Wanaotaka Urais TFF, Uchaguzi Agosti 16,2025 Jijini Tanga

Wanaotaka Urais TFF, Uchaguzi Agosti 16,2025 Jijini Tanga

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatangaza Uchaguzi Mkuu wa TFF utakaofanyika tarehe 16/08/2025 jijini Tanga.

Nafasi zinazogombewa ni Rais (Nafasi 1) na nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji (Nafasi 6)

Gharama za kuchukua fomu Nafasi ya Rais ni 500,000 na Shilingi 200,000 kwa Nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Fomu zitaanza kutolewa kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 16 hadi 20/06/2025 saa 10 kamili jioni. Fomu zinapatikana Makao Maku ya TFF na kwenye tovuti ya TFF.
View attachment 3368490
Karia kashajichimbia mizizi hang'oki leo wala kesho, mikoa yote analazimisha watu wake washinde na kafanikiwa🤣
 
Karia kashajichimbia mizizi hang'oki leo wala kesho, mikoa yote analazimisha watu wake washinde na kafanikiwa🤣
Karia kumuondoa ni mpaka itumike mbinu iliyotumika kumuondoa malinzi kwasababu ashaseti watu wake kwenye vyama vya mikoa na wilaya ambao ndio wapiga kura,,Ile mbinu iliyotumika kumnyofoa malinzi ndio inaweza kumuondoa karia na sio uchaguzi
 
Li Karia litahonga wajumbe, na litalazimisha kugombea kwa mara ya 3 mfululizo as if hakuna watu wengine wenye sifa na bora mara 100 kuliko yeye.

Na mwisho wa siku litajimilikisha shirikisho kama mali yake! Na litalindwa na mamlaka kwa sababu tu ni Liccm lenzao.
 
Karia kumuondoa ni mpaka itumike mbinu iliyotumika kumuondoa malinzi kwasababu ashaseti watu wake kwenye vyama vya mikoa na wilaya ambao ndio wapiga kura,,Ile mbinu iliyotumika kumnyofoa malinzi ndio inaweza kumuondoa karia na sio uchaguzi
Kabisa yan

Keshajimilikisha ile taasisi
 
Kwani Karia si amekaa kipindi cha oili hiki? Katiba inamruhusu kuendelea? Au katiba ya TFF inasemaje kuhusu muda wa Urais wa TFF?
Karia alibadilisha katiba akawekq miaka mitatu
 
Back
Top Bottom