Wahadhiri wa vyuo vikuu vya Afrika wapo kwa ajili ya kujitapa na kujivuna kuwa wao ndio wenye akili nyingi sana. Hawataki kukuza vijana ili wawe kama wao. Ukiwa na akili, wanakundia majungu ili ufeli na usije ukalingana nao.
Katika vyuo vya wenzetu, wahadhiri wanasaidia na kukuza vijana ili waendeleze maarifa yao na nchi yao. Nashukuru sikuwahi kusoma vyuo vya kishenzi vya Waafrika weusi. Ndiyo maana Waafrika wana vyuo vingi lakini matokeo ya utendaji kazi ni sifuri.
Wahadhiri wanajiona wao ndio wao na wanatengeneza genge lao la uhalifu. Wale walioleta mapendekezo ya tafiti watakuwa mashahidi wangu. Wahadhiri wanakushambulia kwa ugomvi kama wamegundua umewakilisha mada nzuri, kwa sababu hawataki uzidi wao.
Hii ndio inafikia mahali ambapo wasomi wa Kiafrika hawaaminiki, hadi raslimali zetu zinaendeshwa na wageni toka nje waliofeli kidato cha nne. Hivi maprofesa wetu wameshindwaje kuendesha bandari, mwendo kasi, madini, T.R.A, gesi, maliasili, misitu, maji bahari, maziwa na mito, umeme, miundombinu, na usafirishaji nk.
Wao wapo kuchekelea kufelisha wanafunzi tu. Waafrika ngozi nyeusi ni kama wana laana sababu ya hao maprofesa uchwara. Maprofesa wa kusubiri mshahara, ugunduzi ni sifuri asilimia. Sasa hivi maprofesa wetu wanakimbilia kufanya kazi za siasa na uchawa tu, na kuhama vyama vya siasa. Hadi nchi inauzwa wapo kimya kwa sababu ya njaa ya mshahara wa milioni tatu, ukiweka makato wanabaki na milioni moja na nusu. Hadi toothpicks tunaagiza nje.
Ni aibu sana kujiita Profesa kwenye nchi zetu. Profesa umegundua nini cha kuisaidia jamii yako? Eti ni Profesa wa kusahihisha mitihani tu. My foot. My mouth.