Wanaotaka kuandamana kesho HESLB soma hapa

Wanaotaka kuandamana kesho HESLB soma hapa

Katibu Afya

Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
56
Reaction score
20
Habari Za majukumu wasomi wenzanu.

Nimeona C vibaya nikitumia fursa hii kuwapa muhtasari wa majibu tuliyopewa jana tarehe 13 October mimi na wahanga wenzangu wa NOT SECURED tulipokwenda HESLB ili tuwe na picha halisi ya jinsi hali ilivyo kwa kuwa naamini wengi miongoni mwa watakaoshiriki kesho kwenda kudai haki yao, jana hatukuwa nao pale BODI.Waswahili wanasema ukitaka kumshinda adui yako lazima umjue jinsi alivyo.

Moja kwa moja nawaunga mkono waandamanaji ili mradi tu maandamano yawe ya amani kama ambavyo tulifanya cc jana na muda c mrefu tukiwa pale pale BODI status za baadhi ya wahanga zikaanza kubaddilika kutoka NOT SECURED na kujikuta wamepata mkopo.

Bila shaka hawa jamaa walifanya hivi kwa wakati ule ili watuy wapunguze jazba na kuona pengine mambo yangekaa sawa kwa sababu wakati ule tunamgonga maswali yaliyoshiba shibe ya kupindukia yule Mkurugenzi wa Bodi, watu wao wa IT walikuwa mitamboni wakiendelea na yao.ENEO tulilokaribishwa lilikuwa ni nje kwa sababu ndani pasingetosha kutokana na idadi kubwa ya watoto wa masikini na yatima wanaojitambua kufurika pale kudai haki yao.

Miongoni mwa mwswali yalikuwa kama ifuatavyo.

1: Nini maana nzuri ya neno NOT SECURED.
Jamaa alijibu ni hali ya kutofanikiwa kupata kitu fulani,pale pale akatwangwa swali jingine lililozaliwa kutoka katika jibu la swali la kwanza bila yeye kujua kwa nini aliulizwa swali rahisi kiasi kile.

2: Kutofanikiwa kupata kitu fulani ni lazima kuwe na sababu za msingi, Tuliokosa mkopo tumeandikiwa NOT SECURED lakini hatujui kwa nini? Jamaa akamtuma msaidizi wake akawaambie watu wa IT waandike sababu ya kila mtu mmoja iliyomfanya akose mkopo.Kwa kuwa hao wataalam wa IT walikuwa mitamboni muda ule, ndo hapo status za watu wengine zikaanza kubadilika na kujiona wamepata mkopo wakati awali haikuwa hivyo na ndipo mwanzo wa kutokea kwa maelezo fulani chini ya NOT SECURED yakionesha sababu za kutopata.

Nilipatwa na Mgagasuko moyoni baada ya kaka angu ambaye tunafanana sifa,Tunalingana umri,Jinsia,aina ya elimu kwa kuwa cc tumezaliwa Pacha,tayari tumemzika Baba mwaka 2008 na tumeambatanisha kila aina ya ushahidi ktk nyaraka za maombi ya mkopo huo na tumechaguliwa kozi moja katika chuo kimoja.Kozi tuliyochaguliwa ni Priority According to TCU Admission Book lakini yeye kapewa mimi cjapewa halafu bado naambiwa sababu ya kutopata eti cjakidhi vigezo, swali lifuatalo nikamdondoshea yule bwana.

3: Ni vigezo gani vilivyofanya kaka angu akapata wakati huo huo mimi nikose wakati mimi na broo ni kama mwenyezi Mungu ali kopi na kupesti wakati wa kutuumba kuanzia mwonekano,tabia mpaka shida za kimaisha (ufukara )

Yule bwana akabadilisha na kusema kwamba...Kuna watu 9000 ambao wana vigezo vya kupata lakini wamekosa kutokana na bajetu kufika kikomo.Nikamtwanga swali jingine

4: Inakuwaje mnaona wazi kwamba pesa iliyopo ni ndogo tofauti na idadi ya watu wanaohitaji halafu hapo hapo wengine wanapewa 100% wakati wengine hamuwapi hata 0% kweli hii ni haki?

5: Kwa nini msingewagawanisha hao wenye uhitaji angalau nusu nusu ili kila mmoja zimsitiri jamani??? Watanzania wenzetu mnatunyanyasa.....Pesa kibao mmepeleka JKT kuchezea wakati maswala ya muhimu kama haya mnashindwa kutekeleza!!!!!! kwa nini mnaanzisha program zisizo na msingi wakati za msingi zinawashinda?

Hii ni aibu kubwa kwa Taifa la Tanzania hivi hamjui kama cc ndo viongozi wa baadaye?? kwa haya mnayotutendea mnapandikiza nini vichwani mwetu?

Nilisogea pembeni na kuwaachia wengine nafsi waendelee ktoa maduku duku yao kwa sababu tayari chozi lilishaanza kunidondoka kwa uchungu xo nlishindwa kuendelea.

Inaonekana maneno yalimwingia jamaa ipasavyo naye kutambua madudu waliyoyafanya hasa kwa kushindwa kugawanya kiasi kidogo cha pesa ili kuwafikia walengwa wote wenye uhitaji wa namna moja.Kutokana na hilo jana niligundua kwamba TANZANIA ina uhaba mkubwa wa watendaji wanaojiongeza kwa kutumia akili zao binafsi,hawa jamaa wanaishi kwa ku kariri jambo ambalo ni hatari sana kwa nchi yetu kwani Mijitu dizaini hii hata makadirio ya bajeti za familia zao huwa zinawashinda na laiti kama hawa jamaa wanafanya kazi ktk falme za kiarabu wangekuwa wameshachinjwa zamani sana.Kwa upole alihitimisha hivi

" Tatizo kubwa ni kwamba Serikali imetoa pesa kidogo sana, pesa yote iliyotolewa ndo hiyo ambayo imegawanywa kwa watu na hakuna hata senti iliyobaki labda kama serikali itaongeza pesa nyingine.

Kwa kuwa mi siishi Dar na tayari nilishakata tiketi kurudi mkoani, Saa nne ile ile niliondoka zangu kuelekea Ubungo tayari kwa safari huku nikiwaacha wenzangu wakielekea zilipo ofisi za TAMISEMI ambapo waliambiwa haya yafuatayo;

"Suala lenu tayari linajulikana na sasa hivi tuna kikao juu ya suala hili tukiiomba serikali yetu tukufu kufanya mchakato wa mkopo kwa vinaja hawa ambao wamekosa hivyo bas kwa kuwa kesho ni ckukuu, nendeni mje tena Jumatano"

Naomba nieleweke, Maneno haya yalizungumzwa TAMISEMI wakati tayari mi nimeshaondoka,Niliambiwa na mmoja wa wenzangu tuliokuwa naye HESLB ambaye yeye alifika hadi katika ofisi hizo.

KWA WALIOPATA MKOPO;

Furaha uliyonayo sasa hivi, kinyume chake ni uchungu na maumivu aliyonayo mwenzako aliyekosa,haina tofauti na kufeli mtihani, nadhani kwa waliowahi kufeli wakati walisoma kwa bidii na kutarajia kufaulu, wanafahamu nini namaanisha.Furaha yako isikupelekee ukamkashifu yule aliyekosa hicho ulichonacho wewe. Nawatakia maisha mema ya chuo na muitumie fursa hiyo mliyoipata kufikia malengo.Katika kila herufi moja unayoisoma ukiwa chuo kumbuka kuna wenzako kibao wapo mtaani kwa kushindwa kuendelea na masomo kutokana na H E S L B kufuta ndoto zao.

Kwa yule mwenye uwezo wa kujisomesha pia usije ukamwona mwenzako anayeshindwa kujisomesha kwa kukosa mkopo ni mzembe........jamani cc ni Fukara lakini ufukara unatofautiana kama unabisha Nenda kesho kaone watoto wa Fukara wanavyolilia haki yao na vielelezo vyote ambavyo wakati mwingine unaweza ukajiona wewe una nafuu.

Nawatakia kila la kheri
 
Duuuh! ! Na mimi kidogo nidondoshe chozi
Kibishi bishi hivyo nitasoma kwa mshahara wa wazazi na kujibana
 
Poleni sana Jamanii, kidogo tu nidondoshe chozi hapa,Mungu awasaidie
 
dah hadi chozi limenitoka poleni sana mkuu MUNGU awasimamie..yani dogo langu alikuwa muhanga wa not selected due to compttn then akaaply bsc in chem unvst f bgmy ili aje afanye transfer,mambo sio mambo dogo kafanya transfer aende bugando coz sifa anazo tatzo lnakuja mkopo wake ushapelekwa bagamoyo hv kunakupona kwel hapa au ndo ajpange tena kwa ajl ya mwakani???..lengo lake awe mfamasia sas hz tcu&heslb ndo vkwaz0
 
Mkuu kwanza pole kwana kwa kukosa mkopo pili hongera kwa mlichokifanya jana hata kama hukupata ila kuna mamia ya vijana wamepata mkopo jana hiyo hiyo wengine hata hawakuwepo kabisa
 
Aisee, pole sana kaka kwa wakat mgumu unaowakabili, content yako inadhihirisha waz jins ulivyo na uchungu! Polen sana but amin m/mungu atawajalia moyo wa matumaini!
 
Dah! Yani pesa za kusomesha wanafunzi elimu ya juu hawana,pesa za kuwalipa wabunge 300,000 kwa kikao kimoja wanazo.


Pesa za kupeleka Kila form 6 kwa mujibu wa sheria wanazo
Hii nchi hii aisee
 
Mm.baba angu analipwa pensheni elfu 28 baada ya miez mieil sijui itakuaje
 
Nina machungu sana, mnanikumbusha maumivu niliyoyapata alafu utashangaa mijitu hapa inaweka comments za dharau na alaaniwe afanyaye hayo
 
daaah inaumiza saana, nimesomeshwa na gvt tangu o.level hadi A.level, coz wazazi wangu walifariki nikiwa std 6, niliscore vzr sana div one olever na div one 6, nituma maombi bodi na tcu education, but mkopo nil, nikakorespond mwaka, kutokana na stress kubwa niliyoipata nilisumbuliwa na ugonjwa fulani uliodumu kwa miaka 2, nimeomba tena mwaka huu education, mkopo not secured reason, eti nimekaa mda mrefu nyumbani, kuna watu wamemaliza 2004 mkopo wamepata sembuse mm, mpaka sasa nalelewa na kaka yangu ambaye kiufupi ana maisha ya ufukara, cjui hata nifanyaje, ndoto zangu zinayeyushwa na serikali yangu it was better to leave the school since ma parents passed away than to study hard with hopeless future lyf, i ril hurted, and regret to be born in tanzania, my b i was in kenya or uganda i could fulfil my dreams,
 
watoto wao wanaenda kuwasomesha ulaya! sisi tunakosa haki elimu! tunakosa maisha na maisha bora hayawezi kuja bila kupata elimu! na elimu ni ufunguo wa maisha! na ufunguo huo tayari ni wa kibaguzi na wakupeana.mmmh masikini mie ngoja nikachome misitu nipate mkaa wakuuza maliasili waje kunifunga! ngoja nikauze nguo za kutembeza askari wa city waje kunipiga! ngoja niwe mwizi segerea inanukia kwangu! wakati elimu niliihitaji nipate maarifa na ujuzi wa kujitegemea kama sijapata ajira niweze kujiajiri!
 
daaah inaumiza saana, nimesomeshwa na gvt tangu o.level hadi A.level, coz wazazi wangu walifariki nikiwa std 6, niliscore vzr sana div one olever na div one 6, nituma maombi bodi na tcu education, but mkopo nil, nikakorespond mwaka, kutokana na stress kubwa niliyoipata nilisumbuliwa na ugonjwa fulani uliodumu kwa miaka 2, nimeomba tena mwaka huu education, mkopo not secured reason, eti nimekaa mda mrefu nyumbani, kuna watu wamemaliza 2004 mkopo wamepata sembuse mm, mpaka sasa nalelewa na kaka yangu ambaye kiufupi ana maisha ya ufukara, cjui hata nifanyaje, ndoto zangu zinayeyushwa na serikali yangu it was better to leave the school since ma parents passed away than to study hard with hopeless future lyf, i ril hurted, and regret to be born in tanzania, my b i was in kenya or uganda i could fulfil my dreams,



Aiseee wewe andamana kabisa hadi Ofisi za Heslb sio fair kabisa onesha na vidhibiti kabisa kuwa hii ni mara ya pili kuomba mkopo
 
Poleni sana ndungu zangu mliokosa mkopo,hakika inauma nina mdogo wangu si wa kuzaliwa nimekutana naye chuo aliugua siku tatu kwa kukosa mkopo.Yote ni kwasababu ya maisha ya nyumbani kwao.Anawaza ni vipi atasoma.Jamani serikali mnatengeneza nini?je taifa la kesho liongozwe na nani?je nchi iongozwe na matajiri na watoto wao tu?Angalieni chozi la mnyonge maana ni laana kwa taifa.
 
Back
Top Bottom