Elections 2010 Wanaotaka kuhama waende ikiwezekana tutawasindikiza - Msekwa

Elections 2010 Wanaotaka kuhama waende ikiwezekana tutawasindikiza - Msekwa

Nadhani ni muda muafaka sasa kwa wale wanaodhani kuwa wako tayari kuhama CCm wafanye hivyo..hofu yangu ni kuwa hawatoki kwa dhati ya moyo bali wanahama kwa mashinikizo ya kisiasa na ndio maana wanarudi CCM baadae na kuvuruga upinzani..

hawa siwatofautishi na waroho wa madaraka ambao wao kushindwa ni karaha na wanataka wao washinde tu..haiwezekani!!! lazma nao siku moja moja washindwe na kama wameshindwa kwa mizengwe basi wafanye yanayotakiwa wakate rufaa na kutumia vyombo husika. tatizo ni migongano ya kimaslahi ktk siasa za kisiku hizi za chuki na visa ndio maana wanatosana.

kama mtu wa kuhama basi atakuwa ameshahama na asingesubiri kushindwa ndipo aseme anahama tena baada ya kuzongwa na makundi ya kisiasa. mi nahisi si wote wanaotaka kuhama wanahama kweli bali huenda kuvuruga upinzani.
 
Wapiga kura za maoni changanya na kadi feki hazikuzidi milioni mbili nchi nzima! Wapiga kura wa Tanznia October ni milioni 19, je itakuwaje? Msekwa kweli amelingala hili au kwa vile ni wazee ambao have nothing to lose!?
 
Naamini ipo siku hii jeuri itawaishia tu.Maneno ya Bob Marley lazima yatatimia tu " You can fool some people sometimes, but you cant fool all people all the time". CCM ni mtandao wa kusaidiana kuwaibia wananchi na kulimbikiza mali kwa viongozi wa mtandao huo. Naamini ipo siku tutaweza kupata viongozi ambao wanajali maendeleo ya nchi na kuthamini wananchi wao. Hali ya maisha huku vijijini inatisha, watu wanazidi kuwa masikini zaidi na zaidi. Soko la mazao yetu halieleweki, tumebaki kuwa vibarua tu kwenye mashamba ya hawa wakubwa..naona ukoloni umerudi kwa sura ya viongozi wetu wenyewe. Wanatuona hatuna maana kabisa!
 
Mkuu kauli za viongozi wa chama zinatia aibu. Msekwa ni mtu mzima alitakiwa kuonesha political maturity, kuongea hivyo ni sawa na kutaka malumbano mipasho style, hakuna mtu mwenye busara anayetaka kitu kama hicho. Huwezi kuwasema hivyo watu waliokitumikia chama kwa nidhamu, kushindwa kwao kuhonga isiwe sababu ya kuwadharau na kuwakejeli namna hiyo.
 
Hajateleza ndugu yangu. Hiyo ndiyo sera ya CCM kwa sasa. Mwenyekiti wa Chama hataki kura za wafanyakzi, na sasa Makamu anafukuza wanachama kuwa hawahitajiki. Subiri Katibu Mkuu naye atatoka na la kwake.

Asiyejua ubaya kiuno, hukigeuza mto wa kulalia!

Hawa viongozi wanajua wanavyoongea kweli?
 
Labda Mweshimiwa huyo alifungua mdomo kabla ya kuunganisha ubongo wake kwanza.
 
Msekwa ananikumbusha machungu kwanza nimeshinda wakalikata jina langu halafu ajue kuna watu tumeuza hadi usafiri wetu kugharamia kampeni wengine nyumba, halafu yeye analete za kuleta. Nasikia mgombea mmoja wa Kelya kaishiwa hadi nauli ya kurudi UK kakopa, Msekwa acha hizo bwana, tunamauchunguu.
 
Inasikitisha sana kwa kiongozi wa juu wa chama kutoa kauli za kigarasa kama hizi dhidi ya wanachama wake hasa wakati kama huu....mmh huyu ndiye aliyekuwa spika wetu kwa miaka kadhaaaaa!

mix with yours
 
tatizo la chama changu ni kutoa matamshi ya hasira bila kupima matokeo/athari zake kisiasa.
hebu angalia jinsi mwenyekiti wangu kitaifa alivyotoa matamshi kwa jazba kuhusu wafanyakazi na matokeo yake kisiasa na jinsi wasaidizi wanavyohaha kukanusha kwamba mzee alisusia pilau ya mbayuwayu.

yanayofanana na mbayu...yatatokea tu baada ya matamshi hayo ya 'kufukuza' wanachama kiaina.
 
Pius ni mropokaji kama alivyo Yusuf, mnakumbuka aliwahi kusema kuwa wanaohoji yeye kuwa na hisa vodacom wana wivu wa kike? Kauli hiyo ilimgharimu sana, sasa angoje gharama atakayolipa kwa kauli yake hii ya kifedhuli.
 
Back
Top Bottom