Wasaalimu Jamii forum
Mimi ni kijana mwenzenu nasoma india kwa sasa. Ni mwaka wa 4. Nasomea medicine.
Ki ukweli huwa nawasikitikia sana vijana wenzangu, ambao pia naweza waita wadogo zangu. Pale matokeo yanapotoka. Wengi huchanganyikiwa "what next".
Ni wazi idadi ya shule Tanzania ni ndogo sana. Hasa kwa A-level na vyuo vikuu. Hivyo inawalazimu wengi kukatisha ndoto zao na kujikuta wakienda kusoma vitu ambavyo hawajatarajia kama vi-diploma n.k.
Na inasemekana kuwa huwa ni mpango madhubuti kufelisha wanafunzi kutokana na idadi ya shule kuwa ndogo au ufinyu wa fedha za mkopo.
Mimi kama mtanzania na mwenye mapenzi mema na wadogo zangu, nimeona niwaeleze opportunity zilizopo. Usikate tamaa kwa matokeo mabaya au kwa kukosa either shule au chuo. India is a place to study. Si kwamba wanapokea wanafunzi wajinga. La hasha, uku kuna shule nyingi sana. And huwa wanashangaa kwa nini vijana wanatoka Tz na matokeo mabaya wakija uku wanafaulu.
Kwa mfano mimi nilipata div3 ya mwisho, na vyuo bongo walinikataa. But nilipata chuo india na sasa nakaribia kuwa daktari. Na nina uhakika wa kuwa daktari mtaalamu na mjuzi zaidi ya wanaosomea bongo. Nyie wenyewe mnajua India ilivyo kwenye udaktari.
Basi kwa wadogo zangu wanaohitaji kuja india wanipigie kwenye hii namba +91 9731 595412. Kwa wanaotaka kuja kosema degree au pre university. mchipuo au Kozi yoyote ile.
Pre univerity ni kama form 5& 6 ya Tz.
NB: ukinitafuta uwe serious. Usilete utani, sina mda wa utani. Ninachojaribu ni kuwasaidia ili msipoteze malengo yenu
Ndugu yangu,
Nakushukuru kwa nia yako thabiti ya kuwasaidia waTanzania ambao wamekatishwa tamaa kutokana na matokeo au mfumo dhaifu wa elimu ya juu hapa Tanzania, lakini hapo kwenye nyekundu ni matusi kwetu hayo...ni matusi na nikiwa kama mtaalamu ambaye nimepatia taaluma yangu hapa Tanzania na vile vile nje ya nchi naona umetudhalilisha!
Si kweli maDaktari wanaosomea nje ya nchi wana taaluma na ujuzi zaidi ya wanaosomea hapa Nyumbani Tanzania. Advantage iliyoukuwepo kwa kusoma India (nje ya Tanzania) ni urahisi wa upatikanaji wa vitabu na journals, vitabu/journals an material nyingine online, na state-of-art medico-technology...kwa sasa gap ya vitabu ni ndogo, Tanzania sasa kuna book shops nyingi unazoweza pata vitabu vilivyokuwa recommended duniani kwa masomo mbali mbali ya medicine, tena vitabu maarufu vilivyoandikwa na wahindi vimejaa kila kona Dar na hata mikoani (mfano Moshi)...Tanzania tumeadvance kwa internet network na kupata online materials..hiyo advantage ya kusoma nje kwa ajili ya vitabu/online materials haipo tena, ni more or less the same.
Medico-technology bado kuna gap, na India imeadvance sana kulinganisha na Tanzania...alkini kama unasoma India halafu ubaki India au ukimbilie ughaibuni kwenye hivyo vifaa, then you can make a point. Kama unategemea kurudi Tanzania, bado hatuna hizo sophisticated machines katika hospitali za kawaida utakazopangiwa kufanya kazi (mfano hospitali ya mkoa au wilaya, ambako ndiko waTanzania waliko). Hivyo knowledge ya state-of-art medico-technology haitamsaidia mgonjwa, kwani huwezi mwambia 'mmmmmh siwezi kukutibu kwa sababu sina CT scan au MRI', inabidi utumie clinical skills zako na experience ya kuona wagonjwa wengi wakati unasoma ili uweze tambua tatizo bila sophisticated machines au lab tests...skills ambazo wengi mliosoma nje (including India) hamna, na waliosoma hapa Tanzania hata experienced nurse anaweza kukuambia hiyo ni tatizo fulani!
Jua kuwa at the end of the day inabidi usave maisha ya waTanzania na kuboresha afya zao kwa hali halisi ya Tanzania na vifaa ambavyo tunavyo, na kuwa na knowledge ya vifaa up-to-date lakini havipo kwa ajili hiyo hakumsaidii mgonjwa.
Mimi nimekufanya kazi kama surgeon Muhimbili kwa miaka kadhaa, an nimesupervise Interns na Registral medical officers wengi sana, na tofauti ya kiutendaji na skills za kuhudumia waginjwa clinic na kwenye wards hata theatre ni kubwa sana kati ya maDaktari waliosoma nje (including India, Russia, and China) na waliosoma hapa Tanzania. Tulikuwa tunafanya kazi ya ziada kuwapa clinical skills, uliza waliokutangulia watakuambia...lakini si kwamba maDaktari waliokuwa trained Tanzania ndio wataalamu zaidi, bali ni kuwa wamekuwa na wagonjwa na kupata opportunity za kuona magonjwa mengi na hivyo kusoma kwa vitendo zaidi (tangu mwaka wa 3 wa chuo kikuu), kitu ambacho kinakosekana kwa wenzetu mliosoma nje, na kitu ambacho pia nilikiona nami nilipokuwa nasoma elimu ya juu nje!
Sasa usidharau maDaktari walikuwa trained Tanzania eti kuwa ninyi ni wataalamu na wajuzi zaidi...inapokuja kumhudumia mTanzania katika mazingira ya kiTanzania...huyu Intern aliyekuwa trained Tanzania anakuwa na skills ambazo wewe uliyekuwa trained nje utazifikia baada ya sichini ya miaka mi2 kama ni mjanja na rahisi kujifunza au hata zaidi ya mi3 kama ni mzito wa kujifunza...believe me, I saw it with my own eyes!