Wanaotangaza vifo vya watu mashuhuri kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii wajumuishwe kwenye uhujimu uchumi, hawana nia njema na Taifa letu

Wanaotangaza vifo vya watu mashuhuri kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii wajumuishwe kwenye uhujimu uchumi, hawana nia njema na Taifa letu

Shetani kazi yake ni kuharibu, kuua na kuiba, ndivyo Biblia inavyosema. Kwa hiyo kila mahali utakapo shuhudia uharibifu, vifo na wizi, ni lazima mkono wa Shetani upo. Si ajabu kwa hiyo kwamba Shetani hufurahia matukio hayo na hufanya kila mbinu chafu ili watu waibiwe, wafe na kuwe na uharibifu.

Kumezuka siku za hivi karibuni tabia ambayo si ya kawaida na kiungwana kabisa kwa binadamu, ambayo sina shaka yeyote kwamba ina mkono wa Shetani. Tabia hii ni tabia ya kutangaza na kushabikia vifo vya watu mbali mbali, hasa wenye mamlaka au ukwasi, katika hali inayo-ashiria kwamba matangazo hayo yanafurahia vifo hivyo. Kiukweli ni Shetani tu anayeweza kufurahia kifo cha binadamu yeyote.

Ukitafakari kwa kina matangazo hayo, utagundua pasi shaka yeyote kwamba ushabiki huu wa watu kufa una misingi ya kishetani. Najua wapo watu wenye nia mbaya na taifa letu, hii ni pamoja na kuona kwamba Taifa letu linapata majanga ya kila aina,i li lisifanikiwe kwa njia yeyote ile. Makundi yenye nia hii ovu ni ya watu ambao waliigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi na hata kulifanya kuwa soko la madawa ya kulevya.

Ni vigumu hasa kuona watu hawa wanapata faida gani kwa hararaka haraka kwa kuitangazia dunia kwamba Tanzania watu wanakufa sana. Hata hivyo ukitafakari kwa kina utagundua sababu ya kushabikia vifo hivyo!

Sababu ya msingi ni Ili Tanzania ionekane kwamba ina ugonjwa wa Corona na hivyo kuharibu uchumi wa nchi yetu. Haishangazi kwa hiyo kwamba Ubalozi wa Marekani umetangaza kwamba Tanzania sio salama kutembelea, eti kwa kuwa kuna Corona wakati Marekani kwenyewe tatizo lipo, tena kubwa sana hata kuliko Tanzania. Haishangazi pia kwamba Marekani imetangaza eti nia yake ya kuisaidia Tanzania ishinde Corona wakati kwao wameshindwa! Nia ya matangazo yote haya ni ile ile, kuifanya dunia iamini kwamba Tanzania kuna Corona na hivyo kuharibu tashwira yake kimataifa na uchumi wake.

Tupo kwenye vita ya kiuchumi ambapo tumediriki hata kuanzisha mahakama za mafisadi. Hawa wanaotangaza vifo vya watu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii na forums zingine,hawana tofauti yeyote na wahuju uchumi, wawe rounded up na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Tukiwachekea tutakula mabua.
Kwa hiyo unachoelewa ni kuwa dunia inafikiri Tz haina korona? Tz iko dunia gani hata isiwe na korona? Kuingilia taasisi ya mkemia mkuu ili wasipime korona, kupiga marufuku uwekaji kumbukumbu wa walioathirika na au kufariki kwa korona, na sasa kupinga chanjo ya korona, hakuifanyi Tz isiwe muathirika wa hili janga.

Serikali inayojiweka pembeni na kuwaacha wananchi bila ya uelewa wa kinachoendelea juu ya ugonjwa, na zaidi kuwajaza wananchi fikra potofu kuwa wako salama, halafu huko vijijini, mtaani wanajikuta kila siku ni kuzikana, kila siku kuumwa mambo wasiyoyaelewa, je si kuuhujumu uchumi? Nguvu kazi inakufa, wazazi wanafariki, ilhali ilikuwa rahisi tu kuwaambia watu, vaeni barakoa, epukeni misongamano, ila serikali inafanya kinyume, viongozi ndio waitishe misongamano wakati wenyewe wanajitenga kwenye gari, jukwaani! Nani anayeuhujumi uchumi hapo?
 
Sio kosa lako mkuu,ungekuwa scientist and more specifically an independent scientist ungeshajua kwamba C-19 sio "pandemic" ni "scandemic," flawed and a hoax.You have been conned.The truth is completely the opposite of what you have been made to believe.Everything about C-19 is fake news.
 
Updates:
Rais John Joseph Pombe Magufuli akemea kitendo cha wana habari kushangilia au kushabikia vifo vya vigogo.Asema ni ukosefu wa uzalendo,utu na uungwana.Fuata link ifuatayo 👇uone taarifa kamili.

Back
Top Bottom