Hii idea kwamba katiba ni msahafu fulani ulioshushwa na mungu kama amri kumi kwa Musa inatoka wapi?
Mzee kama Katiba ya sasa wameshindwa kuillinda ni kitu gani kitawafanya waitete hiyo nyingine? Kama tunashindwa hata kuwaambia watoke Bungeni sasa tutaweza vipi huko mbeleni? Nyerere aliuliza hoja hii hii kwenye UWHT.
As usual hujaongea kitu ndugu yangu.
Muungano umeundwa kwa article of union. Kama haikufuatwa ni kukiuka taratibu lakini haiondoi uhalali.
Mkandara anakuuliza hivi, uliulizwa juu ya mapinduzi? Pemba na Unguja ziliwahi kuulizwa kuwa nchi ya Znbar?
Baraza la mapinduzi halikuridhia!!!!! C'om Mkaimati! kati ya wewe na Karume, Mwinyi ,Kombo, Wakili nani anajua mapinduzi zaidi
Unapokataa kutoa cheti cha ndoa mahakamani, hiyo hafuti uhalali wa ndoa
Sina uhakaika kama unajau unachongelea. Please! please, better you keep quiteAngalai unavyoji contradict, mara Nyerere kaleta mapinduzi mara Wzbar wanatumia fursa, mara Watanganyika wamelala. Do you real know what you want to say or write. Nakushauri ulete hoja zenye mashiko, hadithi na majungu rudisha huko Mzalendo. Please, unazidi kuvuruga mada kwa hoja usizoweza kujibu. Kama mapinduzi yana mkono wa Nyerere, mnampongeza au kumlaumu? Kila mwaka jan 12 mnasherehekea, kwanini msimpongeze Nyerere kuwatoa utumwani. Yaani wewe unayeitaka Zbar huijui Zbar wala historia yake. Unajua unachokitaka lakini? Rudi mzalendo
Tuambie serikali tatu zinaendeshwaje kama wewe na waziri wako Mansoor manavyotaka, na kwanini serikali 3 na si kuvunja kabisa muungano?
Nadhani hutaki kunielewa au unaelewa halafu unazuga.
Unaposema kuwa kama Articles of Union haziondoi uhalali nikuelewe vipi zaidi ya kutumia lugha za kibabe. Si niliulizwa uhalali wa kisheria?
Unapouliza hii ya Mapinduzi na uwepo wa Unguja na Pemba ni upuuzi maana sisi "muungano" wetu ni wa Zanzibar na Tanganyika. Hapa unaonyesha kwamba "kuungana" kwa Tanganyika na Zanzibar ni kwa lazima na sio hiari.
Hao Wakuu uliowataja kuwa wanajua zaidi kuhusu Mapinduzi lakini bado haiondoi kwamba BLM halikuridhia huo "muungano".
Unaesema Nyerere kaleta Mapinduzi ni wewe, mimi nimesema mkono wake umo.
Hii habari ya Mzalendo inakhusu nini? Kwani hii JF wewe ni yako au ni yetu?. Mimi sihusiki na Mzalendo na ni nadra sana hata kufungua huko.
Huna ubavu wa kuninyamazisha maana naona wewe huko kujadiliana bali kulazimisha hoja.
Mapinduzi ya Zanzibar kwa mtazamo wako yametutoa utumwani lakini kwa walio wengi hatukutegemea utumwa huu aliokuja nao huyo Nyerere wenu mnaemtukuza na kutaka kumfanya Saint. Kwamba inasherehekewa ni kweli lakini wako wengi pia wanaosikitika kuuliwa watu wao.
Sio Mansour peke yake lakini Wazanzibari walio wengi wamechoka na huu "muungano". Kama huamini, subiri kidogo tu utajua.
Mansour ni Waziri wa SMZ na wako wengi wa namna yake na ndio maana hata Dr. Shein yuko kimya.
Dawa yenu iko jikoni.
NB: NITAKUWA SAFARINI KIDOGO, USIJE UKASEMA NIMEKUKIMBIA MKUU, SIWAOGOPI NYIE CHADEMA.
Katiba inazidi msahafu, hivyo haiwezi tu kupuuzwa au kubadilishwa.
GHIBUU, nakumbuka ni Mansur huyu huyu aliyevalia njuga suala la mafuta, kwa vile najua unaelewa fika, kuhusu nguvu na jeuri ya Mhe. Mansur inakotokea mpaka kumpa ujasiri na kuzungumza kwa kiburi hoja za Muungano.
Kwa kukusaidieni tuu, yako mambo ya kujadili kuhusu muungano, na yako mambo ambayo sio ya kujadili, miongoni mwa mambo ambayo hayana mdadala, ni suala la mafuta na hili la serikali tatu.
Please mark my words, sisi bara, tumekuachieni Wazanzibari mpige kelele zote kuhusu mafuta, kwa vile mpaka sasa, mafuta hayo mnayoyapigia kelele ni yale ya kujaa kwenye kinibu tuu!, lakini ikija kukutikana Zanzibar kuna mafuta ya ukweli, ya kuchimbwa na kuchimbika, basi hao vizabi zabina wote, wanaopiga kelele, watazibwa midomo, Zanzibar si nchi, ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo mafuta ni rasilimali ya Taifa. Na hizi choko choko za kuuchokoa muungano kwa hoja za serikali tatu, zitakufikisheni pabaya, badala ya 3, tutakupeni moja, na Zanzibar itageuka mkoa wa visiwani wenye vilaya mbili za Unguja na Pemba!.
Nyie haya, endeleeni, msije kulalamika eti hamkujua, nimekwisha waambieni!.
Nashukuru Sana MM Mwanakijiji,
Mimi nataka tu niwaulize wanaotaka muungano uvunjike, Hivi wale wapemba wote walioko Dar, Tanga, na sehemu zingine wataenda wapi muungano ukivunjika? Mfano huyu Mzee wetu Mwinyi, Dr Shein ambao wana Nyumba zao huku bara watafanyaje? Mimi napata hisia kwamba wanaosema muungano uvunjwe wana maslahi binafsi. Tunaomba mikutano ya hadhara ifanyike hasa Zenji na kuwaeleza wananchi wanataka muungano wa namna gani? Na madhara ya kuvunjika kwa muungano uliodumu kwa miaka karibu hamsini.
Napata hisia kuna nguvu nyuma ya pazia inayotaka muungano huu uvunjike? na niseme tu CCM wanachangia sana kwenye hii hali inayoendelea kwa sasa, maana haiwezekani wawe wanakwepa issue za muungano kujadiliwa wakati wananchi wanataka uboreshwe.
Sioni kosa lolote hapa isipokuwa Kiitikadi! Kama mbunge wa CCM anaamini kuundwa kwa serikali tatu, nadhani kisiasa anatakiwa ajiondoe chama hicho na kwenda chama chenye malengo hayo..UCCM ni pamoja na kulinda muungano wa serikali mbili.
Mkuu hili ni swali rahisi sana. Muungano ukivunjika wazinzibar walioko bara watakuwa wageni, na wabara watakaokuwa Zanzibar watakuwa wageni pia, Kuwa na nyumba si hoja, au kuwa na biashara si hoja, nadhani Tanzania kuna biashara kwa ajili ya wageni na kwa ajili ya wenyeji, kama watakuwa wageni basi hawataruhusiwa kufanya biashara ambazo wenyeji wanaweza, kama watakuwa foreign investors itakuwa poa kabisa maana itakuwa wazi kabsa na treatment itakluwa hivyo. Same applies kwa wabara watakaokuwa visiwani.
Bila shaka wanaotaka muungano uvunjike wana maslahi binafsi, na maslahi hayo mwalimu aliwahi kuyaita ni ulevi. Lakini ulevi mtu huwa anaanamua mwenyewe kuutumia.
Sikubaliani na hoja kuwa wazanzibar peke yao ndio wajadili muungano, wabara pia tuujadili, tuna mengi ya kuuliza. Tuna haki sawa na wazanzibar kwenye muungano, na kwa bahati mbaya kwa upande fulani inaonekana kuwa we are paying for it than our isles counterparts, there should be equity in paying for it. We have lost our identity and we are losing more, to keep this Union. What we get out of it is blame that we are stoping them from begging to Arabs. Tuiulize serikali yetu nani analipa mishahara ya jeshi Zanzibar, Polisi, wabunge kutoka Zanzibar, na kama wao wanachangia kuwalipa walioko huku bara, kuna mambo mengi ya kuiuliza serikali ya muungano. Looks like it is high time kuwe na chombo kitakachowasema watanganyika, haiwezekani tuendelee kulaumiwa kila siku.
Mkuu usianze kubadilisha kauli yako wewe mwenyewe. Mimi nimekuuliza wewe nchi ambazo zimeungana na zikawa na ktk uhalali unaozungumzia wewe. Nimesema Uingereza kwa sababu ya hizo act za Union ambazo wewe una quote kama lazima baraza la mawaziri au bunge lipitishe kwa ridhaa ya wananchi. Swala hapa ni ridhaa ya wananchi na kupitishwa na hivyo vikao ili wewe uone uhalali wa Muungano. Na kama ujenisoma vizuri utaona kwamba Mapinduzi yamefanyika hakuna Bunge wala baraza la mawaziri isipokuwa mamlaka na nguvu ya maamuzi ilikuwa chini ya Baraza la Mapinduzi.. Period!Mkuu Mkandara huo mfano au mifano hio unipe wewe wa nchi mbili huru kuungana na matokeo yake yakawa Serikali mbili badala ya tatu au moja.
Mfano wa Muungano wa Uingereza hapa haufai maana kwanza Uingereza, kama ulisema hizo ni koloni zake ambazo Queen ndio Head of State na huko kwenye kolonji zake akaweka Magavana.
Labda unataka kusema kuwa Zanzibar ni koloni la Tanganyika? Lakini sishangai maana hio ndio dhana yenu.
Mapinduzi yalifanyika sio ya kuondoa Chama cha Hizbu bali coalition government iliokuwepo. Inawezekana hata hujui kuwa hata ASP ilialikwa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa lakini ikakataa. Usieyajua Mapinduzi inaelekea ni wewe maana naona umekwepa sana mambo.
Baraza la Mapinduzi ambalo lilikuwa na legislative powers halikuridhia huo "muungano" wenu. Isitoshe 'wanaochombeza' sio waliokuwa Hizbu peke yao bali ni Wazanzibari, jambo ambalo kwa fitna alizozitia Nyerere, hamkutarajia.
Hoja ya kuwa ulikuwa wakati wa Mapinduzi hapa haina mshiko maana Mapinduzi yalikwishamalizika bila ya upinzani wowote wa maana na Articles of Union zilipaswa kutekelezwa.
Mkuu Mkandara wakati umefika wa kuamua juu ya mustakabal wa "muungano", kejeli na jeuri hazifai.
Mzee kama Katiba ya sasa wameshindwa kuillinda ni kitu gani kitawafanya waitete hiyo nyingine? Kama tunashindwa hata kuwaambia watoke Bungeni sasa tutaweza vipi huko mbeleni? Nyerere aliuliza hoja hii hii kwenye UWHT.
Ilikuwa na uhalali machoni pa Nyerere ndio maana akatumia hoja hiyo ya nguvu. Lakini mwananchi ambaye hajashiriki kuipa uhalali wala haguswi na kutoilinda Katiba kunakofanywa na hao wawakilishi. Wananchi tutakaposhiriki na kujua fika kuwa ni Katiba yetu yenye uhalali tutawawajibisha.
Let them go!!!...we don't need them!Ndio maana kuna sehemu nakubaliana sana na madai ya Wazanzibar kwani sioni sababu ya bara kung'ang'ania huu Muungano ikiwa kweli tunawakandamizi Wazanzibar. na nimefanya uchunguzi mkubwa na kugundua kwamba viongozi wa Zanziar wengi ni wanafiki, wenye kutaka madaraka na wepesi wa kutumia asili zao kama sababu za kujitenga. Hakuna mwenye nia ya dhati kama Karume ambaye alisema wazi kwamba Mapinduzi yalikuwa ya kumkomboa mtu mweusi ambao walidhalilishwa na utawala wa Sultan na Washiraz waliungana na wenyeji kudai haki yao ktk nchi hiyo. Leo tunaona tena wenye asili ya KiOman na wakiwatumia Wangazija kuja dai Zanzibar ktk sura ile ya mwaka 1963 au kabla. haya ni matusi makubwa na sidhani kama wanahitaji hata kusikilizwa.
kuna wawakilishi na wabunge ambao wamekuwa wakitoa lugha ya kuonesha kuchoshwa na muungano na bila ya shaka wanazo sababu ambazo wanaamini zinawapa haki ya kutoa hisia hizo. Lakini wapo wengine kati ya hao ambao wanatoa matamshi yenye kuashiria kupigania kuvunjwa kwa muungano. Wapo wawakilishi wa vyama vyote ambao wamekuwa na kauli hizo za kutishia kuvunja muungano hasa katika bunge lililopita na hili la sasa. Ndugu zangu, hawa wawakilishi hawawezi kutoa kauli za kutaka kuvunja muungano na wakabakia wawakilishi halali wa wananchi kwani kwa kutoa kauli za kuvunja muungano wanavunja katiba iliyowaweka hapo.
1. Wawakilishi wote hawa walisimamishwa kugombea nafasi zao au kupata nafasi zao kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa ambavyo viliandikishwa kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vingi. Katiba na sheria zinakataza kabisa kuandikishwa chama chochote ambacho kinapigania kuvunja muungano. Hivyo, wote walisimamishwa na vyama visivyopigania kuvunjwa kwa muungano.
2. Kutokana na hilo la kwanza, hakuna mbunge au mwakilishi ambaye wakati anagombea aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kupigania kuvunja muungano kwa sababu au kisingizio chochote kile. Wasingeweza kufanya hivyo wakati wa kampeni kwa sababu katiba inawakataza na sheria ya uchaguzi ingewabana na kuwaengua mara moja. Kama hakuna chama kilichoandikishwa kwa ajili ya kuvunja muungano hawa wawakilishi wanapata wapi mandate ya kutoa hoja za kuvunja muungano?
3. Waliposhinda uchaguzi au kupewa ushindi wa chee waliingia bungeni/blw na kabla ya kuanza majukumu yao walishika misahafu na kuapa. Waliapa kwanza kabisa "kulinda, kutetea na kuihifadhi katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania". Ninataka kuamini kuwa walimaanisha viapo vyao. Kama walimaanisha walijifunga kuulinda muungano siyo kuuvunja. Hivyo, kauli zozote za kutishia kuvunja muungano au hata kuashiria kuwa "muungano uvunjike" ni kinyume na kiapo chao na hivyo ni kosa tosha kabisa la kumfanya msajili aidha kukifuta chama cha siasa au kumtangaza huyo mbunge/mwakilishi kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi. Huwezi kuapa kulinda katiba halafu ukasimama kutangaza kutaka kuivunja!
4. Kama 1,2 na 3 ni kweli basi wabunge na wawakilishi walioko kwenye nafasi zao sasa hawana haki, uwezo, madaraka wala mamlaka ya kuzungumzia kuvunja muungano. Yote wanayoweza kufanya ni kuutetea na kuuenzi na kuulinda.
5. Kwa vile katiba imeweka toka mwanzo kabisa (ibara ya 1,2) kuwa tanzania ni nchi moja na eneo lake ni eneo lolote la tanzania bara na tanzania visiwani na kuwa katika nchi hii moja kuna vyombo viwili vya utendaji yaani serikali ya muungano na serikali ya zanzibar kauli zozote za kubadilisha serikali hizi mbili aidha kwenda serikali moja au serikali tatu nayo ni kinyume na katiba! Wabunge hawawezi na hawapaswi kuzungumzia kubadilisha muungano kwani katiba inawakataza isipokuwa kama wametekeleza utaratibu wa katiba wa kubadili muungano. Wameapa kulinda nchi moja, serikali mbili! Ndio maana wengine tulipuuzia na kubeza kauli ya rais kikwete kuwa zanzibar ni "nchi ndani ya nchi" kwani haina mantiki na ni kinyume cha katiba!
6. Kama 1, 2, 3, 4 na 5 ni kweli basi wabunge na wawakilishi wetu wanaachiwa uchaguzi mmoja tu nao ni kutatua kero za muungano, kuondoa matatizo yaliyopo na kuboresha ili kuufanya muungano uzidi kuimarika. Hawapaswi kuudhoofisha wala kutoa kauli za kuwachochea watu kuchukua msimamo wa kuuvunja. Siyo wabunge tu wale wote walioapa kulinda katiba na hivyo kulinda muungano wanalazimishwa na katiba hiyo kuulinda muungano kwa nguvu zao zote.
Hii ina maana gani?
Kwamba, kama kuna mbunge au mwakilishi ambaye anaona kuwa muungano haufai na hataki uwepo anaachiwa uamuzi wa kutakiwa kutoka bungeni (ili asibanwe na kiapo) na kwenda kuanzisha harakati za kuvunja muungano. Na kama kundi hili linaweza kupata wafuasi basi ni jukumu lao kutumia nguvu zao zote (na hapa neno zote nalimaanisha) kupigania kuvunja muungano na kwa kufanya hivyo wajue wameamkua kupambana na vyombo vilivyopo vyenye kulinda muungano. Kama hoja yao inaweza kuwa na nguvu sana na kupata wafuasi wanaweza kujikuta hatimaye wanalazimisha muungano kuvunjika aidha kwa njia ya amani au kwa vurugu. Kwa vile muungano wetu haukuwa wa ku-annex zanzibar ni wazi unaweza kuvunjwa kwa njia ya amani kabisa. Muungano wetu siyo kama ilivyokuwa ethiopia na eritrea au sudan na sudan kusini au russia na georgia au ukraine au zilizokuwa jamhuri za yugoslavia. Tanganyika haikuivamia zanzibar na kuichukua kwa nguvu. Ulikuwa ni muungano wa hiari ambayo kusema ukweli ni vigumu sana kuuvunja licha ya majaribio ya baadhi ya watu kujaribu kuwafanya watanganyika wajisikie kama waliivamia zanzibar. Ni vigumu kuvunja muungano wa hiari.
Hivyo, wale walioapa kulinda katiba na muungano na sasa wanataka kuvunja muungano huo hawalindwi na kinga za bunge wala uhuru wa mawazo kwani mwanafamilia hawezi kuja na dumu la mafuta ya petroli na kiberiti mkononi na kuanza kudai kuwa pale nyumbani watu hawampendi na hawamjali na hivyo ameamua kuichoma nyumba moto na watu wasema ati "ni uhuru wa maoni". Pale bungeni mbunge hawezi kusimama na kupiga kelele "moto moto" halafu watu wakikurupuka kukimbia asema "analindwa na haki na kinga za bunge kusema lolote bungeni".
Waondoke kwanza bungeni na blw ili waanzishe hoja za kuvunja muungano; hawawezii kufanya hivyo wakiwa bado wamefungwa na viapo vya kuulinda muungano huo.
'Revolutionary Council of Zanzibar Approved Union with Tanganyika Yesterday and Radio Zanzibar made announcement'Makaimati;2238012]Hao Wakuu uliowataja kuwa wanajua zaidi kuhusu Mapinduzi lakini bado haiondoi kwamba BLM halikuridhia huo "muungano".
Wanaosema ni Wbar sio mimi, ninafahamu mapinduzi yalitokana na Wbar wenyewe. Kama mkono wa Nyerere upo kwanini msimpe credit kwa kuwasaidia ili hali kila mwaka mnashangilia alichosaidia Mwalimu. Tatizo la Wzbar akienda kuvua samaki na hakubahatika, atasema sababu ya Nyerere ili kuituliza nafsi yake.Unaesema Nyerere kaleta Mapinduzi ni wewe, mimi nimesema mkono wake umo