kwasababu wao wanakula na kusaza.

Kwa taarifa yako hiyo pesa ni kubwa na wazazi wengi hawawezi kuimudu. Imagine mzazi akiwa na watoto wawili au watatu tayari mzigo unashindikana kubeba. Hii ndio hali ilivyo kwa wazazi huko kijijini kwetu, na hata huko mujini kwenu hali hii ipo.

Lakini pia naomba tuangalie hiyo elimu inayotolewa kwa ghalama ya sh 20,000; je, mazingira ya shule yakoje? Je kuna maktaba (library) iliyo na vitabu vikitosheleza mahitaji ya elimu? Je inao walimu wenye uwezo wa kitaaluma ili kutoa elimu ubora? Je yapo mabweni ya kutosha kulala wanafunzi wote au wanafunzi wanalazimika kutafuta vyumba vya kupanga huko uraiani? Na hiyo inakuwa chanzo cha baadhi ya wanafunzi kupata mimba na ukimwi katika mazingira hayo magumu ya kuishi. Na bahati mbaya viongozi wetu wameona sababu za matokeo hayo kuwa ni kiherehere cha watoto wa kike! Inasikitisha unapokuta rais ndiye anatamka hivyo!

Mimi nina mifano mingi, ya shule hizo za kata, ili kuthibitisha kuwa shule hizo haziwezi kuleta mapinduzi ya elimu katika taifa hili. Elimu imtaendelea kudidimia zaidi kama hakuna hatua zinachukuliwa ama kubadili uongozi ama kubadili sera za elimu.

Tanzania sasa hivi imekuwa nchi nzuri sana na kimbilio la wageni kuja kunufaika. Umasikini wa wananchi na udhaifu wa viongozi na sera zetu unatowa hiyo fursa. Kwa makisio yangu, baada ya takribani miaka 15 ijayo nguvu ya uchumi, sehemu kubwa ya ardhi, maliasili na uongozi wetu, utakuwa mikononi mwa wageni. Na sisi tutakuwa kama red indians kule America, tutakuwa marginallized katika kila kitu. Mfano hai ni huu: Mwaka 2006/7 serikali ilipima viwanja 20,000 sehemu fulani. Serikali ilipoanza kuuza viwanja hivyo, wengi wa waliomudu kununua viwanja hivyo walikuwa wahindi, wasomali na waarabu! Na baadhi ya waswahili waliokuwepo pale walikuwa wametumwa kununulia maboss wao ili kuepuka kupanga misululu au kushtukiwa. Sasa hivi ukienda sehemu hiyo utakuta zaidi ya 80% ya wakazi ni wageni!!! Je ni kweli kwamba wa-Tz wazawa hawapendi kununua viwanja ili waweze kujenga nyumba za kuishi? Kwanini hawakuja kununua ili na wao wapate kujenga nyumba zao? Jibu ni umasikini wa kutupa. Wa-Tz wazawa hawana uwezo wa kununua ardhi, ila kuiuza. Kama ambavyo hawana uwezo wa kununua elimu ya shs 20,000. Wanahitaji kuwezeshwa kwa kupewa uwezo na elimu ya bure.

CCM haioni tatizo hilo. Umasikini wetu ni furaha kwa watawala wetu ili wapate unafuu wa kugawa khanga, t-shirt na kofia na kununua shahada kwa sh 10,000. Makamba anafurahia wa-TZ masikini wa namna hiyo ili waendelee kumwabudu yeye kama mungu mdogo. Kikwete hilo pia halimsumbui hata kupata shida ya kujua sababu ya umasikini huo hataki. Anaridhika kwa vile yeye ni raisi na anakula na kunywa na kumwandaa mwanaye kurithi uongozi wa nchi baada yake. Viongozi wetu ni wamekuwa vipofu na chama chetu kimepoteza dira. Kwasasa yafaa wakiondoka ama kuondolewa mwaka huu ili wakae pembeni.

Umesema pia kuwa rais Kikwete amewafikisha mahakamani wezi wa pesa zetu na hivyo kumfanya kuwa rais wa pekee hapa nchini kuliko watangulizi wake. Sijui kama hilo ni kweli. Lakini kinachoshangaza ni kwamba wengi wa watuhumiwa wa wizi huo na waliofikishwa mahakamani ni maadui za Kikwete na si zaidi ya hapo! (fanya research ndogo na utaweza kufikia hiyo conclusion). Hata hivyo wakati kesi ikingali bado ipo mahakamani wote tumesikia washitakiwa wa wizi huo wakisafishwa na rais kwenye majukwa, akidai wanaonewa tu hawana hatia. Hili si jambo lakujivunia katika nchi inayodai kuongozwa kwa utawala wa sheria. Tz hakuna utawala wa sheria. Kikwete si kiongozi bora na shupavu. Kikwete hana hata ile hekima ndogo tu ya kulinganisha na kiongozi wa nchi ndogo kama Rwanda. Hafai na anapwaya kama suruali ya baba ukiwa na umri wa miaka 12. Kama wewe unamwona anafaa basi kuna sababu yake ...

Pia umesema watu haweshi kulalamika tangu wakati wa Nyerere. Ukweli ni kuwa ukuu ni jalala. Wananchi lazima watalalamika hata kiongozi akiwa Obama ama Mfalme Suleiman wa zamani. Tofauti ni kuwa, kiwango cha malalamiko dhidi ya Kikwete na CCM yamevuka mipaka, ni makubwa kupindukia. Na watu wameumizwa sana ki-psychologia na kiuchumi. Makosa ya uongozi yamekuwa mengi mno, ukiyajumlisha yote tangu namna alivyoingia madarakani, alivyochagua wasaidizi kutoka mtandao na maswahiba. Aliwaacha viongozi wazuri mfano Mzee Mangula na kumleta Mzee Makamba !! Makamba ameharibu chama. Makamba ni mhuni na hana hana busara. Mimi ni mwana CCM na hilo nilisema mapema sana alipochaguliwa. Mengine tunahifadhi moyoni, Makamba hafai hata kuwa mkuu wa Wilaya acha Mkoa. Makamba ni mzee wangu na ni mtu wa nyumbani kwetu hivyo sina chuki dhidi yake kwa namna nyingine zaidi ya ubovu wake katika uongozi. Matokeo ya chama kuyumba ni serikali legevu ambayo imeshindwa kusimamia uchumi, uchumi umeporomoka na maisha ya watu kuathirika. Nenda vijijini ukajionee mwenyewe watu wanavyoteseka ... kama una moyo wa kuhurumia watu hutaweza kuandika tena hayo uliyoandika.

Huwa sipendi sana kuandika, lakini bandiko lako limenisukuma kuandika hayo niliyoandika. Ninaweza kutoa taarifa nyingi zaidi na za ndani lakini nachelea kuitwa mchochezi. Naomba kuishia hapo kwa leo na kuwasihi wa-Tanzania tuwe wakweli katika mitizamo kuhusu nchi yetu. Ushabiki utaangamiza nchi yetu nzuri tuliyopewa na Muumba kupitia waanzilishi wa taifa letu.
 
wavivu wakufikili mpo wengi sana si wewe peke yako congratulation mkuu!

Muzee na wewe mwenyewe ni mvivu wa kutosha kwa maana hata kapitoletaz na vituo vidogo vina. :hand:
 
Back
Top Bottom