wanaotaka kuja kusoma India


boscomfugale@yahoo.com
 
napenda sana kusoma india ila tatizo nasikia ukija na vyeti vyako vya india ukienda kuomba kazi unaambiwa hatutambui elimu yakooo

Inategemea umesoma chuo gani. Ni kweli kuna vyuo vingine ni ******. Hii ipo duniani kote. Hata Marekani kuna vyuo ambavyo ni below standard.

So cha msingi ni kupata chuo bora. Kama unataka kuja India na una marks nzuri I'L look for you, best universities
 

jamaa yetu mmoja alienda kusoma chuo flan huko india kinaitwa dayanar sagar kiko bangalore,alvorud tz,ilibid aanze kusoma tu diploma pale Cbe,maana alzunguka na vyeti vyake hadi ikawa kero.so ishu ka hzo ndo zinazowatisha watu wengi kuhusu elimu ya india.
 

Ndugu yangu,

Nakushukuru kwa nia yako thabiti ya kuwasaidia waTanzania ambao wamekatishwa tamaa kutokana na matokeo au mfumo dhaifu wa elimu ya juu hapa Tanzania, lakini hapo kwenye nyekundu ni matusi kwetu hayo...ni matusi na nikiwa kama mtaalamu ambaye nimepatia taaluma yangu hapa Tanzania na vile vile nje ya nchi naona umetudhalilisha!

Si kweli maDaktari wanaosomea nje ya nchi wana taaluma na ujuzi zaidi ya wanaosomea hapa Nyumbani Tanzania. Advantage iliyoukuwepo kwa kusoma India (nje ya Tanzania) ni urahisi wa upatikanaji wa vitabu na journals, vitabu/journals an material nyingine online, na state-of-art medico-technology...kwa sasa gap ya vitabu ni ndogo, Tanzania sasa kuna book shops nyingi unazoweza pata vitabu vilivyokuwa recommended duniani kwa masomo mbali mbali ya medicine, tena vitabu maarufu vilivyoandikwa na wahindi vimejaa kila kona Dar na hata mikoani (mfano Moshi)...Tanzania tumeadvance kwa internet network na kupata online materials..hiyo advantage ya kusoma nje kwa ajili ya vitabu/online materials haipo tena, ni more or less the same.

Medico-technology bado kuna gap, na India imeadvance sana kulinganisha na Tanzania...alkini kama unasoma India halafu ubaki India au ukimbilie ughaibuni kwenye hivyo vifaa, then you can make a point. Kama unategemea kurudi Tanzania, bado hatuna hizo sophisticated machines katika hospitali za kawaida utakazopangiwa kufanya kazi (mfano hospitali ya mkoa au wilaya, ambako ndiko waTanzania waliko). Hivyo knowledge ya state-of-art medico-technology haitamsaidia mgonjwa, kwani huwezi mwambia 'mmmmmh siwezi kukutibu kwa sababu sina CT scan au MRI', inabidi utumie clinical skills zako na experience ya kuona wagonjwa wengi wakati unasoma ili uweze tambua tatizo bila sophisticated machines au lab tests...skills ambazo wengi mliosoma nje (including India) hamna, na waliosoma hapa Tanzania hata experienced nurse anaweza kukuambia hiyo ni tatizo fulani!

Jua kuwa at the end of the day inabidi usave maisha ya waTanzania na kuboresha afya zao kwa hali halisi ya Tanzania na vifaa ambavyo tunavyo, na kuwa na knowledge ya vifaa up-to-date lakini havipo kwa ajili hiyo hakumsaidii mgonjwa.

Mimi nimekufanya kazi kama surgeon Muhimbili kwa miaka kadhaa, an nimesupervise Interns na Registral medical officers wengi sana, na tofauti ya kiutendaji na skills za kuhudumia waginjwa clinic na kwenye wards hata theatre ni kubwa sana kati ya maDaktari waliosoma nje (including India, Russia, and China) na waliosoma hapa Tanzania. Tulikuwa tunafanya kazi ya ziada kuwapa clinical skills, uliza waliokutangulia watakuambia...lakini si kwamba maDaktari waliokuwa trained Tanzania ndio wataalamu zaidi, bali ni kuwa wamekuwa na wagonjwa na kupata opportunity za kuona magonjwa mengi na hivyo kusoma kwa vitendo zaidi (tangu mwaka wa 3 wa chuo kikuu), kitu ambacho kinakosekana kwa wenzetu mliosoma nje, na kitu ambacho pia nilikiona nami nilipokuwa nasoma elimu ya juu nje!

Sasa usidharau maDaktari walikuwa trained Tanzania eti kuwa ninyi ni wataalamu na wajuzi zaidi...inapokuja kumhudumia mTanzania katika mazingira ya kiTanzania...huyu Intern aliyekuwa trained Tanzania anakuwa na skills ambazo wewe uliyekuwa trained nje utazifikia baada ya sichini ya miaka mi2 kama ni mjanja na rahisi kujifunza au hata zaidi ya mi3 kama ni mzito wa kujifunza...believe me, I saw it with my own eyes!
 

samahani mkuu, mwaka wa masomo wa pre university (form 5 & 6 ya tz) unaanza lini.
 
Cellozione!

Asante kwa post yako nzuri yenye msaada na upendo kwa Watanzania wenzetu.

Binafsi nimependezwa na uamuzi wako wa kusaidia kile unachokifaham, na hii ndio inaonyesha umuhimu wa JF kwamba watu hujifunza mambo mbalimbali ya kimaisha ili kujikwamua.

Na kushauri usipoteze muda kujibizana na wale wanaofanya utani na kubeza hiki ulichokiweka hapa jamvini, nina imani utawasaidia wengi ambao hawakuwa na uelewa wa hili jambo.

Ulichofanya ni kizuri and keep it up na wala usivunjike moyo kuleta lingine lolote zuri ambalo utalipata toka huko!

Asante Mkuu, JF pamoja!
 


Bonge la mzalendo mdau kwa hilo nakupa big up! Maana wengi tulisoma nje hatukwahi kufanya kama wewe ulivyofanya sijui tulikuwa wabinafsi sana?
Ulipoteleza ni hapo kwenye RED tu,nimeshawahi kutana na wadau madaktari kutoka Russia na China wanalalamika kuwa wanahofu ya utendaji wao wa kazi kutokana na system iliyopo katika nchi hizo ambapo Foreign students hawaruhusiwi kumgusa mgonjwa wanakuwa Observers tu!Sina uhakika nadhani na India ni the same!!Kiutendaji wanaosomea bongo lazima wawe wanauzoefu zaidi kutokana na mazingira kuwa wanayaelewa vizuri zaidi hasa kwa vifaa duni tulivyonavyo na uzoefu wao wakutibu wagonjwa moja kwa moja!!
Otherwise nakupongeza sana kwa kuwa mzalendo ndugu!!

Nawasilisha!!
 
Habari wandugu,

Nafurahi mpaka sasa nimeweza wasaidia wanafunzi watatu. Furaha yangu ni kuona vijana na wadogo zetu wanasonga mbele. Na sio kukaa nyumbani kwa sababu ya kukosa nafasi kwenye shule zetu za hapa kwetu Tanzania.
Muhimu ni kuendeleza career za wadogo zetu.

Kwa sasa niko likizo Tanzania. najua kuna watu watakuwa wameniafuta kwa namba zangu za india.
Kwa wale wanaotaka ushauri, napatikana kwa namba 0687 338128.
 


More than serious kaka. tutakutafuta sana mkuu
 
Huu ndo unaitwa uzalendo kwa kweli.. Big up bro


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Kumtafutia mtu chuo unachaji kiasi gani? Maana kuna jamaa yangu amepata four form six nataka nimlete aje kusoma pre-college kwanza!
 
God Bless U Umekua mzalendo ngoja tutumie hio nafasi vizuri
 

Acha kuongea issue isio kua na tija uyi nduguyi alikua one out of ten na inaelekea alikua kilaza wa kutupwa!!nina ndugu na marafiki kibao wamesoma india wanagombaniwa kwenye makampuni kuajiriwa!wala sio siri ni ukweli ulio wazi kiwango cha elimu india kipo juu!!unaongea pumba sana wkt kwenye ukoo wenu mkipata mgonjwa mahututi mnamkimbiza india!acheni madharau yasokua na msingi!
Watu kibao walipata div one zao wakajiendea india!ni kiwango baba!usipotoshe watu mtu anataka toa msaada we unaanza ponda!tatizo letu watanzania hatupendi maendeleo ya wenzetu!
 
ningependa kujua wakuu kwa anayefahamu, ni nchi gani kati ya india na china yenye vyuo vikuu bora?
 
Awachinji watu weusi siku hizi? Maana tangu auliwe jirani yetu hapa alikuwa anasoma huko nilikosa imani nako kabisa.
 
yes india kuna vyuo mbali mbali na elimu yao iko bora tofauti na nchini kwetu bongo, ningependa nikutafute na mimi nipo gujarat, ahmedabad kwa mambo yangu binafsi sasa sijue wewe upo sehemu gani maana india kubwa sana, ili tuweze kuliongelea kwa undani swala hili
 
Hivi ni lazima uchangie thread hii!!?? ushamba mwingine huu unajichoresha tu hapa jamvini.

Hv kwan uyo lazma achanganyi au o coz anajiona amefka university basi anajiona ameyapatia maisha aache kuuza samaki .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…