Wakati Wananchi wenzetu wa maeneo mbalimbali wakilalamika adha ya kukosa huduma ya maji, huku kwetu Wakazi wa Mbezi Makabe hadi Msumi hali siyo nzuri na ni kama tumeshazoea hali hiyo.
Tunapata adha ya kukosa maji japokuwa tuna mabomba ya DAWASA, Maji yanaweza yasitoke hata wiki tatu bila maelezo yoyote na yakitoka yatatoka baadhi ya maeneo tu.
Ajabu hayo maji ya DAWASA ambayo hayatoki kwetu kuna magari yanakimbizana kutuuzia maji hayo ya DAWASA, Dumu la Lita 1,000 tunauziwa kwa kwa Tsh. 15,000/= hadi 20,000/=
Swali la msingi tunalojiuliza wengi wetu hawa wanaouza maji ya DAWASA wanayapata wapi kwa wingi huo na kwanini sisi hatupati?
Hii kero tunaomba Serikali itusaidie maana imekuwa ya miaka mingi, hata Watu kudhani DAWASA wanakata maji ili hao Wafanyabiashara ya maji wapate fursa ya kufanya biashara yao.