Wanaotumia ving’ora kwenye magari na pikipiki bila ruhusa, faini Tsh. 300,000 au kifungo hadi Miaka 3

Wanaotumia ving’ora kwenye magari na pikipiki bila ruhusa, faini Tsh. 300,000 au kifungo hadi Miaka 3

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Serikali ya Tanzania imetangaza kanuni mpya zinazopiga marufuku ufungaji na matumizi ya ving’ora na taa za ishara (beacon lights) kwenye magari binafsi bila kibali maalum, kufuatia kuongezeka kwa kero na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa barabara nchini kote.

Kanuni hizo, zinazojulikana kama Kanuni za Sheria ya Usalama Barabarani (Ving'ora, Ishara za Sauti, Filimbi na Taa za Mawasiliano) za Mwaka 2026, zilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Juni 19, 2026, chini ya Sheria ya Usalama Barabarani (Sura ya 168), na zimejipatia umaarufu mkubwa baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Agosti 13, 2026.

Akitoa maelekezo kuhusu sheria hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amebainisha kuwa matumizi ya ving’ora na taa za dharura sasa yamezuiliwa na kutengwa maalum kwa ajili ya magari ya dharura pekee pamoja na makundi saba ya viongozi wakuu wa kitaifa. Chini ya kanuni hizi mpya, mtu yeyote atakayefunga au kutumia vifaa hivyo bila kibali rasmi cha waziri atakuwa ametenda kosa la jinai na atakabiliwa na adhabu ya faini ya hadi Shilingi 300,000 au kifungo gerezani.

Hatua hii imekuja ili kukabili tabia inayokua kwa kasi miongoni mwa madereva—wakiwemo wanaoomba na kuendesha magari binafsi ya kifahari (SUVs), mabasi ya mikoani, malori ya biashara, bajaji na pikipiki—ambao wamekuwa wakifunga vifaa hivyo kiholela ili kukwepa foleni au kukwepa ukaguzi wa Jeshi la Polisi.

Mbali na kero za barabarani, maafisa usalama wamebainisha kuwa taa hizo za dharura zimekuwa zikitumiwa na baadhi ya wahalifu kama kivuli cha kusafirisha mizigo haramu, ikiwemo mirungi, kupitia vituo vya ukaguzi kwa kujifanya wanasafirisha viongozi na wageni waasi wa serikali.

KANUNI MPYA ZA UDHIBITI WA VING’ORA VISIVYO RASMI, TAA ZA VIMULIMULI KUANZA KUNG’ATA

Serikali imechapisha katika Gazeti la Serikali, Kanuni mpya za Udhibiti wa Ving’ora na taa za vimulimuli, kwenye magari barabarani.

Kanuni hizo zinajulikana kama Sheria ya Usalama Barabarani (Kanuni za Ving’ora, Ishara Zinazosikika, Filimbi na Vimulimuli) za 2026, Tangazo la Serikali Na. 151 la tarehe 19/6/2026, yaani THE ROAD TRAFFIC (SIRENS, AUDIBLE SIGNALS, WHISTLES AND FLASHING BEACONS) REGULATIONS, 2026, Government Notice No. 151 Published On 19/6/2026.

Katika mfululizo wa Makala hizi, tutakuletea sehemu ya Kwanza ya Makala itakayoangazia matumizi ya Kanuni na misafara inayoruhusiwa kuwa na ving’ora na Vimulimuli.

Matumizi ya Kanuni

Kanuni hizo zitatumika kwa magari rasmi ya Viongozi na magari ya dharura yaliyoidhinishwa.

Use of Siren,Audible signal,Whistle, and Flashing Beacons

Kwa mujibu wa Kanuni, ving’ora na taa za vimulimuli zitatumika kwenye magari ya Viongozi yafuatayo:

(a) Kwa upande wa Msafara wa Rais, Msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za rangi Nyekundu na Nyeupe pamoja na king’ora cha sauti;

(b) Kwa upande wa Msafara wa Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar, msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za rangi Nyekundu na nyeupe na king’ora cha sauti;

(c) Kwa upande wa Msafara wa Waziri Mkuu, Naibu Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zinazowaka za njano (amber) na nyeupe na king’ora cha sauti;

(d) Kwa upande wa msafara wa Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Naibu Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi, Msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli/bikoni zenye mwanga wa Bluu na Mweupe pamoja na King’ora cha Sauti;

(e) Kwa upande wa msafara wa Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, msafara utakuwa magari yenye kimulimuli/bikoni zenye mwanga wa Bluu pamoja na King’ora cha sauti, wakiwa katika kazi zao za kiofisi.

(f) Kwa misafara ya ma-Rais wastaafu. Msafara utakuwa na magari yenye ving’ora vya sauti na taa za ukungu (fog lights) bila kimulimuli.

Haya ndiyo Makundi sita yanayostahili kuwa na vimulimuli na ving’ora.

Sasa wewe mwenzangu na mimi, mtumishi wa serikali sijui mkuu wa nini, unaweka kimulimuli kwenye Kirikuu yako, IST au hata kama ni hilo benzi lako kwa sheria ipi? Sheria ndio imeshatoka sasa.

Hata DC tu hayumo kwenye orodha, wewe je?

Kwa mujibu wa Kanuni ya 7, mtu yeyote haruhusiwi kufunga king’ora, ishara ya sauti, filimbi au kimulimuli kwenye gari isipokuwa tu kama amepata idhini ya Waziri mwenye dhamana itakayotolewa chini ya Kanuni hizi.

Kwa mujibu wa kanuni ya 9, yeyote atakayekiuka au kukaidi Kanuni hizi atakuwa anatenda kosa na adhabu yake ni kati ya shilingi 50,000 na 300,000 au kifungo kisichopungua miezi 6 na kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja.

Kuchapishwa kwa kanuni hizi kwenye Gazeti la serikali, kuna maana kwamba muda wowote kuanzia zilipochapishwa askari sasa wanaweza kusimamisha gari lolote na kukagua iwapo lina King’ora na kama king’ora hicho kimeruhusiwa au wanaweza kusimamisha gari lolote na kujiridhisha iwapo lina ruksa ya kuwa na king’ora au kimulimuli, kama hakuna ruksa hiyo ni adhabu.

Ndugu zangu neno “gari” hapa ni pamoja na boda boda na bajaji, kwa hiyo usijitoe ufahamu.

Serikali imechapisha katika Gazeti la Serikali, Kanuni mpya za Udhibiti wa Ving’ora na taa za vimulimuli, kwenye magari barabarani. Kanuni hizo zinajulikana kama Sheria ya Usalama Barabarani (Kanuni za Ving’ora, Ishara Zinazosikika, Filimbi na Vimulimuli) za 2026, Tangazo la Serikali Na. 151 la tarehe 19/6/2026, yaani THE ROAD TRAFFIC (SIRENS, AUDIBLE SIGNALS, WHISTLES AND FLASHING BEACONS) REGULATIONS, 2026, Government Notice No. 151 Published On 19/6/2026.

Katika mfululizo wa Makala hizi, tutakuletea sehemu ya pili ya Makala itakayoangazia matumizi ya Ving’ora na vimulimuli kwa Wageni wa heshima wanaoitembelea nchi na Magari ya dharura yaliyoruhusiwa kutumia ving’ora na vimulimuli.

Matumizi Ya Ving’ora na Vimulimuli kwa Wageni wa Heshima Wanaoitembelea Nchi

Kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1) Matumizi ya ishara zinazosikika na vimulimuli kwa magari ya msafara wa Kiongozi anayeitembelea nchi yataelekezwa na Waziri mwenye dhamana kwa kushauriana na Wizara yenye dhamana ya mambo ya nchi za nje na vyombo vya ulinzi na usalama, kwa kuzingatia renki ya Kiongozi husika, sababu ya ziara na itifaki ya kidiplomasia.

Bila kuathiri kanuni ndogo ya kwanza, viwango vifuatavyo vitatumika kwa ziara rasmi za wakuu wa nchi:

(a) Kwa ziara ya Mkuu wa nchi, msafara utakuwa na magari yenye kimulimuli cha rangi nyekundu na nyeupe na king’ora cha sauti;

(b) Kwa ziara ya Mkuu wa serikali, magari ya msafara yatakuwa na kimulimuli cha rangi nyekundu, nyeupe na bluu, pamoja na king’ora cha sauti;

(c) Kwa ziara inayomhusu kiongozi mwingine yeyote wa heshima, aina ya kimulimuli na king’ora kitakachotumika, vitakuwa kadiri ya maelekezo ya Waziri mwenye dhamana, kwa kuzingatia hadhi ya kiongozi, sababu za ziara na itifaki ya kidiplomasia.

Magari ya Dharura Yaliyoidhiniwa

Kwa mujibu wa kanuni ya 6, matumizi ya ving’ora, filimbi au vimulimuli kwa magari ya dharura, yatakuwa kama ifuatavyo:

(a) Magari ya Polisi au pikipiki zinaweza kufungwa mchanganyiko wa vimulimuli, ving’ora au filimbi kama itakavyotakiwa kulingana na aina ya msafara au dharura;

(b) Magari ya Jeshi au vyombo vya ulinzi, yanaweza wakati wa dharura, kufungwa vimulimuli vya rangi nyekundu na bluu pamona ving’ora kulingana na aina ya dharura;

(c) Magari ya wagonjwa, zimamoto na uokoaji, au mengine yaliyoidhinishwa yanaweza kufungwa bikoni za duara zenye rangi nyekundu pamoja na ving’ora kulingana na aina ya dharura.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 7, mtu yeyote haruhusiwi kufunga king’ora, ishara ya sauti, filimbi au kimulimuli kwenye gari isipokuwa tu kama amepata idhini ya Waziri mwenye dhamana itakayotolewa chini ya Kanuni hizi.

Kwa mujibu wa kanuni ya 9, yeyote atakayekiuka au kukaidi Kanuni hizi atakuwa anatenda kosa na adhabu yake ni kati ya shilingi 50,000 na 300,000 au kifungo kisichopungua miezi 6 na kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja.

Kuchapishwa kwa kanuni hizi kwenye Gazeti la serikali, kuna maana kwamba muda wowote kuanzia zilipochapishwa askari sasa wanaweza kusimamisha gari lolote na kukagua iwapo lina King’ora na kama king’ora hicho kimeruhusiwa au wanaweza kusimamisha gari lolote na kujiridhisha iwapo lina ruksa ya kuwa na king’ora au kimulimuli, kama hakuna ruksa hiyo ni adhabu. Ndugu zangu neno “gari” hapa ni pamoja na boda boda na bajaji, kwa hiyo usijitoe ufahamu.

Makala ya Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania (RSA Tanzania)
 

Attachments

Back
Top Bottom