Mzee kama Katiba ya sasa wameshindwa kuillinda ni kitu gani kitawafanya waitete hiyo nyingine? Kama tunashindwa hata kuwaambia watoke Bungeni sasa tutaweza vipi huko mbeleni? Nyerere aliuliza hoja hii hii kwenye UWHT.
Mwanakijiji ni kweli Nyerere ni baba wa Taifa na alikuwa na hoja nzuri. lakini haina maana kwamba tutafanya kila kitu kwa kum-quote Nyerere hata kwenye mambo ambayo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe. Kuna mambo mengi sana yamebadilika kutokana na wakati. Inaonekana wazanzibar wanataka kujitenga, kuwepo kwenye muungano kwa kuwalazimisha si jambo la busara, na wabara kuwepo kwenye muungano unaotufanya tusikitike kwa kulaumiwa kuwa ni wanyonyaji ni kitu ambacho hakifai. Kwa hiyo solution ni kujadili kwa uwazi benefits na umuhimu wa kila upande kwa muungano, na hoja zote around muungano.
Unatakuwa kujua kuwa mbunge anapoingia bungeni anakuwa na
uwajibikaji wa aina nne. Kwanza ni lazima awajibike
kwa taifa lake, pili ni lazima awajibike
kwa wapiga kura wake, tatu ni lazima awajibike
kwa chama chake, na nne ni lazima awajibike
kwa dhamira na nafsi yake mwenyewe.
Si kweli kuwa kila mbunge anaingia bungeni na kufanya yote aliyosema wakati wa kampeni, kuna mamia ya mambo ambayo hawakusema na wanayafanya kila kukicha, mengine yana maslahi makubwa kwa constituents na kwa taifa. Ukiangalia huku bara hakuna constituents wengi wenye interest ya moja kwa moja ya muungano, hata ukupiga kampeni yenye connection na muungano utaonekana chizi fulani, lakini ukiaa kimya bungeni kuhusu issue ya muungano eti kwa kuwa hukuizungumzia kwenye kampeni yako, ni uchizi zaidi. Kuna mambo mengi tu yana interest kubwa kwa taifa ambayo hayazungumzwi kwenye kampeni lakini yanazunguzwa bungeni.
Vilevile ni kweli wabunge wengi wanashindwa kutetea katiba, hasa wa chama tawala kwa ajili ya maslahi ya Chama (sina haja ya kutoa mifano), lakini hii si excuse ya kuacha kuirekebisha katiba yetu mbovu ya sasa, na si tikiti ya kuwafanya washindwe kuilinda na kuitetea katiba itakayokuja. Hawaitetei na kuilinda kwa kuwa system yetu tayari iko corrupted, katiba mpya inatakiwa kuwafanya wawajibike kuitetea. Moja ya sababu za kutaka katiba mpya ni kuifanya iwe na vipengele vya kuwafanya na kuwapa nguvu ya kuilinda na kuitetea wanaotakiwa kuieteta. Kama sasa hawapo kutokana na system mbovu, haina maana kuwa hawatakuwepo baadaye .
Wasomi na wajuzi wakipewa nafasi mambo Tanzania yatakwenda vizuri, lakini wasomi vihiyo na wanasiasa njaa wakiachiwa kazi hii, tutakuwa tunaenda mrama kila kukicha. Kuna watanzania wengi sana kote bara na visiwani who can wisely and intelligently address and deal with issues regarding union. Tukiacha uvivu na uoga, ana kuonda excuse za kusema issue hii haikuwepo kwenye manifesto ya chama au haikuzungumzwa kwenye kampeni, na tukiwapa nafasi wenye uwezo wa kushughulikia issue hii, it is very simple.
Mwalimu alituingiza mkenge kwa ku-postpone issue hii ndio maana sasa imeibuka tena. So the smart thing for current administration and the coming one, is to deal with the issue head on. Tusiikwepe kwa sababu zisizo na maana. Tukubaliane tu kuwa tujadili issue hii kwa msimamo wa kujenga.