Wanaotaka tuwaonyeshe medali za Simba fainali na Stella 1993 wamezaliwa juzi, hawajui watendalo

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kuna watu wana hoja dhaifu sana, tena waandishi wa habari ndio nawalaumu ingawa wengi wao akiwemo Ally Kamwe walizaliwa juzi tu, bahati nzuri mimi ni mmoja wa vijana tulioshuhudia mechi ya fainali pale uwanja wa uhuru Simba akizamishwa mabao 2 0 na Stella Abidjan, huku Boli Zozo akiunyamazisha kabisa siku ile.

Kuna malofa waliokosa hoja wanauliza, medali za mchezo kati ya.Simba vs Stella Abidjan ziko wapi?

Jibu ni jepesi tu, nyie waandishi feki nendeni kwa Mwameja au Godwin Aswile, au Kasongo Athuman, Feruzi Telu, Malota Soma, David Mihambo, Deo Mkuki, Twaha Hamidu, Mavumbi Omary, George Lucas Gaza, Hussein Masha, Mbuyi Yondan au muulizeni Azim Dewji watawaonyesha maana mm nilishuhudia Simba akipewa medali siku ile, labda ziliwe na panya maana 1993 had Leo ni miaka 18 ss.
 
Mtu akiamua kukupinga hakosi sababu. Ukiwaonyesha medali watakuja na lingine. Waulize na wao fainali gani ya CAF wamecheza Dar wakati kombe hatujaliona?
 
Nilipoona umeandika 1993 mpaka sasa ni miaka 18 nikaacha apo apo.
 
Kumbe tupo mwaka 2011 [emoji28]
Rage apewe Tuzo
 
Kumbe wewe ni miongoni mwa Mipang'ang'a AKA Kolowizards?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Yanga ina Mashabiki mizwaro Sana. Mtu anataka klabu imuonyeshe medali wakati medali anapewa mchezaji/mtu. Ni upuuzi wa kiwango cha lami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…